Wednesday, December 12, 2012

NIMEUPENDA UBUNIFU HII ...AKILI NI MALI KILA MTU ANA ZAKE/USITUPE VIZIBO VYA BIA/SODA NI MALI!!!

Mwaka jana nilipita Mikumi katika maduka waozayo mambo ya urembo na vitu vingine..Nilishikwa na mshangaO baada ya kuona hizi heleni zilizotengenezwa na vizibo vya sodana bia (visoda). Nilipenda sana ubonifu wao na binti yangu akaniambia twaweza pia kufanya kazi hiyo kwa mikono yetu. Lakini, kumbe si kazi rahisi. Nawasifu watu waliofanya kazi hii kwa mikono yao. kunywa soda au bia yako na vizibi ( visoda ) usitupe ni mali... NAWATAKIENI WOTE SIKU HII YA JUMATANO IWE NJEMA SANA NI SIKU MAALUMU MAANA NI TAREHE 12-12-12..KILA LA KHERI!!!

7 comments:

  1. siku hizi hakuna kutupa tupa vitu......ubunifu unazidi kukua...safi sana.......nawe pia siku njema

    ReplyDelete
  2. Ni ubunifu mzuri,lakini ubora wa visoda hivyo uko je katika mwili wa binaadamu(kwa afya). nimependa tarehe ya leo,12/12/2012. siku njema kwako pia.kaka s

    ReplyDelete
  3. Je vigezo na masharti ya bidhaa za urembo yamezingatiwa katika ubunifu huu?

    ReplyDelete