Tuesday, August 28, 2012

HAPA WENGI TUNAKUMBUKA MALEZI YA WATOTO!!


Katika malezi/makuzi watu tumetoka mbali, huyu binti hapa ananikumbusha mbali sana.Wazazi wanaondoka asubuhi huku wakitegeme binti mimi/huyu afanye kazi ya kuchota maji. Na hapo labda sio ndoo moja tu pipa zima. Na hapo hapo amtunze mdogo wake. Na labda kuchochea maharage pia. Hali hii kwa sasa hakuna kabisa maisha yamebadilika kabisa ndiyo kwanza utakuta mtoto anamtuma mzazi wake. Maisha siku hizi yamekuwa  watoto na TV, Komputa, simu nk. Hata kumwona mtoto siku hizi anasoma kitabu ni mara chache sana. Ndiyo maana  sisi tuliolelewa  katika malezi ya aina hii kama huyu binti inatupasa tuendeleza kwa kuwahimiza  watoto wetu waweze kufanya hivyo hata kama ni kidogo. Polepole ni mwendo...Hata hivyo najua hali hii ya watoto kusaidia kazi za nyumbani vijijini bado inaendelea. Binafsi niitazamapo picha hii najiona ni kama mimi...na naweza nikasema natamani niwe tena kama huyu binti...Je? umewahi kuifanya kazi hii? au labda kuchunga mbuzi na ngómbe kama watoto hawa hapa....


....na hapa ndipo watu wanapojifunza maisha  ni nini/ hawa ndiyo  wataweza kuyamudu maisha yoyote yale na pia kujua ugumu na uzuri wa maisha ....JUMANNE NJEMA!!!!

17 comments:

  1. Namshukuru Mungu alinipa nafasi ya kukulia kwenye mazingira yanayofanana sana na haya ya kwenye picha. Sina hakika ni lipi la kijijini sijalifanya. Nimechota maji mtoni, nimebeba sana kuni kichwani, nimekoboa sana mahindi kwenye kinu, nimechunga mbuzi kama Mmasai, mimi na pori, pori na mimi. Nasikitika tu sikupata nafasi ya kwenda JKT, nadhani hiyo ingenisaidia kuyamudu maisha ya namna yoyote ninayoweza kukutana nayo kwenye taifa hili. Hata hivyo siyo mbaya, huko nilikopitia kumenikomaza vya kutosha, maisha yanaenda.
    AMANI KWENU NYOTE.

    ReplyDelete
  2. Duuh lakini KADALA, Huyu kama ni mtoto sana au anaiga/kujifurahisha tuu? wewe ulianza kubeba ndoo au vidumu? na jee ulikuwa na umri gani?

    mimi nimebeba lakini nilikuwa mkubwa kidogo yaani najielewa.

    Watoto wa .com wanamambo meeengi sana,kama mzazi hukukomaa nao kweli wanakutuma tu.

    Wenu KACHIKI.

    ReplyDelete
  3. Haya maisha hayakuwa mazuri hata kidogo nawala si ya kukumbuka. ukiangalia kwa undani zaidi maisha haya yalikuwa ya mojakwa kwa moja,yaani mtoto alipokea amri tu na sivinginevyo. mazingira yalichangia sana watoto wa enzi hizo mnazo ongelea kuwa hivyo.mimi binafsi nikiangalia picha kama hizi zinanitia huzuni sana. haya ni mawazo yangu. kaka s.

    ReplyDelete
  4. Kaka Mhagama yaani usiseme na mimi hivyo hivyo na nawashukuru sana wazazi/walezi wangu kwa walivyonilea.

    Kachiki! mie nadhani ana miaka 6-8 vile mimi nilianza kubeba vidumu .. nadhani nilikuwa miaka 8.

    Kaka S. unajua maisha hata yakiwa mabaya au mazuri ni vizuri kuwa na kumbukumbu ..lakini kama umepatwa na huzuni kwa picha hizi basi pole kakangu.

