Kama kawaida ni kile KIPENGELE CHETU CHA MARUDIO MBALIMBALI YA MADA, PICHA NA VITU VINGINE MBALIMBALI. NA LEO TUANGALIE KUHUSU MAPAPAI. Hiii niliiweka hapa kibarazana lakini kama mnijuavyo huwa napenda kurudia kusoma kitu ili nielewe zaidi. kusoma maoni mazuri ya wasomaji gonga KAPULYA. Karibuni sana.
Hapa ni mti wa papai, leo nimekumbuka faida mbili za majani ya mipapai moja ni dawa ya tumbo hasa kama una tatizo la choo kubwa . Unachukua hayo majanai na unachemsha na halafu unakunywa yale maji yake. Pili ni sabuni unaweza au niseme mimi nimewahi kufulia nguo ila usifulie nguo nyeupe basi itakuwa kijana. Nguo nyingine zote sawa kabisa.
Na hapa ni tunda lenyewe nalo lina faida zake kwanza ni kwa ajili ya kula ni tamu sana na pia nalo kama una tatizo la choo kubwa ni nzuri. Halafu jambo jinginge papai ni kilainisho kizuri sana cha chama hasa nyama ya ngómbe. Toa hizo mbege weka kwenye chombo, pondaponda papai na uchanganya na hizo mbegu koroga taratibu katakata nyama vipande vidogovodogo weka humu kwenye mpondo na subiri masaa kadhaa. Hakika utaifaidi nyama yako mno itakuwa lainiiii. Ila kusema kweli nimetamani kweli papai ni muda sasa sijala:-). PANAPO MAJALIWA BASI TUONANE TENA KATIKA KIPENGELE HIKI JUMATANO IJAYO!!!!!!
Tunda tamu sana hili,hasa ukilipata lenyewe....lililoiva mtini, sio la kuivishwa...wewe
ReplyDeleteemu3! na kweli ukilipata lile lililoivia mtini mmmhh utajinoma...Siku moja nilikuwa dukani hapa nikaona papai ukubwa wa embe dodo na bei hiyo mbona niliacha na kukimbia....Halafu jaribu na Juisi ya papai ni tamu sana....
ReplyDeleteUtamu wa papai hauna maelezo na ni tunda maridhawa kwa familia.
ReplyDeletebasi faida nyingine ya mpapai au papai ktk mambo ya kiasili {sio ushirikina}kama kuna mtu anakusumbua au anakuletea bugudha katika shughuli zako basi unachukua papai dogo bichi na kitu fulani kutoka kwa huyo jamaa unalitoboa unaweka hicho kitu halafu unapeleka jalalani kwa manuizo basi ndani ya siku tatu anakukimbia yaani kwa yule mtu msharishari mgomvi hiyo inaitwa kupigwa kipapai jamani tusisahau jadi zetu na ndio faida nyingine ya huo mti
ReplyDeleteWadau, miye ndo nishapanda kama heka moja na nusu ya mipapai. Nimeanza kwa majaribio. Naomba kama una utaalamu nimwagie kwa moddyguyz@yahoo.com ama twende kwa sms 0787519910. Shamba lipo hapo Kimanzichana wilaya ya Mkuranga. Shamba ni kubwa lakini nimeanza na heka hiyo moja na nusu.
ReplyDeleteNinapenda ushirika na ubia katika kilimo hicho, karibuni tafadhali....
This comment has been removed by the author.
ReplyDelete