Wednesday, March 14, 2012

KUVAA SHANGA... NI UREMBO AU?

Ndiyo ndugu zanguni ni JUMATANO TENA na ni kile kipengele chetu cha MARUDIO..katika pita pita nimekutana na mada hii nikaona si mbaya tukirudia kujadili tena . Nimeipata hapa.
watu huvaa shanga kwa maana nyingi naamini, hivi shanga zina maana ngapi? najua maana za nyekundu, nyeusi na nyeupe je nihizo tu ama na rangi nyengine pia zinamaana tofauti? na wanaume hupendelea nini kwenye shanga? na wanawake waova je hujisikiaje kuwa nazo..


kuna wakati nilikuwa navaa shanga kwenye kiuno sio kwamba nilipenda ila mpenzi wangu kipindi hicho ndio alikuwa anapenda nivae akisema anapoziona anasisimuka lakini baada ya kuachana naye nikaachana nazo kwakuwa sikuwa nazipenda kuvaa bali kumridhisha tu..

kitu cha kushangaza ni kwamba kuna rafiki yangu anaolewa karibuni mchumba wake amemletea shanga avae, anasema yeye anapenda kumuona mpenzi wake akiwa amevaa ndipo nilipo mshauri azivae baada ya kumpa story yangu hapo juu..

wanaume kuna raha gani ambayo mnaipata pindi wapenzi wenu wanapo vaa shanga????na je ni wanaume wa makibala fulani ama wote kwa ujumla? maana rafiki yangu huyo mchumba wake mkuria na ndicho kilicho zidi nishangaza...na mwanaume aliyenifanya mimi nivae ni mmakonde ndio inazidi kunichanganya..

sio vibaya nikufahamishana tu ili tujuwe kama tutaendelea kuzivaa ama tuziweke kapuni.....

TUTAONANA TENA JUMATANO IJAYO KATIKA KIPENGELE CHETU CHA MARUDIO!!!

26 comments:

  1. Shanga hereni bangili mimi nahis ni mapambo tu, sizani kuwa yanaongeza chachizo fulani, ni wewe mwenyewe kama unapebnda huo urembo kwa mkeo basi zitakuvutia!

    ReplyDelete
  2. Desturi,mila na tamaduni zetu ni sehemu ya maisha na mafanikio.Wewe ukisema cha nini mwenzio anasema nitakipata lini?Hatuwezi kuwasemea wala kuwahukumu wadau wetu wanaoendelea kulinda na kuhifadhi mila,desturi na tamaduni zao bali acha wao wenyewe watuelimishe na kutushawishi pale inapowezekana.

    ReplyDelete
  3. this is what we miss as African men nowadays. Our ladies ought to go back to our culture and start again putting on beads. In the past all married women had to wear beads.

    ReplyDelete
  4. Naungana na ray njau
    ukweli ni huo kuwa huwezi kuusemea moyo wa mtu wengine wanafuata mila kama kwaida ila wengine ni fasheni kwavile wamesikia watu wanapagawa nazo, kumbe hayo mambo waliyaweza mabibi zetu hapo siku za nyuma wanakueleza kila ushanga una maana yake ukivaa mmoja ,ukivaa miwili nk. hivyo hapo nyuma bibi akivaa shanga mmoja babu alikuwa anajuwa leo bibi hastahili kuguswa kama wiki wiki anajua yupo kwenye siku zake yaani piriod, na siku akisha maliza piriod anamvalia babu zile za mvuto hapo babu anajuwa leo ameruhusiwa kubabuka, sasa hawa bibi au watu wetu wa siku hizi hajuwi maana ya hizo yeye siku ya piriod ndo anakupigia zile ili uchanganikiwe zaidi na hata kama yupo nahiyo piriod hakuambii ye anajali maslahi zaidi ukweli pambo hili kwasasa mtu anavaa kiushabiki tuu hajuwi maana wala sababu ya hizo shanga hivyo kusema kuvaa shanga kunachochea mvuto kwenye mapenzi ,kwa miaka hii nasema hamna mimi ndo wazo langu kwa leo
    CHe Jiah

    ReplyDelete
  5. Issack unachosema kinaweza kuwa naukweli mia kwamia. tatizo letu sisi watanzania tuwashabiki sana wamambo ambayo tumeyakuta na yanayo tokea.kuhusu shanga,hakuna kiukwelia ambaye amewahi kueleza zina mahusiano gani na kujamiana/ngono.maranyingi niujanja ujanja wa baadhi ya wanawake/wadada kuhusisha shanga na mahaba.wengine husema ni ushamba,wengine husema ndoutamaduniwetu,swali enzi zile nikiwanda gani afrika kilitengeneza shanga,kama siyo biashara za waarabu nawatu kutoka china.kwamaana hiyo kabla ya hilo mama zetu,bibizetu walivaa vitu vingine katika kuhamasishana wakati ngono.mi sijuwi ila vijiwe ndo vinakuza mambo yote haya,japokuwa baadhi makabila yanajuwa umuhimu washanga lakini siyo mwanamke akivaa shanga ndo anadumisha utamaduni /mila!?.ukisema ni urembo naweza kukubaliana nawewe,pia kama issack alivyo sema kamanjia ya kujikumbusha siku zake mwanamke ,japokuwa itakuwa zilipoingia shanga ndo zikaendeleza urembo badala ya kufunga kamba au sijuwi nini kilitumika kutoa ishara aliyosema issack. kaka s.

