Friday, September 7, 2012

PALE HALI YA HEWA INAPOBADILIKA /UPWEKE UNAINGIA PIA!!!

 Sasa ndio ule wakati baridi inaanza kunyemelea. Kama uonavyo katika picha majani siyo ya kijani tena isipokuwa ni njano njano. Höst "majira baridi ya kuputika majani"na baada ya hapa kutakuwa na baridi zaidi theruji..brrrrriii. Na sasa  kwa watu waliozoea kujichanganya  ni ngumu sana hakuna mtu/jirani anaonekana nje. Kaaazi kwelikweli..NIWATAKIENI MWISHO WA JUMA MWEMA..TUKISHIRIKIANA/UNGANA TUTAFANIKISHA TU.

9 comments:

  1. Wakati Jua Halichomozi

    NA MWANDISHI WA AMKENI! NCHINI FINLAND

    “JUA hutoka, jua hutua; huenda zake lirudie mahali litakapotokea tena,” inasema Biblia. (Mhubiri 1:5, Verbum Bible) Lakini kuanzia katikati ya Novemba hadi mwisho wa Januari, huenda kukawa na mabadiliko katika macheo na machweo katika maeneo mengi kaskazini mwa Mzingo wa Aktiki. Katika maeneo hayo inawabidi watu wavumilie usiku mrefu wa Aktiki katika majira ya baridi kali.

    Kwa kiwango kidogo, maeneo yaliyo kusini mwa Mzingo wa Aktiki yanakuwa na usiku mrefu pia. Kwa mfano, mwangaza wa jua huonekana tu kwa saa sita hivi katika majira ya baridi kali huko St. Petersburg, Urusi; Helsinki, Finland; Stockholm, Sweden; na Oslo, Norway, majiji yaliyo umbali wa kilomita 800 hivi kusini mwa Mzingo wa Aktiki.

    “Wazo la kwamba majira ya baridi kali katika maeneo ya Aktiki huwa na giza tititi si kweli,” anasema Ari, aliyelelewa huko Kiruna, Lapland ya Sweden. Sehemu kubwa ya siku inaweza kulinganishwa na machweo. Paula, msanii anayeishi kwenye Lapland ya Finland, anasema, “Wakati Lapland imefunikwa kwa theluji, rangi hugeuka na kuwa bluu na zambarau.”

    Watu fulani huathiriwa na giza la majira ya baridi kali. “Ninaathiriwa sana na mabadiliko ya majira na hali ya hewa,” akaandika Jean Sibelius, mtungaji maarufu kutoka Finland. Aliongezea hivi: “Katika majira ya baridi kali, wakati mchana ni mfupi, mimi hufadhaika.” Mbali na Sibelius, watu wengine pia wamefadhaishwa na giza la majira ya baridi kali. Hata mwanafizikia Mgiriki Hipokrati (mnamo 460-377 K.W.K.) aliamini kwamba majira huathiri hisia za watu.

    Hata hivyo, kufikia miaka ya 1980 ndipo mfadhaiko unaotokea wakati wa majira ya baridi kali ulipofafanuliwa kuwa ugonjwa. Uchunguzi umeonyesha kwamba asilimia ndogo kati ya watu wanaoishi katika maeneo yanayoathiriwa na majira hayo wanaugua ugonjwa wa majira ya baridi kali (SAD). Watu wengi zaidi wanaathiriwa na aina fulani ya ugonjwa huo ambayo si mbaya sana. Inaaminiwa kwamba mamia ya maelfu ya watu wanaathiriwa kwa kiwango fulani.

    Andrei, anayeishi huko St. Petersburg, Urusi, anasema, “Ninahisi usingizi kila wakati.” Annika, anayeishi Finland, anahuzunika majira ya baridi kali yanapokaribia. “Wakati mwingine,” anasema, “giza hunifanya niwe na wasiwasi mwingi kana kwamba nimefungiwa katika sehemu isiyo na nafasi kubwa bila njia ya kutokea.”

    Wataalamu wanapendekeza njia mbalimbali za kukabiliana na mfadhaiko unaotokea wakati wa majira ya baridi kali. Kwa mfano, baadhi yao hupendekeza kwamba mtu anapaswa kukaa nje kwa kipindi kirefu iwezekanavyo kunapokuwa na mwangaza wa jua. Wale wanaofanya kazi nje wakati wa mchana wanasema kwamba hawaathiriwi na mfadhaiko unaotokea wakati wa majira ya baridi kali.

