Tuesday, November 27, 2012

MTAZAMO WA MAISHA YA ZAMANI NI TOFAUTI KABISA NA MAISHAYA SASA!!!

Habari hii nimetumiwa na msomaji wa Maisha na Mafanikio nami nimeipenda na nimeona nisiwe mchonyo pia ni vema kujadili kwa pamoja...pamoja daima...
---------------------------------------------------------------------------------------------------------
Kwanini nasema hivyo:-  Nasema hivi nikiwa na maana yake, ni kwamba  zamani maisha yalikuwa mazuri na mepesi na yenye khekima kwa wakubwa na wadogo. Vyakula vilikuwa vingi pesa ilikuwa ina thamani. Ikiwa na maana watu waliishi kwa mapenzi mema tena sana. Watoto wakike walifundishwa jinsi ya usafi, kupika, kujiepusha na vitu vya anasa na kadhalika. Na pia wazee waliwapenda wajukuu wao. Wakati wa jioni walikaa nao wakiota moto wakiwa wanawasimulia hadithi nzuri ambazo zilikuwa na mafunzo na pia watoto waliburudika sana. Pamoja na kuwa palikuwa na uhaba wa huduma za jamii ila watu waliishi kwa kula vyakula asilia, na kutumia dawa za miti shamba....,,, Namalizia kusema MAISHA YA ZAMANI YALIKUWA NI BORA KULIKO YA SASA!!! Napenda kusema tena:- Maisha ya kisasa ni tofauti na zamani kwanini nasema hivyo. Maana yake siku hizi watu sio vijana sio wazee wanapenda mambo ya kisasa NA PIA YA KUIGA. Utakuta  wanavaa mavazi tofauti na zamani, wanapenda anasa sana kuliko vitu vinginne, hawapendi kukaa na watoto wao kama wazee wa zamani, hawapendi vitu asilia....! Je? Kuna ukweli kuwa  maisha ya zamani ni bora? KILA LA KHERI!!!!

5 comments:

  1. @Yasii;
    Hii imebeba ukweli mtupu!!

    ReplyDelete
  2. Kaka Ray! ila kwa nini sasa twapenda sana kuiga vya wenzetu?

    ReplyDelete



  3. Inaktivera för: swahili









    Hakika kuna ukweri kabisa maisha ya zamani ni bora zaidi kuriko ya sasa, Make nasababu nyingi ya kutetea hiyo mada. Sababu ya kwanza watu waliishi miaka mingi tofauti na sasa, watu walikuwa wanamaadiri mema tofauti na sasa, watu walikuwa awauguwi ovyo kama sasa, watu walikuwa wananguvu kuliko watu wa sasa, ugonjwa wa ukimwi aukuwepo, watu walikuwa wanakula vyakula asilia tofauti na sasa, akika maisha ya zamani ni bora zaidi kuriko ya sasa ukweli utabaki palepale, ushauri TUACHE KUIGA TUNAPOTEA KABISA

    ReplyDelete
  4. maisha ya kale weachatu ingekuwa hiari yangu tungerudisha hayo ya zamani maana watu wote walikuwa na upendo,kuaminiana,kushirikiana na hata mtoto ulikuwa ukikanywa unakanyika sio sasa hivi imekuwa tabu.zamani babu alikuwa halichakula bila kuwa na wajukuuzake na ilkuwakosa kwayule ambaye atamzuia mtoto kwenda kula na babu yake na hata ambaye alikuwa hakujaliwa kupata mtoto lakini bado naye alikuwa na upenda na watoto wandugu zake,hivyo basi ulikuwa upendo mwanzo mwisho lakini sasahivi watu ikifika wakati wa kula watu wanafunga mlango,na hiiyote ndio ilikuwa inachangia watu kutokupata maradhi ya hovyo maana mtu ukiwa naupendo hata stress huna.lakini sasa hivi umuweke hata nduguyo kweshughuli furani ataiharibu eti utawaringia au mfano unajenga mwachie nduguyo kukusimamia atashirikiana na mafundi kukuibia sementi yaani imekuwa tabu sana

    ReplyDelete
  5. kingine kinachotuponza kuiga vitu visivyo namsingi,tumeacha utamaduni wetu,watu sikuhizi hatakama mtu anozesha hawatakikupiga ngoma zetu za asili eti vimepitwa na wakati yaani tabu tupu

    ReplyDelete