Nawapenda sana wanyama hawa Twiga...wana pendeza pia wana mwendo wa maringo...
Na Chui nao wamo....
Pundamilia ..ebu angalia mwonekano huu hapa ....
Na hapa ni Ndovu/Tembo...huwa wanaonekana wapole lakini ..nakumbuka siku moja nilinusurika ilikuwa Tarangire tulikuwa tumepiga hema eeh bwana wewe ingekuwa hadithi nyingine kabisa..
hahaaha... Yasinta hebu tupe hiyo hadithi ya kunusurikia..
ReplyDeleteMungu ni mwema..
Mija!Kunusurika kwangu ni kwamba kama nilivyosema hapo tulikuwa tumepiga hema katika Mbuga ya wanyama Tarangire. Sasa, sijui nao tembo wananusa wakawa wanapita pale tulipolala na giza/kiza ndo kimeshaingia. Wacha nianze kutetetemeka mwenzangu akaniambia kaa kimya ukitoka nje tu utakwisha. Nikamuuliza je hapa hawawezi kutukanyaga? maana hawajui kama kuna hema..sisi ndo tumewaingilia katika nyumba yao..Lakini Mungu mkubwa tukaamka salama ....Kisa kingine siku hiyohiyo tukiwa na marafiki wengine tulisimama kula matunda na mara tembe wakaja na mmoja kati ya marafiki akawa mbishi na kusema kwa nini tutoke mapema mbona wako mbali sana? Sisi wengine tukaingia kwenye gari naye akaendelea kuwa mbishi na mara Tembo wakaanza kutimua mbio na dereva kwa woga akagonga mti na kuharibu gari lakini wote tukawa salama....kwa ufupi ni hivi..
ReplyDeletePole sana unanikumbusha mtoto mmoja alikwenda kijijini,yeye hajawahi kuona ng'ombe, alipomuona ngombe anapita akamwambia baba yake,
ReplyDelete'Baba unanona zinga mdudu...'
Sasa wenzako tembo, wanamfanya kama gari, wewe unamuogopa, je ungekutana na mfamlewa nyika ingekuwaje....au nyoka,chatu,...
@Yasinta;
ReplyDeleteAsante kwa kuonyesha kuonyesha sifa za muumba wako kupitia kazi ya mikono yake.
-------------------------------------
Ayubu 39:1-30
1 “Je, umepata kujua wakati uliowekwa wa mbuzi wa milimani kuzaa?
Je, unaangalia wakati ule paa wanapozaa kwa uchungu?
2 Je, wewe huhesabu miezi ambayo wao hutimiza,
Au, je, umepata kujua wakati uliowekwa ambapo wao huzaa?
3 Wao huinama wanapotoa watoto wao,
Wanapoondoa uchungu wao.
4 Wana wao huwa wenye nguvu, huwa wakubwa porini;
Kwa kweli wao huenda zao wala hawarudi kwao.
5 Ni nani aliyemwachilia punda-milia awe huru,
Na ni nani aliyevifungua vifungo vya punda-mwitu,
6 Ambao nimeweka nchi tambarare ya jangwa kuwa nyumba yao
Na ambao makao yao ni nchi ya chumvi?
7 Yeye huyacheka machafuko ya mji;
Naye hasikii kelele za mwindaji.
8 Yeye hutafuta-tafuta malisho yake milimani
Naye hutafuta kila namna ya mmea wa kijani.
9 Je, ng’ombe-mwitu hutaka kukutumikia,
Au, je, atalala usiku kwenye hori yako?
10 Je, utamfunga imara ng’ombe-mwitu kwa kamba zake katika mtaro,
Au, je, yeye atalima nchi tambarare za chini nyuma yako?
11 Je, utamtegemea kwa kuwa ana nguvu nyingi,
Na, je, utamwachia yeye kazi yako ngumu?
12 Je, utamtegemea kwamba atarudisha mbegu zako
Na kwamba atakusanya kwenye uwanja wako wa kupuria?
13 Je, bawa la mbuni-jike limepiga-piga kwa shangwe,
Au, je, yeye ana mbawa za korongo na manyoya?
14 Kwa maana yeye huyaacha mayai yake katika nchi
Naye huyatia joto katika mavumbi,
15 Naye husahau kwamba mguu fulani unaweza kuyavunja
Au hata mnyama wa mwituni anaweza kuyakanyaga.
