Friday, October 12, 2012

IJUMAA YA LEO NGOJA TUWATEMBELEE NDUGU ZETU WACHAGGA NA NGOMA YAO HII YA JADI/ASILI!!!


Ni ngoma ya kabila la Wachagga kutoka katika Wilaya ya Arusha wakicheza ngoma ya Jadi/asili.....IJUMAA NJEMA NA MWISHO WA JUMA UWE MWEMA KWA WOTE!!!!!!

7 comments:

  1. Nimeipenda ngoma hii ingawa sielewi wanasema nini kwangu hiyo midundo na jinsi ya kucheza ni raha mno...uasili ni mtamu.Wachagga oooyyeeee!!

    ReplyDelete
  2. UNAPOTAJA JINA KILIMANJARO KWA HAKIKA UNATAJA TANZANIA KUTOKANA NA UMAARUFU WA MLIMA KILIMANJARO AMBAO NI MAARUFU KULIKO YOTE AFRIKA.NGOMA KUBWA YA ASILI YA WACHAGGA NI IRINGI.IRINGI HUCHEZWA KATIKA MDUARA HUKU WATU WAKIWA WAMESHIKANA MIKONO IKIWA NI ALAMA YA UPENDO NA MSHIKAMANO WA KIFAMILIA.UPO UTANI KUWA ZAMANI NGOMA HIYO ILICHEZWA BILA KUSHIKAMANA MIKONO LAKINI BAADAE WATU WALIJIKUTA MIFUKO YAO MITUPU.WAZEE WA KIMILA WAKAAMUA KUONDOA UTATA KWA KUWEKA AMRI YA KUSHIKANA MIKONO WA KUCHEZA NGOMA HIYO.WACHAGGA WANAISHI KWENYE WILAYA NNE ZA MKOA WA KILIMANJARO AMBAZO NI SIHA;HAI;MOSHI NA ROMBO KWA MPANGILIO UFUATAO:

    -----------------------------------

    1.WASIHA

    2.WAMACHAME [ WILAYA YA SIHA NA HAI]

    3.WAMASAMA

    -----------------------------------

    4.WAKINDI

    5.WAKIBOSHO

    6.WAURU

    7.WAOLDMOSHI

    8.WAMBOKOMU [ WILAYA YA MOSHI ]

    9.WAKIRUA

    10.WAKILEMA

    11.WAMARANGU

    12.WAMAMBA

    13.WAMWIKA

    -----------------------------------

    14.WAKENI

    15.WAMKUU

    16.WAMASHATI [ WILAYA YA ROMBO ]

    17.WASSERI

    18.WANGASA

    ReplyDelete
  3. Nimeona hii juhudi ya kutafuta ngoma ya Wachagga inapaswa kupongezwa sana.
    Lakoni sisi Wachagga tunatokea Kilimanjaro Walaya za Rombo,Moshi Vijijini,Siha, Hai na Moshi Mjini kwa kiasi.Watani zetu ni Wapare wanapatikana kwa wingi Wilaya ya Same na Mwanga.Ni kuweka historia/kumbukumbu vizuri.

    ReplyDelete
  4. Ngoma ya Wachaga"Iringi"Asante sana kiongozi.

    ReplyDelete