    ReplyDelete
  6. Wazee hizo zina raha yake hasa wale wanaojua kucheza nazo, Wanawake
    wengi wa huku kwetu pindi wanapo wekwa kwa makungwi hupewa somo la
    uvaaji wa hizo mbwasha kwa ajili ya kunogesha mchezo kunako uwanja wa
    seremala, tena kama kafundishwa na jinsi ya kupika mkuyati kwa ajili
    ya kuongeza chaji betrii ya nyama ( ! ) siku akikukandamizia 3 lazima
    vurugu za mahaba ziendane na idadi yake. Siku akikuvalia 6 utafute na
    pakutokea kabisa maana utakuwa kama umesusiwa sinia la Biriani.

    Na kwa wale wapenzi wa mpira mara nyingine huwa zinavaliwa zenye rangi
    ya Timu au ukijulikana niwa timu gani halafu siku hiyo ikawa
    imeshinda, Basi zitavaliwa kama idadi ya magoli inavyo onyesha, Kazi
    kwako ukutane na dhahama ya magoli mengi kama ile gemu ya jamaa
    waliobatizwa jina la utani la Man 6.

    VIGEZO NA MASHARTI KUZINGATIWA.

    Nmemnukuu
    -Mohamedi Mtoi

    ReplyDelete
  7. Duuhh leo naona uwanja wa wanaume, Wanawake mkowapi?Teheteheteheh ooohhiiiii!!!

    ReplyDelete
  8. Nachukua nafasi hii na kusema ahsanteni sana kaka zangu na dada Rachel kwa mchango wenu ama kweli wote waliopita hapa wamejifunza kitu kwa kusoma alichoandika mwingine maana ndio kujifunza. Kwa mimi binafi bahati mbaya au nzuri nilichelewa kumuuliza mama swali hili ila nakumbuka nilipokuwa mdogo nilikuwa naona watoto wadogo hasa wa kike wanavalishwa hizi shanga na nikauliza kwanini nikajibiwa ni kutaka umbile lake liwe zuri...Sasa haya mengine mweh kwa mimi ni urembo tu kama vile nivaovyo kidani.....Hapa kwenye maelezo wamesema walivaa tu ili kuwapendeza wapenzi wao. Je? Ni sahihi hiyo kufanya kitu akipendacho mtu mmoja? Hata kama wanasema MAPENZI YANA NGUVU KULIKO MAUTI.

    ReplyDelete
  9. Hapa Yasinta umekuwa mkali kidogo kulikoni?

    ReplyDelete
  10. Kaka Ray! Una maana gani kusema kuwa nimekuwa mkali?

    ReplyDelete
  11. Kamala tusaidie kufafanua maana umesema hujuwi na kisha ukasema umemkatisha tamaa kabisa....
    Tukubaliane leo au kesho kuwa shanga kidani na hereni na kipini pia ndonya ni vitu vya UREMBO kwa mwanamke wa kiafrica... nyingi ya familia za kiafrika zilitumia urembo huo,, hii ni hata kabla ya karne ya 19 ukisoma historia shanga zililetwa na waarabu na waasia ila urembo wa asili kabla ulikuwepo wengine walidiriki kusinga kamba na kuvaa shingoni na ngozi pia zilitumika kwa urembo ,kuna wale wengine walitoboa pua ,masikio, na hata mdomo kuweka urembo ,hao nao walichochea urembo wa mwanamke na urembo wa mama yaani mwanamke pia waweza sababisha mvuto wa kupata magoli mengi huwezi kuwa na mvuto au speed ya kufunga magali mengi ukiwa na kitu kimesheeni harufu au nk ,tukirudi miaka yenu hii ya kizazi kipya cha 80 ndo mnashukiwa kuharibu mambo mengi mmeelekeza kibiashara zaid
    mimi nimekaa JANDO miesi kama 2 hayo mambo sisi enzi hizo tulikuwa tunaelekezwa na miaka ile jando kama mimi niingia nikiwa na miaka 11 tosha kabisa kwani ukiniuliza jambo nililoambiwa mwaka1974 leo hii nakuambia si utani kwakweli ila sasa angalia wanapelekwa jando miaka hii kule kwetu ni mtoto hata kunyonya hajaacha niliona mtoto alipelekwa jandoni alianza kulia toka siku ile mpaka anarudi je pale amekwenda kupata maadili au karaha hapo ndipo mambo yalipoharibika tangia mwaka 80 nakuendelea mimi leo sisubutu kumpeleka mtoto wangu jando kwanza akizaliwa siku ya tatu anapigwa suna yaani we acha hayo ndo yamepelekea mambo ya mahaba yahribike ,kuvaa shanga na urembo mwingine kiunoni ni kweli kunaleta mzuka kwenye mahaba kwa wengine mimi simo na kuna wengine tunapenda urembo wa nyele n.k tutazua mjadala mwingine bure ngoja niachie hapo
    sam mbogo asante na da yasinta poleni
    che jiah