16 Yeye huwatendea wanawe kwa ukali, kana kwamba si wake—
Kazi yake ngumu ni ya ubatili kwa sababu yeye hana hofu.
17 Kwa maana Mungu amemfanya asahau hekima,
Naye hakumpa fungu katika uelewaji.
18 Wakati anapopiga-piga mabawa yake juu,
Yeye humcheka farasi na mpandaji wake.
19 Je, unaweza kumpa farasi nguvu?
Je, unaweza kuivika shingo yake manyoya yanayotetema?
20 Je, unaweza kumfanya aruke kama nzige?
Fahari ya kukoroma kwake ni yenye kutisha.
21 Yeye huparapara katika nchi tambarare ya chini na kufurahia nguvu;
Husonga mbele kukutana na silaha.
22 Huicheka hofu, naye hatishiki;
Wala harudi nyuma kwa sababu ya upanga.
23 Podo hupiga kelele juu yake,
Kichwa cha mkuki na pia fumo.
24 Yeye huimeza nchi kwa mwendo wa kishindo na msisimuko,
Wala haamini kwamba ni sauti ya baragumu.
25 Mara tu baragumu inapopiga yeye husema Aha!
Naye hunusa harufu ya pigano kutoka mbali sana,
Mshindo wa wakuu na kelele za vita.
26 Je, ni kwa sababu ya uelewaji wako kwamba kipanga hupaa juu,
Kwamba yeye hunyoosha mabawa yake kuuelekea upepo wa kusini?
27 Au, je, ni kwa agizo lako
kwamba tai huruka kuelekea juu
Na kwamba hujenga kiota chake huko juu,
28 Kwamba yeye hukaa kwenye mwamba na wakati wa usiku hukaa
Juu ya ncha ya mwamba na mahali pasipoweza kufikiwa?
29 Kutoka hapo yeye hutafuta chakula;
Macho yake huendelea kutazama mbali sana.
30 Na watoto wake huendelea kunywa damu;
Na mahali walipo wale waliouawa, yeye yupo hapo.”
Duuhh poleni sana, ndugu wa mimi emu wa 3 hahaaha.
ReplyDeleteJamani sijui mwenzenu ni mshamba yaani naogopa sana mambo ya mbugani si mpenzi kabisaaaa, kwani siwaamini naona kama watanishinda mbio.
em3..nafurahi kama nawe umepata kukumbuka hicho kisa...
ReplyDeleteKaka Ray.. Bila mikono ya Muumba wetu hata nasi hatungekuwepo na ndio maana kila kuchapo na kila uendapo kulala ni lazima tumshukuru.
Rachel/Kachiki ndo maana nakuambia njoo tuwe tunakimbia..mchakamchaka/mazoezi. Ukifanya hivyo utawashinda tu na ndio nasema hakuna mtu mshamba Kachiki::::
@Yasinta;
ReplyDeleteKutokana na mikimikiki ya maisha kuelekea mafanikio huenda kwa njia moja au nyingine tukabakie tunamzungumzia muumba wetu kupitia haditi,nyimbo na mashairi na kusahau wajibu wetu kama binadamu mbele za muumba wake.
------------------------------
@Wadau tutafakari maneno ya mtume Paulo kwa Timotheo na kuchukua hatua thabiti na dhahiri;
---------------
2 Timotheo 3:1-7
1 Lakini ujue jambo hili, ya kwamba katika siku za mwisho kutakuwa na nyakati za hatari zilizo ngumu kushughulika nazo. 2 Kwa maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda pesa, wenye kujidai, wenye majivuno, wakufuru, wasiotii wazazi, wasio na shukrani, wasio washikamanifu, 3 wasio na upendo wa asili, wasiotaka makubaliano yoyote, wachongezi, wasiojizuia, wakali, wasiopenda wema, 4 wasaliti, wenye vichwa vigumu, wenye kujivuna kwa kiburi, wanaopenda raha badala ya kumpenda Mungu 5 wakiwa na namna ya ujitoaji-kimungu lakini wakizikana nguvu zake; nawe geukia mbali kutoka kwa hao. 6 Kwa maana kutoka kwa watu hao huinuka wale watu wanaojiingiza kwa ujanja katika nyumba na kuwachukua mateka wanawake walio dhaifu ambao wamelemewa na mizigo ya dhambi, wanaoongozwa na tamaa za namna mbalimbali, 7 wakijifunza sikuzote na bado hawawezi kamwe kufikia ujuzi sahihi juu ya kweli.