Monday, May 21, 2012

BAADA YA MAPUMZIKO NIMEONA TUANZA JUMATATU HII KIHIVI!!!

Ni matumaini yangu kuwa wengi wetu  twnajua/twakumbuka hapa ni wapi. Labda tu niuliza Je? unajua hapa ni wapi?...Nawatakieni mwanzo wa juma hili uwe mwema.

12 comments:

  1. Hapa naona lakini nashindwa kutoa jibu la moja kwa moja.Acha wengine waendelee!!

    ReplyDelete
  2. Mie sijui!

    Ila... nakutakia mwanzo wa JUMA uwe kibonge kwako pia!

    ReplyDelete
  3. kaka Ray na Kaka Simon nilitegemea ninyi mngeweza kujua hapa ni wapi:-( Haya nawe uwe na bonge la mwanzo wa juma..Kadoda.

    ReplyDelete
  4. Labda piga kwa upande mwingine! Nikitaja itakuwa ni KUBUNIA tu! Ila ningependa kweli kujua kila kitu... ila maudhaifu ya UBINADAMU tu yanafanya mambo mengine kama sehemu nyingine hata zile zisizo sehemu za siri nisijue!:-(@Kadala Yasinta

    ReplyDelete
  5. mimi sijatembea sana lakini hapo ni bagamoyo
    Che JIAH

    ReplyDelete
  6. TUNASUBIRI UTUJUZE HAPO NI WAPI MAANA INAONYESHA WOTE LEO UMETUCHEMSHA ILA KAMA NI SONGEA UNGETUELEZA NA WENGI WANGEJIBU ILA INAONYESHA HPO NI MAJENGO YA WALE WATAWALA WETU NA HILI NI KANISA BASI TUANGALIE KULE MWANZA BASI
    CHE JIAH

    ReplyDelete
  7. @Yasinta;
    Mimi na mtani wangu Simon umeamua kututania kuwa sisi kama sisi na wao kama wao sote ni wamoja.Kama ni Songea sisi hatujasogea na kama si Songea na sisi hatusogei ila wao kama wao na waendelee kusogea na wakifika Songea na sisi tutakuwa tumesogea.

    ReplyDelete
  8. Ndugu zanguni! Naona picha hii imekuwa ni vigumu kugundua hapa ni wapi..Basi ngoja tu nichukue nafasi hii na kusema hapa ni wapi. Nilifikiri watu wangegundua ni wapi kumbe imekuwa ni vigumu sana. hapa ni SONGEA BOYS Sec. School(LUILA) kwa wala waliosoma Boys sasa mnakumbuka enzi hizoooo sasa kumebadilika. Ahsante kwa kuwa nami .

    ReplyDelete
  9. Dah ... umeumiza sana kichwa changu. Hisia na mawazo yangu yote ilikuwa ni picha ya eneo la Songea Boys, tatizo sikuwa na uhakika zaidi mpiga picha alikuwa amesimama wapi.

    Hilo jengo linaloonekana ilikuwa ni maktaba ya shule (sijui kama bado ni maktaba mpaka leo). Hilo eneo linaloonekana hapo mbele ya jengo, ilikuwa ni Assembly Area na kuna mlingoti wa bendera. Hii njia inatoka General Office (Staff Room na Wakuu wao) kuja assembly area. Marehemu Philip Nkoma alikuwa akipita hapo siku za Jumamosi kuja kwenye Master Parade.

    Nyuma ya mpiga picha kushoto kun Staff Room na kulia kuna madarasa mengine ya O-Level pamoja na zahanati. Nyuma ya kuna barabara inayokwenda kuungana na barabara ya Tunduru - Songea.

    Kulia kwa hilo jengo kuna kijengo kinaonekana kwa mbali, ilikuwa ni Geography Room na mara nyingi ilitumika kwa vipindi vya wanafunzi wa A-Level na pia F6 wa arts walitumia kama sehemu yao ya kujisomea nyakati za Prep.

    Majengo yanayoonekana kushoto yalikuwa ni madarasa ya O-Level na mbele yake kidogo kulikuwa na maabara ya Fikizia ambayo ilitumiwa mara nyingi na wanafunzi wa F5 PCB; pia kulikuwa na maabara ya kupasua vyura (Biology) ambayo ilitumiwa na F6 PCB.

    Nyuma ya Geography kulikuwa na mabweni ya Uhuru na juu yake kulikuwa na Bwalo. Upande wa kushoto mara baada ya maabara kulikuwa na mabweni ya Muungano. Mabweni mengine yalikuwa juu zaidi kuelekea kijijini (ulokoni) ambayo ni pamoja na Ujamaa na Maendeleo. Then upande kulia baada ya mabweni ya Uhuru na Bwalo, kulikuwa na mabweni ya Azimio.

    Best yangu Yasinta asante sana kwa kunipa kumbukumbu nzuri. Ubarikiwe sana, ningejua unachopenda sana ningekupa kama zawadi. Kwa muda wa wiki nzima kuanzia leo nitasitisha utani.

    ReplyDelete
  10. Duh! Kumbe Mtani umesoma hapo aise. Yaani katika maeelezo yako inaonekana kama vile upo hapo unatembea tembea vile...Mtani huhitaji kunipa zawadi kwani tayari umekwisha nipa. Ahsante sana.

    ReplyDelete
  11. @Yasinta;
    Asante kwa kutusogeza Songea.

    ReplyDelete
  12. songea boys' secondary school,skuli yangu nafundisha hapa!nimepnda,je ulisoma hapa nn?

    ReplyDelete