Tuesday, August 14, 2012

METHALI ZETU:- METHALI ZAFAA SANA KWA MAFUNDISHO YA ADILI!!!!

1. Penye urembo ndipo penye urimbo.
2. Radhi ni bora kuliko mali.
3.Siku utakayokwenda uchi, ndiyo siku utakayokutana na mkweo.
4. Ukitaka kula nguruwe, chagua iliyenona.
5. Ulipendalo hupati, hupata ujaliwalo.
6. Ungelijua alocho nyuki, usingekula asali.
7. Vyako, vyako na mwenzio; vikikupata ni vyako peke yako.
8. Wagombanao ndio wapatanao.
9.Yote yangáayo usidhani ni dhahabu.
10. Zimwi likujualo, halikuli likakwisha.
Tusisahau methali zetu, tuwetunazitumia katika mafundisho. Pia tuwaambia na kizazi kijacho. Maana hii ndio asili yetu......

3 comments:

  1. Kuendako hisani hakurudi nuksani bali shukrani.Asante sana!!

    ReplyDelete
  2. nimepita kukusalimia tu rafiki yangu ujue nipo sijapotea!

    ReplyDelete
  3. Omo na tezi marejeo ngamani na pema usijapo pema ukipema si pema tena.

    ReplyDelete