    Jarmo, ambaye amekabiliana na majira ya baridi ya baridi kali kaskazini na kusini mwa Finland anasema, “Kunapokuwa na giza zaidi, tunatumia mishumaa mingi zaidi na kuwasha taa nyingi zaidi.” Baadhi yao wamepata nafuu kwa kupata matibabu ya kumulikwa kwa mwangaza mwingi. Wengine huepuka giza linalotokea wakati wa majira ya baridi kali kwa kwenda likizo katika nchi zenye joto. Hata hivyo, wengine huonya kwamba baada ya watu kutoka likizo kwenye eneo kama hilo, huenda wafadhaike zaidi wanaporudi kwenye giza la majira ya baridi kali.

    Ni muhimu pia kula vizuri. Kwa kuwa jua husaidia mwili kutokeza vitamini D, kukosa mwangaza wa jua kunaweza kufanya mwili uwe na upungufu wa vitamini hiyo. Hivyo, watu fulani wanapendekeza kwamba watu wale vyakula vingi vyenye vitamini D kama vile, samaki, maini, na vitu vinavyotokana na maziwa.

    Mambo yaleyale yanayofanya kuwe na giza wakati wa majira ya baridi kali pia hufanya kuwe na mwangaza mwingi. Dunia inaposonga kwenye mhimili wake, pole kwa pole inageuka na upande wenye baridi unapigwa na jua. Jua huanza kuonekana kwa muda mrefu zaidi katika siku. Kisha kipindi cha kiangazi cha Aktiki huanza. Huo ndio wakati kunapokuwa na mwangaza wa jua hata katikati ya usiku!

    ReplyDelete
  2. nanukuu “Wazo la kwamba majira ya baridi kali katika maeneo ya Aktiki huwa na giza tititi si kweli,” anasema Ari, aliyelelewa huko Kiruna, Lapland ya Sweden. Sehemu kubwa ya siku inaweza kulinganishwa na machweo. Paula, msanii anayeishi kwenye Lapland ya Finland, anasema, “Wakati Lapland imefunikwa kwa theluji, rangi hugeuka na kuwa bluu na zambarau.”Mwisho wa kunukuu....Nakubaliana na hapa kama ni mgeni utapata sana shida unaweza ukafikiri ni mchana wakati wote hasa huko Kiruna..na sehemu nyingine jua huzama mapema sana hasa wakati wa baridi kali saa tisa jioni giza tayari..kwa mtindo huo kama ni mfanyakazi au mwanafunzi utaondoka nyumbani na giza wakati ni asubuhi saa moja-mbi na utakaporudi giza tena kwa hiyo unaweza usilione jua mpaka miezi ya tatu-nne.

    ReplyDelete
  3. Kuhifadhi Joto Katika Theluji
    =================================

    NA MWANDISHI WA AMKENI! NCHINI FINLAND

    BILA nguo za kutosha na viatu vinavyofaa, wanadamu wangeumia sana au hata kuangamia katika majira ya baridi kali katika maeneo ya Kaskazini ya Mbali. Lakini wanyama wengi wanaendelea na maisha yao ya kawaida katika majira yote. Zaidi ya kuwa na manyoya mengi, wanyama pia hutumia uwezo mzuri wa theluji wa kuzuia baridi isipenye ndani.

    Theluji hufanyizwa kwa chembe ndogo za barafu ambazo hutokana na mvuke wa maji. Theluji yenye kina cha sentimita 25 ni sawa na maji yenye kina cha sentimita 2.5 hivi. Kwa hiyo, theluji ina kiasi kikubwa cha hewa ambacho kinapatikana katikati ya chembe hizo za barafu. Muundo huu wa ajabu unafanya theluji isipenye baridi kali, na hivyo kulinda mbegu na mimea hadi majira ya kuchipua. Kisha, mkusanyo huo wa maji yaliyoganda unayeyuka na kulowesha mchanga na kuingia kwenye vijito.

    Maisha Chini ya Theluji

    Wakipitia mitaro mingi iliyo chini ya theluji, wanyama fulani wadogo wenye manyoya wanaendelea na shughuli zao, wakati mwingi wakitafuta chakula. Wanyama hao wanatia ndani lemming, panyabuku, na aina ya fuko ambao hula wadudu nyakati za usiku. Nao panya wengine wanaonekana wakikimbia juu ya theluji wakitafuta beri, njugu, mbegu, na maganda ya miti michanga.

