Sunday, September 9, 2012

KANISA NI KANISA...JUMAPILI NJEMA KWA WOTE!!

Kumwomba mungu/kusali si lazima kuwa  na kanisa la kifahali. Tena inawezekana kanisa kama hili ndio maombi yako yatapokelewa zaidi kuliko kwenye makanisa ya kifahami. Kumwomba Mungu ni sehemu yoyote ile na maombi yatapokelewa. Nimelipenda kanisa hili...JUMAPILI IWE YENYE UPENDO NA BARAKA KWA WOTE.

14 comments:

  1. Nikweli sala /ibada yaweza kufanyika popote ilimradi unamtukuza muumba wako. sijuwi kwa nini watu huiona nyumba iliyo enzekwa kwa nyasi kama si nyumba yenye hadhi ,ama mtu anayeishi mle ndani yake huonekana masikini nk.swali unaishi kijijini mazingira yaliyo kuzunguka ni nyasi ,miti na udongo,ukijenga nyumba kwa kutumia vitu vilivyo kuzunguka,kama nilivyo vitaja, na ukatumia utaalamu wa kiasili kuijenga,na nyumba ikawa bora kuna tatizo? kuna umasikini kweli hapo? au nyumba ya bati ndo utajiri? sijuwi mnalionaje hili swala la nyumba ya kuenzekwa kwa nyasi inauhusano wowote na maisha duni? jumapili njema wote.kaka s

    ReplyDelete
  2. Uliyecomment hapo juu, Nyumba ya nyasi haiwezi kuwa na umeme, kuvuta maji ndani,nk. Huo ni umaskini tosha hata bila kuuliza! Na lazima itakuwa na wadudu ndani jamani tuwe wawazi na wakweli kwenye kucomment. Mungu atusaidie ili maendeleo yafike hata vijijini. Comments zingine kama zinakashifu.

    ReplyDelete
  3. Yasinta unaishi ulaya, leo hii uende kuishi kijijini kwenye nyumba kama hiyo na mume wako na watoto, nadhani practically its impossible but theoretically its possible! Tuwe wakweli na wawazi. Jumapili njema.

    ReplyDelete
  4. Usiye na jina wa 3:42!
    Nimeshawahi kuishi kwenye nyumba kama hiyo na wala hatukuona shida..Sio kwamba nakubaliana tusiwe na maendelea lakini mtu unaridhika na ulichonacho..Jumapili njema nawe pia.

    ReplyDelete
  5. Nikienda na nguo nzuri na safi katika hiyo nyumba ya nyasi ni rahisi kuchafuka.Hivi nitahitaji kubadili mara nyingi kufua mara nyingi na kununua sababuni mara nyingi=matumizi zaidi ya hela.Wakati wa mvua mashaka zaidi,itavuja tu kama si mwaka wa kwanza basi wa pili au wa tatu.Lazima kuezeka upya=matumizi zaidi na muda zaidi.Nyumb aya nyasi ni rahisi kushika moto na hivi mashaka zaidi.
    Kama mtu una uwezekano wa kununua taa au kutumia umeme fanya hivyo uking'ang'ania kibatari ni matumizi mabaya ya akili ambazo tumepewa na Mungu.Ni sawa na mtu ambaye uwezo wake ni alama 100% au 90% lakini anabaki na alama 20% au 30 ati ameridhika na zinamtosha.Utadaiwa kwa kutotimiza wajibu.Daima tufikiri vizuri kwenda mbele,kwenye mazingira bora na safi zaidi wajameni.

    ReplyDelete
  6. Usiye na jina wa 4:36! nakubaliana nawe asilimia 100% kwa yote uliyosema. Hapa ilikuwa kuonyesha jinsi watu wanavyojishughulisha hata kama hawana uwezo lakini pawepo mahali pa kumwabudu Mungu hata jkama sakafu ni udogo na paa ni nyasi. Pia hii ni kama mila kwa vile mababu zetu walikuwa na nyumba kama hizi kwa hiyo mara nyingi tuwe tunakumbuka piua tulikotoka ni kama kumbukumbu.

    ReplyDelete
  7. IBADA POPOTE PALE......MUNGU ANATUSIKILIZA TU...IWE NA BARAKA KWAKO PIA DADA

    ReplyDelete
  8. Kazi kwelikweli!!.Nyumba iliyo enzekwa nyasi huwezi kuweka umeme! sina hakika.ila muhimu hapa nikuangalia maisha katika mazingira yanayo tuzunguka.je mbona katika maendeleo ,hoteli zilizo ufukweni,nyumba zilizo jengwa kwa matumizi ya starehe zimeenzekwa kwa makuti au nyasi. nyumba kuenzekwa kwa nyasi au makuti wala siyo tatizo.nasikweli kuwa ukienzeka kwa kwa nyasi hazidumu sikweli ,na wala maswala ya moto si kweli moto ukitokea ni ajali tu. na hapa hoja yangu ilikuwa kwamba nyumba zilizo enzekwa kwa nyasi siyo tatizo kama zimejengwa vizuri,badala ya kukaa kusubiri bati,kamauna uwezo na lina patikana weka lakini siyo usipo weka bati wewe ndo hoi kimaisha.kaka s

    ReplyDelete
  9. Nyumba ya nyasi ina uhusiano moja kwa moja na maisha duni. Mfano Dada Yasinta umecomment uliwahi kukaa kwenye nyumba kam hiyo na hukuona tabu, kama hivyo ungeendelea na ku-maintain hayo maisha na kuwa mpaka leo ukienda ukakae kwenye nyumba kama hiyo, kwa nini tunajenga basi za kisasa? kumbukumbu muhimu sana.

    ReplyDelete
  10. Hivi wewe,mtoa mada usiye najina,kuwa nanyumba yenye bati ndo utajiri? wangapi wanakaa nyumba za bati humu mijini halizao hofu bin taabani,hata hiyo nyumba ya manyasi iliyo enzekwa kwa nyasi hawezi kuipata. kumbuka wazee wetu walianzia huko kwenye nyumba za manyasi,na wakaweza kusomesha watoto wao ambao wengine walikuja kuwa viongozi wakuu wanchi hii. muhimu kwako kumbuka kuishi kulingana na urefu wa kamba yako,na wala siyo kuishi ukiwa na umasikini wa fikra/akili.kakas.

    ReplyDelete
  11. Hakuna sehemu niliyoandika nyumba ya bati ni utajiri! ila wewe ndio umeandika hivyo. Sihusishi bati na utajiri la hasha, bali nasema nyumba ya nyasi na udongo ni ya hali duni. Kwani maendeleo ni nini? mie sizungumzii kuwa utajiri ni direct propotion to nyumba ya bati. Ila tunazungumzia nyumba ya nyasi na kwa comment zangu ni ya hali ya chini, hata kama kijiji kizima waméjenga nyasi basi utakuta wana maisha ya chini. Unajua kwa nini Tanzania ni least developing country? Mojawapo kupikia kuni, nk. sasa hapo utasema mie napikia kuni nimeendelea kwa kuwa kupikia umeme ni utajiri. Tunazungumzia maendeleo na sio kulinganisha!

    ReplyDelete
  12. Pamoja wapendwa,Natumaini J'Pili ilikuwa njema!!!!

    ReplyDelete
  13. mungu ana abudiwa mahali popote

    ReplyDelete