Evarist Chahali
JUMAMOSI Februari 2 mwaka huu itabaki katika kumbukumbu zangu kwa muda mrefu, pengine katika uhai wangu wote.Majira ya saa 3 asubuhi nilikurupushwa usingizini na kelele za mlango uliokuwa ukigongwa kwa nguvu. Wakati ninajiandaa kwenda kufungua mlango, nikasikia sauti yenye dharura ikisema, “bwana Chahali, polisi hapa, tafadhali fungua mlango.”
Nilichanganyikiwa kwani tangu nifike nchi hii zaidi ya miaka 10 iliyopita sijawahi kufanya kosa lolote au kukwaruzana na vyombo vya dola/sheria. Baada ya kufungua mlango, askari waliovalia kiraia walijitambulisha na kuonyesha vitambulisho vyao. Pia walinisihi kuwa nisiwe na hofu ya kudhani kwamba nimefanya kosa lolote.
Kwa kifupi, walinieleza kuwa wamepewa ujumbe kutoka moja ya taasisi za intelijensia za hapa kuwa kuna tishio la uhakika dhidi ya maisha yangu. Hata hivyo, walieleza kuwa kwa vile wao walipewa tu ujumbe huo na kutakiwa kuuwasilisha kwangu, hawakuwa na maelezo ya ziada. Walisisitiza kuwa nichukue tahadhari muhimu na kunipa maelekezo ya mawasiliano ya dharura.
Kwa vile nilikurupushwa usingizini, awali taarifa hiyo ilionekana kama ndoto iliyokuwa inaendelea hata baada ya kutoka usingizini. Ilinichukua takriban saa tatu kuzinduka kutoka katika mshituko huo, na kutambua uzito wa taarifa niliyopewa na polisi hao.
Nikaamua kwenda kituo kimoja cha polisi kupata ufafanuzi zaidi. Mara baada ya kujitambulisha, mazingira ya namna suala hilo lilivyokuwa likishughulikiwa kituoni hapo lilinipa picha kuwa jambo hilo lina uzito. Kwa kifupi, baada ya kitambo nilipewa ufafanuzi ambao haukutofautiana na maelezo niliyopewa awali na polisi walionitembelea katika makazi yangu.
Kikubwa ni kuwa taarifa hiyo ilionyesha kuwa tishio hilo dhidi ya maisha yangu linatokea huko nyumbani. Swali linaloendelea kunisumbua kichwa ni KWA NINI iwe hivyo.
Wakati si vigumu kwangu kuhisi wahusika wa mpango huo wa kijahili, napata shida kuelewa kwanini wahusika hao watumie fedha za walipakodi kuandaa operesheni ya kutaka kunidhuru ilhali ninaamini kwa asilimia 100 kuwa mimi si tishio kwa usalama wa Taifa letu.
Ndiyo, baadhi ya ninayoandika kwenye makala zangu na tweets zangu huko kwenye mtandao wa kijamii wa twitter yanaweza kuwachukiza baadhi ya watu, lakini kwa hakika kuchukizwa huko si sababu ya kutaka kunidhuru.
Hadi wakati ninaandika makala hii nimekuwa nikiishi kwa tahadhari kubwa. Faraja kubwa kwangu inatokana na sababu tatu za msingi. Kwanza, kwa vile nilizaliwa na kukulia katika familia inayomtanguliza Mungu katika kila jambo, nina imani kubwa kuwa mamlaka pekee kuhusu uhai wangu (yaani kuwa hai au kufa) ni Mungu pekee. Hakuna mwanadamu anayeweza kupora jukumu hilo la Mungu na kufanikiwa kufupisha uhai wa yeyote.
Pili, nina imani kubwa na taasisi za usalama za hapa Uingereza. Kimsingi, wenzetu hawa wanathamini sana usalama na uhai wa binadamu pasi kujali mhusika ni mzaliwa wa hapa au ni ‘mgeni’ kama mimi. Ushauri na sapoti ninayoendelea kupata inanipa matumaini makubwa kuwa nipo kwenye ‘mikono salama.’
Lakini tatu ni ukweli kwamba takriban miaka mitano sasa nimekuwa nikiishi na uelewa kwamba kuna baadhi ya watu huko nyumbani wanaoniona kama kimelea cha maradhi hatari ambacho kikiachwa bila kudhibitiwa kitazua balaa.
Kwa sababu hiyo, tangu wakati huo nimekuwa nikiishi kwa tahadhari japo si kubwa kama hii ninayolazimika kuichukua sasa. Lakini ili uweze kuchukua tahadhari ni lazima uwe na mbinu na ujuzi wa kuchukua tahadhari husika. Kwa bahati nzuri, watu hao wanafahamu fika kuwa nina ujuzi wa kutosha na kuelewa na kumudu fika mbinu za kuishi kwa tahadhari.
