Monday, August 27, 2012

TUENDELEZE JUMATATU HII KINAMNA HII:- MFANANISHO!!!



Nimeamka asubuhi hii kama kawaida nikafungua email yangu . Nikakutana na ujumbe/ picha hii ya kwamba nimefanana sana na huyu dada Angela Chibalonza...nimeiangalia hii picha yake na kufananisha na yangu, kwangu imekuwa ngumu kuona na nimeona afadhali nipata msaada hapa kibarazani je ni kweli tumefanana? angalia picha hizi hapa chini...

Marehemu dada Angela Chibalonza
Yasinta Ngonyani
Nawatakieni wote JUMATATU njema maana mwanzo wa juma huwa na mikikimikiki sana !!!!!!

17 comments:

  1. Kiaina unafanana naye. KAKA S

    ReplyDelete
  2. kaka Sam! kwanza karibu sana tena ...Kiana ukiwa na maana gani? Je unaweza kufafanua?

    ReplyDelete
  3. Dada Yasinta, kweli duniani watu wawilwawili, ningelitamani kuona 'fingerprints' zenu kama zafanana. Kabla ya kusoma maandishi sikusita kusema ni wewe. Haya tuwasikie wengine wanasemaje kuhusu kufanana kwenu!

    ReplyDelete
  4. kwa picha hiyo hapo juu ya huyo dada,kimapozi! kuna kaufanano fulani.kaka s

    ReplyDelete
  5. Hakika huu ni mfanano makini katika ufananishaji na mkaribiano wa sura za watu katika mchakato wa maisha na mafanikio.

    ReplyDelete
  6. Siwezi kusema sana lakini kwa hiari ya moyo nalazimika kutamka:Ndiyo!!

    ReplyDelete
  7. Yah kufanana kupo, na huenda mumechangia damu, sio mbaya...!

    ReplyDelete
  8. Nimgundua kuwa mimi siku zote ni mtu wa mwisho kugundua kama wamefanana, sijui kwa nini. Labda sijui kufananisha. Ila nikifika hatua ya kusema wamefanana, nina wasi wasi kama kuna mtu ataweza kuwatofautisha, maana watakuwa wamefanana kweli kweli. Sijui aliyeanza kusema mmefanana aliangalia nini.Pua, midomo, masikio, macho au pua? Ila ukichukua jumla jumla, ninapata ujasiri wa kutosha kusema HAMFANANI ati!!
    Ni mtazamo tu...

    ReplyDelete
  9. Kaka Juma Nyumayo!Yaani kweli tumefanana kihivyo duh...labda dada yangu..LOL
    Kaka Sam:-)

    Chacha! labda kivipi?

    Usiye na jina! unaweza kusema ni kipi hasa tulichofanana?
    Kaka Ray! Labda nawe nikuulize ni kivipi tumefanana hasa?

    Ester! Ni mfanano gani ulipo?

    emu3..:-) haiwezekani...
    Kaka Mhagama..hata mimi sijui kufananisha na ndio nikaona niombe msaada...Du nitafanana na watu wangapi?

    ReplyDelete
  10. Nawaunga mkono waliosema wanafanana!

    ReplyDelete
  11. Mimi sioni kama kweli mnafanana bali kiaina kama wengine walivyosema. Kwa waliomuona kwa karibu akiwa nchini Kenya si rahisi kukubaliana kuwa mnafanana.

    ReplyDelete
  12. Kwa maoni yangu sioni kama mnafana hata kidogo. Zaidi ya hayo kwa nini mtu akufananishe na Marahemu? Jee huo ni utamaduni wetu?

    ReplyDelete
  13. mnafana kiaina na Marehemu ANGELA CHIBALONZA!

    ReplyDelete
  14. Kaka Malkiory...:-)

    Mwal. Mhango. Hiyo kiana ningependa kujua ina maana gani?

    Remija! karibu sana katika kibaraza hiki. Ahsante, kama nakumbuka vizi nakumbuka si vibaya kumfananisha mtu na marehemu labda inategemea na sehemu unayotoka.
    Elly! nawe karibu sana...Kiaana vipi twafanana?

    ReplyDelete
  15. @Yasinta;
    Ukitaza uso ndiyo majibu yenyewe!

    ReplyDelete