Thursday, August 23, 2012

ALIYE TELEKEZA MTOTO SONGEA AKAMATWA NA JESHI LA POLISI!!!!


Mara baada ya kukamatwa na Police alipewa mtoto amnyonyeshe huku akijutia baada ya kudanganywa na Mwanaume

Habari hii imenisikitisha sana kuona Songea yangu imegeuka na kuwa hivi. Huyu mama/binti ni bado hajakomaa kuwa mama halafu wanakuja wanaume na wamemdanganya na pengine wazazi pia wamemfukuza kwa kupata mimba haruhusiwi kuishi nyumbani halafu anapata mimba na baadaye kujifungua. Hapohapo wanakuja  mwanaume na kumdanganya tena maskini afanye nini? Nyumbani kumezuka mbogo.Najaribu kujiuliza binti wa miaka kumi na nane na halafu una mtoto peke yako aliyekupa mimba amepotea je utafanya nini peke yako?. Mwanzoni kuna kuwa na mapenzi, maneno mazuri, zawadi nzuri na msichana anazuzuka na mwisho ndio unakuwa huu..hakika ni safari ndefu sana tunayo...hebu soma hapa chini habari ya huyo dada Zawadi yalimsibu. Habari hii nimeipata hapa
-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Adamu Nindi, Songea.

Jeshi la Polisi Mkoani Ruvuma limefanikiwa kumtia mbaroni Mama aliyemtupa Mtoto katika Guba ya kutupia takataka eneo la Mitumbani Majengo Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoa wa Ruvuma Ana Tembo ameyasema hayo wakati akiwa katika Ofisi ya Polisi wanawake Mkoani Ruvuma amesema Mama huyo ambaye alimtupa Mtoto wa kiume mwenye ummri wa miezi 5 wiki iliyopita amepatikana baada ya msako mkali ulioendeshwa na Jeshi la Polisi.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoa wa Ruvuma Anna Tembo amesema Mama huyo alipatikana katika nyumba ya kulala wageni eneo la Majengo akiwa amejificha chini ya uvungu wa kitanda akikimbia mkono wa Dola.
Jeshi la police lilipo mhoji Zawadi Komba 18 alidai siku hiyo alikuwa akifukuzwa na kichaa ndipo alipo mtupa mtot lakini baada ya kubana na mkono wa sheria ndipo alipo eleza ukweli kuwa alitumbukia katika dimbi la mapenzi
Mama aliyekayekamatwa na Jeshi la Polisi Zawadi Komba18 kwa tuhuma za kumtupa mototo wake na kutaka kuhatarisha maisha ya motto kwa kuliwa na Mbwa, amesema yeye alidanganywa na Mwanaume kuwa angeweza kumuoa endapo angemtupa mototo halafu wangekwenda kuishi Mkoani Mbeya.
Wadau mbalimbali wa Mtandao wa Polisi Wanawake, wakiwakilishwa na Fadhili Chacha wameshauri Wanawake wajishughulishena katika Biashara mbalimbali badala ya kutegemea Wanaume pia wajitahidi kuingia katika mpango wa uzazi wa mpngo ili kuepukana na kubeba mimba bila kutarajia.
Kwa Mkoa wa Ruvuma kuhusu ukatili dhidi ya Watoto hii ni mara ya tano katika mwezi mmoja, tukio la kwanza Baba na Mama walidiriki kumuua Mtoto kwa kumvunja shingo na kumtupa katika daraja la Bombambili, Tukio la Pili Mama mwenyewe na Baba walimuua Mtoto na kumtumbukiza katika sinki la maji taka, tukio la tatu Mtoto alitupwa eneo la Majengo na kuliwa na Mbwa na kubakizwa kichwa, watoto wengine wawili waliweza kuokolewa akiwemo na Mtoto mmoja ambaye alitupwa eneo la Msikitin

8 comments:

  1. Kwa mtaji huu,tutaishia kubaya, maana laana itatuandama kila kukicha, hebu jiulize kiumbe kama huyu (mtoto)ana husikaje katika starehe zenu, hebu jiulize kiumbe kama huyu kakosa nini

    ReplyDelete
  2. kwakweli ukatili kwa nini hauishi????? inasikitisha sana

    ReplyDelete
  3. emu3! yaani mtoto/ malaika huyo haina hatia yoyote ile na pia ukijiuliza tena na tena, huyu mama anafikiri kweli huyo mwanamume aliyemwambia /danganya wataenda kuishi Mbeya kweli angemfanyia hivyo? na anafikiri huko Mbeya angeishi naye tu bila kumpa mimba nyingine? Na je angefanya nini na hicho kiumbe? najiuliza tu kwa sauti...

    Ester..Ukatili hautaishi sasa wewe fikiria ametunza mimba miezi tisa amejifungua na mtoto miezi mitano halafu anamtupa na kuondoka bila wasiwasi yaani kabisaaaaa...sipati picha kabisa..watu wanatafuta watoto hadi kwa dawa na wengine wanapata na halafu wanatupa....

    ReplyDelete
  4. Mwanzo hadi mwisho, hii yote ni kazi ya shetani, baba wa uwongo.

    ReplyDelete
  5. Naungana nawe kaka Mhagana..

    wangemcharaza viboko kwanza,kwani hizo starehe sindiyo zilimpatia mtoto,tena hizohizo zinamfanya aache mtoto jee akipata mtoto?

    ReplyDelete
  6. Kaka Mhagama hakika inasikitisha sana na kweli huyu ni shetani.

    Da`kachiki! kweli angepata kwanza viboko aliwaza starehe tu lakini hakuwaza baada ya starehe itakuwa nini? kaaazi kwelikweli...

    ReplyDelete
  7. Asante sana Dada Yasinta kwa Ukomavu wa kuomba radhi, lakini masage sent. Tupo pamoja kw nia yako njema

    ReplyDelete
  8. Asante sana Dada Yasinta kwa Ukomavu wa kuomba radhi, lakini masage sent. Tupo pamoja kw nia yako njema

    ReplyDelete