Hata hivyo, kumudu mbinu ni suala moja na kuishi kwa kutumia mbinu hizo ni kitu kingine. Si jambo la kupendeza hata kidogo kuishi ukiwa na uelewa kuwa siku moja, mahala fulani unaweza kukumbana na madhara fulani. Lakini kadri unavyolazimika kuishi kwa namna hiyo inakuwa kama sehemu muhimu ya maisha yako, na ndivyo ilivyo kwangu.zaidi soma hapa
Kama ulivosema hapo juu kwamba:- nukuu "Faraja kubwa kwangu inatokana na sababu tatu za msingi. Kwanza, kwa vile nilizaliwa na kukulia katika familia inayomtanguliza Mungu katika kila jambo, nina imani kubwa kuwa mamlaka pekee kuhusu uhai wangu (yaani kuwa hai au kufa) ni Mungu pekee. Hakuna mwanadamu anayeweza kupora jukumu hilo la Mungu na kufanikiwa kufupisha uhai wa yeyote." mwisho wa nukuu Mungu atakulinda tu, pole sana kakangu.
ReplyDeleteChahali kwanini husemi ukweli kuwa unatafuta namna ya kujilipua ubaki ughaibuni? Nani akufuate kukua wewe na wasifanye hivyo ulipokuwa Tanzania kwenye msiba wa mama yako? Sioni mantiki yoyote zaidi ya kutumia mwanya huu kutafuta jinsi ya kuendelea kuganga njaa yako huko Uingereza. Karibu nyumbani hakuna atakayekuua. Ingekuwa ni kuua watu ambao ni mwiba kwa maslahi ya hao unaowashuku nadhani walengwa wanajulikana. Swali dogo tu. Hivi wewe ndiye mtanzania anayeishi ughaibuni? Uuawe kwa lipi bwana mdogo wangu? Nadhani hao waingereza nao wajinga umewaingiza mkenge. Kumbe mchezo wa wanaijeria unatumiwa na watanzania!
ReplyDeleteAcha utoto bwana mdogo. Tueleze nani hao au huyo anayetishia maisha yako. Kama mambo yamekuwia magumu na unashindwa la kufanya basi jiunge CCM kama wengi wenzako walioko ughaibuni angalau ukirudi huenda unaweza kupata kibarua.
Bwana Anonymous, kama una wasaa jaribu kuwasiliana na MaryhillandKelvinCommunityPolicingTeam@strathclyde.pnn.police.uk labda itasaidia kukuaminisha tofauti. Lakini pengine kabla ya kukurupuka na theories zako ungenitendea haki kwa kuulizia residential status yangu hapa UK. Hata hivyo, ni vema ukatambua kuwa hawa Waingereza sio mazuzu kamaunavyofikiria.Anyway, sikuandika makala hiyo kusaka simanzi za mtu yeyote, na mwenye mtizamo tofauti na dhima ya makala hiyo yupo huru kutafsiri atakavyo.
ReplyDeleteBwana Chahali pole sana. Nakushauri usihadaike na hao wanaotaka kukupaka matope. Usishangae huyo Anonymous anayetapika na kunya kwa mdogo-ashakum si matusi, akawa ni miongoni mwa hao wanaotumwa na mabwana zao kutaka kukudhuru. Ni aibu kwa mijitu mizima kutumika kama vifaa kutetea uoza. Hata hivyo, hao washenzi na wauaji ni woga na hawatafanikiwa kutekeleza jinai yao kwenye ardhi ya Uingereza. Ila chunga kama utatokea kuingia Tanzania,usitangaze wala kutembelea sehemu ambazo wanajua wanaweza kukupata.
ReplyDeleteKimsingi unachofanyiwa licha ya kuwa unyanyasaji ni ushahidi kuwa utawala wetu umeishiwa kulhali so to speak.
Nakushauri ujione sasa umekuwa katika mapambano. Ulikuwa mtoto baadaye ukawa kijana katika mapambano. Sasa umepitia jando la mapambano. Kawaida mapambano hukufanya uwe na wapenzi na maadui wengi. If anything what is happening is your baptism by fire. Chukua kila tahadhali na uendelee kunoa kalamu yako. Ingawa umesema kuwa unaamini kuwa uhai au ufu wa mwanadamu uko mikononi mwa Mungu, sikubaliani nao. Ndiyo maana amri ya sita inasema USIUE. Hii maana yake ni kwamba binadamu wanaua. Ndiyo maana hakuna amri inayosema usiumbe. Bwana mdogo na rafiki yangu nakushauri uwe makini. Ila mpambano uendelee tena kwa ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya. Inshallah mwenyezi Mungu akulinde na kuzidi kukupa ithibati ya kuendeleza mapambano.
Asante sana dada Yasinta na Mr Mhango
ReplyDeletehaya ashaingia na matusi mwalimu mahando hapa tunatumia lugha safi mheshimuwa
ReplyDelete