Saturday, March 17, 2012

MWONEKANO MPYA WA KAPULYA....

Hapa ilikuwa mwaka huu 2012/5/1 nilipopiga picha hii nikiwa nimesuka nywele za kimasai ......
...na hapa ni leo nimefumua zile nywele za kimasai na sasa nipo naturel /yaaani na nywele zangu nilizozaliwa nazo. Watoto wangu wameshangaa kwani nilifumua zile rasta minywele yangu ilikuwa mirefu si kawaida baada ya kuosha zikashiling/rudi na kuwa fupi...Yakajia maswali umenyoa mama?...ila wote wamependa mwonekano wangu mpya . Je wewe unayeangalia ni mwonekano upi unaupenda niendelee nao? JUMAMOSI NJEMA KWA WOTE....NA KUMBUKENI WOTE MNAPENDWA :-)

14 comments:

  1. Rafiki mbogo unauona ugomvi huo anauanza dada yangu? mimi sijtoe maoni mpaka wewe useme kwani mtani wako dada yako anataka kwenda kwenye mashindano ya urembo leo hii jumamosi sasa fanya haraka kumpa jibu ajiandae pe salamu mimi dada ninzachosema ni kuwa nakutakia mashindano mema
    Che Jiah

    ReplyDelete
  2. Muonekano asilia ni maridhawa bila madhara.Wikiendi njema kibarazani.

    ReplyDelete
  3. Muonekano asilia nao unakupendeza kumbe.. Safi sana.

    Umependeza zaidi bila umasai

    ReplyDelete
  4. VIPI Mbogo hujaamka MKWE wangu? mwanagu Rachel Isaac hajakuamsha? Nawe mwanangu Rachel amka toa maoni yako shangazi yako Yasinta anataka kwenda kwenye mashindano ya warembo anataka ushauri wako tao maoni yako mwache huyo mkwe wangu mbogo aendelee kulala mpe maziwa ya ng'ombe anywe akiamka atatoa maoni yake
    mimisiwezi kumshauri Dada yangu kuwa anaonkana amependeza au la ila napenda anonekane kama alivyozaliwa pale nyumbani Ruhuwiko
    Dada chagua uasilia kama upendavyo kula vitu vya asili
    Che Jiah

    ReplyDelete
  5. Yaani nimecheka mpaka basi tu..huu wala si ugomvi na wala si kutaka kugombea shindanno la urembo...isipokuwa ni muonekano wa asili yaaani mimi kama mimi...ila niwachekeshe kidogo hapa jana jioni Kijana Erik kaniangalia na akasema mama, unaonekana mzee bila rasta...

    ReplyDelete
  6. yaani hapo umependeza sana huyo mwanao anakudanganya wala hujazeeka ,umependeza hasa nywele kipilipili bwana asikudanganye mtu sio hayo mauzi unayajaza kichwani

    ReplyDelete
  7. Haya njomba nachukuru chana, maana baaaa! bwana wewe che Jiah, huyu chemwali Rachel amakweli nakuchukulu kwa kuniachia tulikuwa vile tukicheza likasaula chonde chonde! bwana weweee!. Da Yasinta kiukweli hatua ulio chukua ni bubkubwa safi na uamuzi huo si mchezo unataka moyo.sasa kipengere cha kupendeza, au hujapendeza ni hatua nyingine. kinacho fuata ni matunzo najinsi unavyo taka ziwe,ukitaka ziwe virasta vidogo dogo unaweza kupendeza pia,wewe fanya majaribio nahizo nywele za asili utapata mtindo ambao utakufaa .ila ukitaka nikusaidie nitafute. kaka s.

    ReplyDelete
  8. Vivyo hivyo natamani wanawake wajipambe kwa mavazi yenye mpangilio mzuri, pamoja na kiasi na utimamu wa akili, si kwa mitindo ya kusuka nywele na dhahabu au lulu au mavazi yaliyo ghali sana,bali kwa njia inayowafaa wanawake wanaodai kumheshimu Mungu, yaani, kupitia matendo mema. _1Timotheo 2:9,10.

    ReplyDelete
  9. Umependeza sana MWALI WEWE!!!Duhh tumekuwa wengi na Nywele hizi sasa,Jana nilipita blog moja nikakuta wametuua/kutucheka,sanifu Eti ukiwa na nywele hizo/hizi Unatofauti na baba yako!haaahahaha!

    @baba yangu Isaack Che nimeamka hahahhhaha maziwa ya Ngo'mbe na bili hizi baba?

    Hahhaahahhaha bwanawewe baa Sam mwana wa Mbogo!!!!

    @da'Yasinta Erik anawasiwasi hahahhaha.

    ReplyDelete
  10. Umetoka chicha ile mbaya. nimelipenda pozi la hiyo picha ya chini. safi sana da Yasinta.

    ReplyDelete
  11. mwonekano wako ni mzuri sana ila ungesokota dred za asili ungependeza na ukifanya hivyo naomba unitumie picha maana i lke u!

    ReplyDelete
  12. mi napenda uonekane kama picha ya pili ambayo umefumua kwani umpendeza sana.

    ReplyDelete