    ReplyDelete
  5. Hakika kila zama na waja wake na asante Yasinta kwa kutusaidia kurudisha mawazo nyuma.Asante sana.

    ReplyDelete
  6. Ndio maisha, ...kama kijiwe kilivyo, maisha na mafanikio! Ukifanikiwa mshukuru mungu wako, maana tumetoka mbali!

    ReplyDelete
  7. nimekulia humu humu, kwakweli....ila watoto wa siku hizi wanakosa sana hizi ladha za maisha...u-dot com mwingi mno

    ReplyDelete
  8. Kaka Ray..Nafurahi kama umeweza kurudisha mawazo nyuma..Pamoja daima.

    emu3! :-) nimetabasamu hapa kwa ulivyosema nimependa....Na kweli watu tumetoka mbali...

    Ester!! nakuona na kadumu kako unatoka kisimani ..tusikate tamaa tuwahamasishe watoto wetu ili hii mila isipotee...

    ReplyDelete
  9. Unachojaribu kutukumbusha ni kile kinachoitwa na kilichokuwa kinazingatiwa awakati huo kulea kwa vitendo na kuzoesha hali halisi ya maisha.
    Kilichokua kinafanyika ni kutenganisha majukumu ya mtoto katika malezi yake ambapo siku hizi wanaharakati wanachanganya na kuweka masuala hayo katika ajira za watoto wakati si kweli.
    Tuanakazi ya uwakuza watoto kwa msingi wa uhalisia na si maisha bandia. lakini jamii imekata tamaa na imaekubali kuruhusu mambo yaende kombo. Tumebakia kulalamika na kalaumu wakati wate tunahusika katika kuahakikisha jamii kuanzia familia inalelewa kwa misingi ya uhalisi na kuweka ukweli wa kuwaamini watoto wetu wetu kuwa utu na ubionaadamu wetu unajengwa kwa misingi ya kufanyakazi na kuheshmu tamaduni na mila zetu hata kama tunajidanganya kuwa tunaishi katika dunia ya usasa/
    Kila la kheri

    ReplyDelete
  10. HAYA MALEZI MIE NAONA NI BORA ZAIDI KWA SABABU UNAMFUNDISHA MAISHA YA KUJITEGEMEA

    ReplyDelete
  11. You should be a part of a contest for one of the greatest
    websites online. I will recommend this site!

    my web-site; Tyrone Jaquez

    ReplyDelete
  12. Hello colleagues, its fantastic post on the topic of teachingand entirely defined,
    keep it up all the time.

    My page :: Mohammed Malcolm

    ReplyDelete
  13. Someone necessarily help to make severely articles I might state.
    That is the very first time I frequented your web
    page and up to now? I amazed with the research you made to
    make this actual publish extraordinary. Excellent task!

    Feel free to visit my page :: Will Hassan

    ReplyDelete
  14. It's appropriate time to make some plans for the future and it is time to be happy. I've read this post and if I could I wish
    to suggest you few interesting things or advice.
    Perhaps you can write next articles referring to this article.
    I desire to read more things about it!

    Feel free to visit my website ... Trey Israel

    ReplyDelete
  15. Howdy! I know this is kind of off-topic however I needed to ask.

    Does building a well-established website such as yours take a lot of work?
    I'm completely new to writing a blog however I do write in my diary every day. I'd like to start a blog
    so I will be able to share my own experience and thoughts online.
    Please let me know if you have any ideas or tips for brand new aspiring bloggers.
    Thankyou!

    My web-site; Vaughn Jaron

    ReplyDelete
  16. Howdy! This is kind of off topic but I need some help from
    an established blog. Is it difficult to set up your own blog?
    I'm not very techincal but I can figure things out pretty quick. I'm thinking about making my own but I'm not sure where to start. Do you have any tips or suggestions? Thanks

    Take a look at my site Trey Jaiden

    ReplyDelete