    Wanyama wadogo wanawezaje kudumisha joto la mwili linalofaa? Zaidi ya kuwa na manyoya mengi, wanyama wengi pia hutokeza joto jingi kwa kuyeyusha chakula haraka. Kwa hiyo, ili waweze kutokeza joto jingi wanahitaji kula chakula kingi. Kwa mfano, kila siku panya hula kiasi cha wadudu kinachokaribia uzito wao. Nao aina fulani ya panya wadogo wanakula chakula kingi hata zaidi! Kwa hiyo, wanatumia karibu wakati wao wote kutafuta chakula.

    Panya hao wanawindwa sana na wanyama fulani kutia ndani bundi na jamii kadhaa za kicheche, na ermine. Vicheche ni wanyama wembamba na wepesi, kwa hiyo ni rahisi kwao kupitia chini ya theluji katika vijia vilivyofichika wanapotafuta chakula. Wao huwinda hata sungura, wanyama wanaowazidi kwa ukubwa.

    Bundi pia huwinda. Bundi mkubwa wa rangi ya kijivu ana uwezo mkubwa wa kusikia hivi kwamba anaweza kumfuata panyabuku anayetembea chini ya theluji ikiwa theluji hiyo si yenye kina kirefu. Bundi anapomwona mnyama anayetaka, anaruka na kuingia ndani ya theluji na kumbeba akitumia kucha zake. Hata hivyo, kukiwa na theluji yenye kina kirefu wawindaji hukosa chakula au hata kufa na wanyama wanaowindwa huongezeka sana.

    Ili wasife njaa katika majira ya baridi kali, wanyama wengi hutumia mafuta waliyokusanya katika miezi yenye joto. Lakini kwa kawaida wao hupata kiasi fulani cha chakula. Kwa mfano, kongoni hula matawi ya miti michanga hasa misonobari. Kindi hula mbegu walizokusanya na kuhifadhi, nao sungura-mwitu hula maganda ya miti michanga, matawi, na majani. Jamii fulani za ndege hufurahia beri zilizoganda na vitawi vya msonobari.

    Kuingia Ndani ya Theluji!

    Ndege kadhaa hutumia uwezo wa theluji wa kuzuia baridi isipenye kwa kupumzika wakati wa mchana au kulala wakati wa usiku chini ya theluji. Ndege hao wanatia ndani hazel hen, kwale weusi, na ptarmigan, pia ndege wadogo zaidi kama vile linnet, aina fulani ya shorewanda, na shore. Ikiwa theluji ina kina kirefu na ni nyororo, ndege fulani huingia ndani ya theluji, kama vile tu ndege wa baharini wanavyopiga mbizi majini. Mbinu hiyo inawasaidia wasiache alama zitakazoonekana au kunuswa na wanyama wanaowinda.

    Baada ya kuingia ndani ya theluji, ndege hao wanachimba shimo lenye upana wa sentimita 60 hivi linaloitwa kieppi katika Kifini. Upepo unaovuma usiku unafanya isiwe rahisi kutambua kwamba kuna viumbe chini ya theluji. Watu wanaotembea wanapofika karibu sana, ndege hao wanawasikia kwa sababu ya kelele ya kutembea kwao. Wanaporuka ghafula na kutifua theluji huku wakipiga mabawa yao wanaweza kumshtua sana mtu ambaye hakuwatarajia.

    ReplyDelete
  4. Zawadi ya Manjano Kutoka Kaskazini
    ==================================
    NA MWANDISHI WA AMKENI! NCHINI SWEDEN

    ‘Tutawapelekea zawadi gani kutoka nchini mwetu?’ mimi na mke wangu tulijiuliza kabla ya kuondoka Sweden ili kuwatembelea rafiki zetu huko Uingereza. Tulitaka kuifanya zawadi yetu ya jemu ya matunda ya cloudberry tuliyotengeneza wenyewe iwe yenye kuelimisha. Kwa hiyo, tuliandika kibandiko chenye maelezo yaliyotegemea mambo tunayojua na utafiti kutoka kwa vitabu vya kwetu. Tumeeleza matokeo ya utafiti wetu hapa chini.

    Cloudberry Ni Matunda ya Aina Gani?

