Monday, April 23, 2012

TUANZE JUMATATU YETU KIHIVI:- JE UNAJUA HAPA NI WAPI?

Wengi wanaotokea kusini kwetu wanajua hapa ni wapi ila hata wale wasiotoka huko nadhani mtajua hapa ni wapi...haya tuona kama tunakumbuka Geografia ya nchi:-)....Jumatatu njema

11 comments:

  1. Rafiki huu ni msitu kati ya Mafinga na Nyololo! Kuelekea njia panda ya Brooke Bond Mufindi kwa kupitia Ng'wazi....upo hapo?

    ReplyDelete
  2. Kwa kumbukumbu zangu za JKT,mafinga enzi zangu.hapa ni baada ya kutoka changarawe unashuka kilima kuna msitu mkubwa tu unaofananahivyo.ila kama siyo hivyo basi bado ni maeneo ya mafinga .kaka s

    ReplyDelete
  3. Hapa ni ndani ya msitu wa Sao Hill - Mafinga

    ReplyDelete
  4. Hapa ni ndani ya msitu wa Sao Hill - Mafinga

    ReplyDelete
  5. Mimi hapa leo napita tu.
    Hii ni mandhari nzuri iliyohanikizwa na uoto wa kijani kibichi ikiwa sehemu ya mazingira maridhawa.Nami hisia zangu zinanituma mkoani Iringa.

    ReplyDelete
  6. Huu ni msitu wa miti ya mbao wa Mafinga, nikipita hapo huwa navutiwa sana, hii picha nimeipenda na mpiga picha kapatendea haki

    ReplyDelete
  7. Hapo ni yale maeneo ambayo Zitto aliwindwa akashindikana....Iringaaaa!

    ReplyDelete
  8. ni raha ya aina yake kuona Geografia ipo sawa:- Kwa mujibu wa picha hii hapo ni MUFINDI. Nami nasema ni kweli kwani ni mwaka jana tu nimepita hapa... ruksa mjadala kuendelea.....

    ReplyDelete
  9. Hilo ni eneo la misitu ya mbao SAO HILL Wilayani mufindi mkoani iringa....Japo kwasasa jamani msitu huo unaelekea kupotea kabisa kwani aliyeingia ubia wala hana mpango wa kuendeleza kama ilivyokuwa awali chini ya wazawa...

    ReplyDelete
  10. YES, NACHANGANYAGA MUFINDI NA MAFINGA

    ReplyDelete
  11. Iringa kuelekea njombe

    ReplyDelete