Friday, March 16, 2012

UNAJUA KISA CHA WANGONI KUAMKIANA MONILE??

Ni hivi:- Kulikuwa na mzungu pale Peramiho aliyejenga lile kanisa. Na aliishi miaka mingi pale Peramiho. Mzungu huyo alikuwa na tabia ya kuamka asubuhi na kupita kuwatembelea watu majumbani mwao. Yaani kwa nia ya kuwajulia hali wazee na vijana. Yeye alipenda sana kutembea kwa mguu, toka Peramiho Hospitali mpaka njia panda ya kwenda Mbinga. Kijiji kimoja kiitwacho Lipokela. Na baadaye kurudi.
Sasa yeye kwa kuwa alikuwa hajui kiswahili na alitaka kujifunza. Basi alikuwa ana wasalimia ile GOOD MORNING!
Kwa mkato yaani MORNING na wale wazee wakawa wanamuuliza tukujibuje? Naye aliwaaambia mujibu MORNING. Basi wale akina BAMBU wakawa sasa ni kila mtu wakimuona asubuhi wanasema MONILE.... wanajibishana MINILEEE...Kisha wanamalizia TUWAONE....jibu lake ..YEOO..Yaani tumemwona leo mzungu ndiyoo.
Basi toka miaka hiyo mpaka leo WANGONI wanasalimiana hivyo. Ikiwa Asubuhi MONILE...MONILE ..TUWAONE BAMBU ...YEOOO
SIKU NJEMA NDUGU ZANGUNI!!!!

16 comments:

  1. Kumbe hicho kithungu,Ahsante da'Yasinta kwa kutuelewesha.

    ReplyDelete
  2. Dsda Yasinta MONILEE ,.
    Nasi tuanze kwa salamu hiyo ...
    tumepata maana yake asante sana nawewe monile tumemwona mzungu YEWOO ..Haya umusalimie huyo bambu hapo nyumbani,lakini hawa babu zangu wangoni ni wabunifu sana wa lugha
    kwahiyo kabla ya hapo walikuwa wanasalimiaje?
    CHe Jiah

    ReplyDelete
  3. pia kunakabila fulani ,wanatumia maneno yaliyo toholewa kiingereza, isipooni, isopu.wakiwa na maana kijko na sabuni.sasa sijuwi nawao ilikuwaje labda kuna mtu analijuwa kabila hili atujuze wana janvini. haya da Yasinta,bisikuti yanguRachel,che Jiah,Ray Monile. kaka s

    ReplyDelete
  4. vizuri mbogo wewe unajuwa kabisa kuwa hao ni wale wana kukaja wa kule ileje akina kibona ndo wanatumia sana ispooni na isopu mimi nilikuja wajuwa hawa rafiki zangu nilikuwa nao miaka hiyo nasoma nao kule mbinga hawa kwakweli nami nilikuja wasikia hinyo wanaongea ila nitakuja kujua walianzia wapi habari hiyo ila hii ya hawa ndugu zangu ya monile tumwachie dada atueleze kabla ya monile walisalimianaje? labda amwulize yule mzee wa nyasa atatuambia
    CHE jiah

    ReplyDelete
  5. Tukopamoja Che Jiah. Che, unajuwa najikuta tu nataka kukuuliza wewe ni Che chipoku,nsumari ,chichemi, che nkapa? unatoka kwa hawa rafikizangu wa ntwara/lindi.samahani kwa kuanza hivyo ila kunakitu nilikuwa nataka kukuuliza kuhuzu akina Che. haya kwetu salaam hai in giliani kabisa na chizungu,Mwangaluka/mwadila au mwandila,yote poa tu ila sijafuatilia kwa ukaribu kujuwa, mimi nikisema mwangaluka na mija nae anasema mwangaluka,nani kamdesa mwenzie,mija tafadhali,nawengine wanaojuwa mnijuze hapa. kaka s.

    ReplyDelete
  6. KUMBE NDUGU YANGU WEWE NILIKUWA NAJUWA KUWA NI NDUGU WA DAMU ILIKUWA VIZURI KAMA UNGENIJULISHA KAMA MWENZANGU UMETOKA KULE AMBAKO RAFIKI YANGU KITAMBO ALIMPELEKA MZUNGU SAFARI ALIPO MUULIZA :NI KILOMETA GAPI TOKA NZEGA MPAKA KAHAMA JAMAA AKAJIBU TWENTE TU MZUNGU ALIWASHA GARI MPAKA TNDE AKAMULIZA TENA BADO KILOMETA NGAPI JAMAA AKAJIBU TWENTE TU KUFIKA MWENDA KULIMA AKAULIZA TENA BADO GAPI AKAJIBU TWENTE TU HAPO MZUNGU AKAMSHUSHA MSUKUMA AKAMWAMBIA NIMEKWENDA KILOMETA NYINGI SANA UNASEMA TWENTE TUU SHUKA AKAMPIGA MAKOFI NA KUMWACHA PALE AKWASHA GARI MPAKA KAHAMA NA YULE MZUNGU AKUHAMA TENA KULE KAHAMA
    POLE HICHO NIKITENDAWILI MBOGO TEGUA UKIPATA NITAKUOZESHA MWANANGU RACHEL S ISAAC
    CHeJiah Issack