    Matunda ya cloudberry, Rubus Chamaemorus katika Kilatini, hukua kwenye mimea isiyozidi urefu wa sentimeta 30. Kila mmea huchanua ua moja jeupe na kuzaa tunda moja tu. Tunda huwa jekundu na gumu linapokuwa bichi lakini linapoiva linakuwa na rangi ya manjano au ya machungwa na linakuwa laini na lenye majimaji. Jina cloudberry (tunda la mawingu), huenda lilitungwa kwa sababu kwa kawaida huko kaskazini mwa Uingereza matunda hayo hukua milimani karibu na mawingu. Unaweza pia kuyaona kwenye sehemu zenye unyevu, hasa katika maeneo mapana yasiyokuwa na miti na yale yenye majimaji kusini mwa Aktiki. Huko Sweden, matunda hayo huiva Agosti, kabla tu ya majira ya kuchipua kuanza.

    Dhahabu ya Maeneo Yenye Majimaji

    Kwa karne nyingi, wenyeji Walapp wamekusanya matunda hayo ili wayatumie wakati wa baridi kali. Yana vitamini C nyingi na vitamini nyingine, na kwa sababu yana kemikali ya kiasili inayoyahifadhi, jemu iliyotengenezwa kwa matunda hayo inaweza kudumu kwa miaka mingi ikiwekwa mahali baridi. Kwa kuwa walowezi wa mapema katika maeneo haya ya kaskazini walikula nyama na samaki hasa, matunda hayo yaliwapa vitamini. Si ajabu kwamba yameitwa dhahabu ya maeneo yenye majimaji!

    Siku hizi, matunda mengi sana ya cloudberry hukusanywa ili yauzwe madukani na viwandani. Kwa mfano, nchini Sweden, katika mwaka mmoja, zaidi ya tani elfu moja za matunda hayo huchumwa na kuuzwa! Wafanyakazi wanaochuma matunda hayo kwa bidii, hasa wanafunzi wa shule walio likizoni, hupata pesa nyingi kwa njia hiyo. Wenyeji wa Ufini wameyasifu matunda hayo kwa kuweka picha yake kwenye sarafu mpya ya euro mbili!

    Mlo Mtamu

    Tunda la cloudberry lina ladha tamu na chungu yenye kuburudisha. Unaweza kupata jemu ya cloudberry, mvinyo, na vitu vingine vilivyotengenezwa nazo katika maduka ya chakula au maduka mengine katika majiji makubwa ya Ulaya na Marekani. Mara nyingi, aiskrimu ya cloudberry huliwa baada ya milo ya sherehe za kila mwaka za kuwatunukia washindi wa Tuzo ya Nobeli, inayofanywa Stockholm, Sweden. Mikahawa fulani huuza jemu iliyopashwa joto pamoja na aiskrimu ya vanila. Isitoshe, jemu hiyo huliwa kwa keki ya jibini ya Sweden au jibini ya Camembert iliyokaangwa na hutiwa pia ndani ya vitobosha kuongeza ladha. Mvinyo wa manjano wa matunda hayo hutengenezwa nchini Ufini, na divai yake imeanza kuuzwa hivi majuzi huku Sweden.

    Ukitembelea mahali penye matunda hayo, yachume na ufurahie ladha yake tamu, na unaweza kuongeza sukari laini na kupaka juu krimu nyingi iliyopigwapigwa. Utagundua kwamba ni ya pekee sana kama dhahabu na huenda ukachochewa kumshukuru Muumba wako kwa zawadi hiyo yenye ladha tamu sana.

    ReplyDelete
  5. majira ya baridi vinter
    majira ya chipuko vår
    majira ya joto sommar
    majira ya kuchipua vår
    majira ya pukutiko höst

    ReplyDelete
  6. Barido na kipengere cha uzazi wa mpango.....!? patamu hapo watu husema kipindi cha barido mimba huwa kibao..... luku ni muhimu.haya kila lakheli kwa kipindi hiki.Huku UK,naona tuna malizia na jua bado linawaka wiki yoote, sasa hali ya hewa kuna kijijoto jua. kaka s.

    ReplyDelete
  7. POLENI SANA.....NA BARIDI YA HUKO NI NOUMAAAAAAAA

    ReplyDelete
  8. naweza sijuiiiiiii

    ReplyDelete
  9. naanza kuwezaaaaaa

    ReplyDelete