    ReplyDelete
  12. Ukali wenyewe ndiyo huu Yasinta:
    ----------------------------------
    .Sasa haya mengine mweh kwa mimi ni urembo tu kama vile nivaovyo kidani.....Hapa kwenye maelezo wamesema walivaa tu ili kuwapendeza wapenzi wao. Je? Ni sahihi hiyo kufanya kitu akipendacho mtu mmoja? Hata kama wanasema MAPENZI YANA NGUVU KULIKO MAUTI.

    ReplyDelete
  13. shanga pamoja na urembo bado unaleta hamasa kwenye mambo ya fundi selemara kama alivyosema mtakatifu kitururu,zamani ilikuwa ni kutoa ishara kama alivyosema ukuvaliwa ushanga mwekundu ni kwamba uwanja umechafuka hivyo kunakuwa hakuna mechi vilevile ushanga mwekundu unamfukuza jini mahaba hasakwa wale wanoota ndoto za kufanya mapenzi usiku.....bila kuwa na mwanamme.

    ReplyDelete
  14. ukikutana na mwanamke wa kitanga anakwambia hesabu zote ndio nitakuruhusu kuondoka ukistuka umelala nyumba ndogo bila kujua

    ReplyDelete
  15. Hayo ni mapokeo tu tuliyoyarithi kutoka kwa babu na bibi zetu,kama ulivyosema wengine wamejenga hisia kuwa akiwa na mpenzi aliyavaa shanga aski ya kukuitanae kimwili inakua kubwa. sual al amwanaume wa kabila gani hilo halina mshiko maana kuna kuiga kwingi siku hizi.

    ReplyDelete
  16. Mambo mengi hata ya starehe za ngono yanategemea jinsi tulivyokua na kuiona dunia. Utagundua pia kwamba hata our sense of aesthetics au kutambua uzuri inategemea makuzi au jamii tulikokulia. Wanaume Waswahili wanapenda mawowowo ambayo ni makubwa na round. Watu wa magharibi wengi wanaona matiti makubwa ndiyo dili, na makalio yanatakiwa kuwa flat. Je hapo?
    Sasa angalie pia lingerie za kimagharibi. Kuna nyingine nahisi utaona hazina mvuto kama vile ambavyo nilijaribu kuwaelezea vijana wa Kimarekani kwamba kanga nyepesi kwetu ni lingerie yenye kuamsha hamu sana. Vijana walinishangaa hawakuona chochote cha kuvutia hapo. Kuna watu wanafikiri hakuna nywele za kuvutia na kuamsha ashki kama blonde wakati wengine wanaona nywele nyeusi tii ndiyo hasa zenyewe.
    Ongezea pia msemo wetu wa urembo wa ndonya.
    Binafsi simshangai asiyezipenda shanga, ingawa mimi mwenyewe ni mshabiki mkubwa kabisa. Kwa wengine ni urembo tu, na kwa wengine ni chachandu.

    ReplyDelete
  17. shanga ni urembo kwa mwanamke kama ulivyo urembo mwingine wa uvaaji bangiri na hereni, ila shanga kila sehemu utakayovaa kuwa na maana yake

    ReplyDelete
  18. kweli asiyenazo hafaidi uwanjani...
    mwanaume akijua kuzitumia kwa mkewe mke hatokubali mwingine wa nje. baadae nitafafanua ngoja nimalize kazi....

    ReplyDelete
  19. kweli asiyenazo hafaidi uwanjani...
    mwanaume akijua kuzitumia kwa mkewe mke hatokubali mwingine wa nje. baadae nitafafanua ngoja nimalize kazi....

    ReplyDelete
  20. kweli asiyenazo hafaidi uwanjani...
    mwanaume akijua kuzitumia kwa mkewe mke hatokubali mwingine wa nje. baadae nitafafanua ngoja nimalize kazi....

    ReplyDelete
  21. kweli asiyenazo hafaidi uwanjani...
    mwanaume akijua kuzitumia kwa mkewe mke hatokubali mwingine wa nje. baadae nitafafanua ngoja nimalize kazi....

    ReplyDelete
  22. I visited several web pages however the audio quality
    for audio songs existing at this website is truly fabulous.

    ReplyDelete