Unapokuwa na mapumziko ya siku mbili tatu hivi kabla hujapata likizo kamili basi unakimbia na kujificha hapa (SUMMER HOUSE/SOMMARSTUGA). Mahali ambapo unaweza kupumzika tu hakuna eti ngoja niangalia mtandaoni kuna nini HAKUNA.
Na ukitokwa na jasho au ukijisikia uchovu basi ni kujitupa tu majini huna haja ya kwenda mbali kutafuta maji.......
Ila kula ni muhimu ..akina mama wapo jikoni, na hapo ni mzee wa nyumba na pia ni raha kufikiwa na wageni aliyevaa kofia ni mgeni wetu mzee Masawe.......
...Wanapofika wageni ni raha kwani siku hii nilipata zawadi ambayo nilikuwa naitamani siku nyingiiiiii:-) Hiyo hapo juu UTAMADUNI !!!
Tunapojisikia hamu ya samaki basi ni kuchukua boti na kwenda kujaribu...wavuvi wadogo haoooo wanakwenda kutafuta kitoweo....
Baada ya muda wanarudi mikono mitupu hakuna kitoweo...hivi ndivyo ilivyokuwa siku mbili/tatu nilipokuwa kimya...NAWATAKIENI WOTE JUMAMOSI NJEMA.....KAPULYA:-)
Hongereni sisi tumerudi jana.
ReplyDeletesafi sana, waswahili wanasema "raha jipe mwenyewe, ukisubiri kupewa utajistukia una manundu mwli mzima" hahaha
ReplyDeleteEdna! kwanza ahsante na pia Hongera na wewe:-)
ReplyDeleteEster! Nimeupenda huo msema kwa kweli..Ahsante ndugu wangu!!
KWELI MWAYA WEE1! raha jipe mwenyewe na waubavu wako.kweli tulikumosso saniii. mimi nahesabu siku naenda kujipa raha BONGO .kaka s
ReplyDeletehahahaha! Hii ni kuumizana roho eti "mimi nahesabu siku naenda kujipa raha BONGO" Kaka Sam, haya basi twasubiri dhawadi..LOL
ReplyDeleteKimya chako kilikuwa pouwaa kumbe umefaudu sana tuu!!!
ReplyDeletej'Mosi njema nanyie pia.
Wakati mwingine lazima raha upewe siyo ujipe mwenyewe.. inategemea ni raha gani so to speak.
ReplyDeleteHaya Kachiki ..kumbe hata hukunimiss..LOL. "Umefaudu" nahisi ulitaka kuandika "Umefaidi" yaani hasa kupata hiyo zawadi natamani nialikwe kwenye sherehe na niivae.:-)
ReplyDeleteMwl. Mhango! Nakubaliana nawe raha si lazima ujipe. Au pia inawezekana raha kupeana au kumpa/kuwapa mwingine/wengine...
Misemo ya siku hizi ni mingi mnooo, kila mara inazaliwa mipya
ReplyDeleteUmekula,umekunywa,umepumzika na sasa umerejea maskani na nguvu mpya ukiwa mwenye tabasamu laini kwa afya njema.
ReplyDeleteKaka S, nami kama wewe nahesabu siku kikapewe maraha....hahahahaha!!! kaka Mhango nakubaliana na wewe kabisa kaka yangu..
ReplyDeleteIla Yasinta nimekukubali kwa kula raha mwanawane..
jamani dada yasinta nimekupenda bure,waonekana mpole wala huna makuu...na mimi mume wangu ni nyoni,wangoni wa songea.
ReplyDeletemama nyakomba!