Tuesday, July 10, 2012

UNAKUMBUKA? WIMBO WA TANZANIA!!!


1, Tanzania Tanzania,
Nakupenda kwa moyo wote,
Nchi yangu Tanzania,
Jina lako ni tamu sana,
Nilalapo nakuota wewe,
Niamkapo ni heri mama wee,
Tanzania Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote.

2. Tanzania Tanzania,
Ninapokwenda safarini,
Kutazama maajabu,
Biashara nayo makazi,
Sitaweza kusahau mimi,
Mambo mema ya kwetu kabisa,
Tanzania Tanzania
Nakupenda kwa moyo wote.

3. Tanzania Tanzania,
Watu wako ni wema sana,
Nchi nyingi zakuota,
Nuru yako hakuna tena,
Na wageni wakukimbilia,
Ngome yako imara kweli wee,
Tanzania Tanzania
Heri yako kwa mataifa.

4. Nchi nzuri Tanzania,
Karibu wasio kwao,
Wenye shida na taabu,
Kukimbizwa na walowezi,
Tanzania yawakaribisha,
Mpigane kuime chema wee,
Yanzania Tanzania 
Mola awe nawe daima.

6 comments:

  1. Karibuni Tanzania kwenye ardhi ya mlima Kilimanjaro,visiwa vya Zanzibar,mbuga za Serengeti na daraja la kibiashara na uchumi kwa nchi za maziwa makuu kupitia bandari ya Dar es Salaam.

    ReplyDelete
  2. Kweli Tanzania ni nje nzuri,maana ina utajiri sana, na matajiri sana, lakini cha ajabu ni maskini!
    Na wenyewe ni wavumilivu sana, na wanawapenda sanawageni, ambao wakija wanachukua UTAJIRI wao na kupelekwa kwenye nchi zao.
    Ni ajabu kabisa

    ReplyDelete
  3. @emu-three;
    Hii siyo ajabu bali ni changamoto kwetu.Usilaumu ulipoangukia bali jiulize ulijikwaa wapi?

    ReplyDelete
  4. kaka Ray! Ahsante..Kweli kuna vitu vingi sana vya kuvutia...

    emu3! ndivyo inavyokuwa ...na pengeni tunaona hivyo tulivyo navyo si mali.

    ReplyDelete
  5. @Yasinta & emu-three;
    Hii ni Tanzania na wajenzi ndiyo sisi na maliasili zote zinahitaji usimamizi na uwezeshaji wa wadau wote.Je kwa pamoja tumekwama wapi??????????

    ReplyDelete
  6. Nilikuwa safari ni kwnye msiba wakati narudi nikiwa kwnye gari ndugu yangu wimbo umenifariji sana na kunikumbusha mbali

    ReplyDelete