    ReplyDelete
  7. kivingine kidogo.

    mie nadhani kamchapo/hekaya hii imetengenezwa ili ifiti mazingira. je kabla ya mzungu huyo wangoni walikuwa wanasalimianaje? au hawakuwa na lugha ya kuongea. kama walikuwa na lugha, basi lugha hiyo haiikuwa na sehemu ya salamu. kama hawakuwa na lugha basi kingoni kingefanana na kizungu kwa asilimia 90 na zaidi. tukipata jibu, uhalali wa hiki kibwagizo cha leo utakuwa 'unaswihi'

    ReplyDelete
  8. Wewe dada mbona huingilii hii mada watu mpaka wametoka kwenye mstari nawewe ndo muhusika hawa ndugu wamefikia hata kuulizana jibu majibu ya watu umeulizwa na mwaipopo na che jiah kimyaa toa maamuzi

    ReplyDelete
  9. Haya ndugu zanguni MONILE...SikukaA KIMYA bali ilikuwa ni makusudi:-) ni kwamba kabla ya mzungu kuja wangoni walikuwa wakisalimia MYIMWIKI NA JIBU LAKA MYIMWIKI au akiwa mmoja UYIMWIKI...JIBU NIYIMWIKI..

    ReplyDelete
  10. Sawa Dada Tuyimwiki hapo sasa nadhani umemaliza kibaraza cha leo nami ndicho nilikuwa nakijuwa kabisa ,Sasa mwambie kaka yako mbogo pole kwani kupigwa na mzungu kwa ndugu yake yule wa kisukuma kwa kumsumbua mzungu wa watu kila akipiga speed kilometa 20 zilipit yeye anasema twente tuu kumbe anasema twende tu hayo yalimkuta rafiki yangu mmoja anaitwa mwanakitambo
    asanteni ila mwambie MIMI NIMZALIWA WA KUSINI KANDA YOTE YA KUSINI NAWAJUWA KAMA ANAHITAJI NIMPATIE email aseme tuwasiliane ila kwao tumeolea akitaka kujua kwanini naitwa CHE NITAMWELEZA MAANA YAKE
    CHe Jiah

    ReplyDelete
  11. Aaaa! baaa! bwana wewe che jiah mbonimambo! chacha makubwa! wewe uniletee tu huyo che mwali Rachel ntakuchukulu chanaa. unajuwa nimecheka mpaka mwanangu kani uliza baba vipi mbona unacheka! anyway haya mkuu tutawasiliana tu tuko pamoja namsubiri chemwali Rachel!!?. kaka s

    ReplyDelete
  12. Hahhahaahaaahaha!!!!Yaani Chocolate wangu Mwana wa mbogo baba yangu Che Jiah mzee Isaac amekutunuku hahahhahaha yaani nimecheka leo mpaka basi,Asanteni sana Waungwana, kibalaza leo kilikuwa poa,dadake Yasinta tupe japo Kahawa yakhe ile chengu ya vikombe vidogo!!!

    ReplyDelete
  13. Dada Yasinta unadaiwa kahawa na wadau kwani wewe jana umeleta mdahlo mrefu mpaka watu wakvalishana pete sasa mimi mzazi wa Rachel nataka mahari yangu toka kwa kaka yako sam na faini juu kanivunjia heshima sana Na wewe mwanangu unafurahia nini kupewa mimi mahari ya ngo'ombe hewa ndo umefurahi hivyo? leo nimekasirika sana mwanagu ila nimeongea na shangazi yako YASINTA Kasema atawasilana na mbogo atamdai mahari yako kwani mimi nilikataa kupokea.
    Che Jiah

    ReplyDelete
  14. Hahhahahaha baba yangu Isack che Jiah, jamani sijafurahi kabisa, tena Ng'ombe mwenyewe TASA!!!!Bora ukatae baba yangu kwanza kaniambia eti ananifanyia mazoezi kunipeleka kwao kulima viazi yaani nipasue matuta, kama Wakwe wakikubari ndiyo Ndoa"""

    ReplyDelete