Friday, March 23, 2012

LEO NI KUMBUKUMBU YA NDUGU YETU ASIFIWE NGONYANI!!!

Asifiwe alizaliwa 26/11/1989 na alitutoka 23/3/2011

Ni mwaka mmoja sasa tangu mpendwa wetu Asifiwe atutoke.Umetuacha na majonzi na maumivu moyoni mwetu.

Tunakukumbuka sana uwepo wako. Tukiamini Mungu angekuacha japo kwa miAka michache. Midomo yetu haiwezi kuelezea jinsi tulivyokupenda.

Lakini Mwenyezi Mungu anajua ni jinsi gani tulikupenda/tunakupenda. Na jinsi gani tunakukumbuka. Mapenzi yako kwetu pia wema wako ni baraka kubwa kwetu.

Unakumbukwa sana na sisi wanafamilia wote pamoja na ndugu wote na pia marafiki. Kimwili hauko nasi, bali kiroho uko nasi daima. MWENYEZI MUNGU AIPUMZISHE ROHO YAKO MAHALA PEMA PEPONI!! AMINA!!!

14 comments:

  1. Nikweli Dada Yasinta kimwili hatunae ila kiroho tupo pamoja mungu ata mbariki
    Che Jiah

    ReplyDelete
  2. Kimwili katutoka, lakini kiroho tutaendeela kuwa naye, na kumuombea mahala pema peponi

    ReplyDelete
  3. mungu ashukuriwe.kaka s.

    ReplyDelete
  4. kwakweli miili, akili, mioyo na hata nafsi zetu haziwezi kuelezea ni namna gani Tulivyo mmisi ASIFIWE GALVAS DADI NGONYANI.japokuwa tu tumekuwa tukijifariji kwa kusema mungu akulaze mahali pema peponi mpendwa wetu lakini nafsi zimekuwa zikijisemea kwamba, pengo lako ASIFIWE kamwe haliwezi zibika kwani ni jambo lisilofikiriwa na YEYOTE katika sisi kwamba atakuja kupatikana mtu wa dizaini yako.
    kiukweli hatuna namna mapenzi yetu yalishindana na yule alokupenda zaidi na huyo ndiye alotuumba sote kisha akajipa mamlaka juu yetu na ndo mana kaamua kukuchukua ukaishi nae milele. sisi tunazidi kukuombea na tupo nyuma tunafuatia mana ni njia ya kila mmoja wetu.

    REST IN PEACE OUR BELOVED ASIFIWE DADI.......

    ReplyDelete
  5. kwakweli miili, akili, mioyo na hata nafsi zetu haziwezi kuelezea ni namna gani Tulivyo mmisi ASIFIWE GALVAS DADI NGONYANI.japokuwa tu tumekuwa tukijifariji kwa kusema mungu akulaze mahali pema peponi mpendwa wetu lakini nafsi zimekuwa zikijisemea kwamba, pengo lako ASIFIWE kamwe haliwezi zibika kwani ni jambo lisilofikiriwa na YEYOTE katika sisi kwamba atakuja kupatikana mtu wa dizaini yako.
    kiukweli hatuna namna mapenzi yetu yalishindana na yule alokupenda zaidi na huyo ndiye alotuumba sote kisha akajipa mamlaka juu yetu na ndo mana kaamua kukuchukua ukaishi nae milele. sisi tunazidi kukuombea na tupo nyuma tunafuatia mana ni njia ya kila mmoja wetu.

    REST IN PEACE OUR BELOVED ASIFIWE DADI....... ni hbib mshana(shem)

    ReplyDelete
  6. Pumzika kwa amani mdogo wetu,yote ni mapenzi ya mungu,sote njia yetu ni moja.

    ReplyDelete
  7. MPENDWA WETU ANAPOKUFA
    4 Je, umewahi kufiwa? Huenda ukalemewa na uchungu, huzuni, na kuhisi kwamba huna la kufanya. Nyakati kama hizo tunahitaji kutafuta faraja katika Neno la Mungu. (2 Wakorintho 1:3, 4) Biblia hutusaidia kuelewa jinsi Yehova na Yesu wanavyohisi kuhusu kifo. Yesu aliyekuwa na hisia kama za Baba yake, alielewa uchungu wa kufiwa. (Yohana 14:9) Yesu alipokuwa Yerusalemu, alikuwa akimtembelea Lazaro na dada zake, Maria na Martha, ambao waliishi katika mji wa Bethania uliokuwa karibu. Wakawa marafiki wakubwa. Biblia inasema: “Yesu alimpenda Martha na dada yake na Lazaro.” (Yohana 11:5) Hata hivyo, kama tulivyojifunza katika sura iliyotangulia, Lazaro alikufa.

    5 Yesu alihisije rafiki yake alipokufa? Masimulizi hayo yanaonyesha kwamba Yesu aliungana na familia na rafiki za Lazaro walipokuwa wakimwombolezea. Yesu alipowaona, alilemewa na hisia. “Akaugua rohoni na kutaabika.” Kisha masimulizi hayo yanaendelea kusema kwamba ‘Yesu alitokwa na machozi.’ (Yohana 11:33, 35) Je, huzuni ya Yesu ilimaanisha kwamba hakuwa na tumaini? Hapana. Yesu alijua kwamba jambo la kupendeza lilikuwa karibu kutukia. (Yohana 11:3, 4) Hata hivyo, alihisi uchungu na huzuni ambayo hutokana na kifo.

    6 Kwa njia fulani, huzuni ya Yesu inatutia moyo. Inatufundisha kwamba Yesu na Baba yake Yehova, wanachukia kifo. Lakini Yehova Mungu anaweza kumpiga na kumshinda adui huyo! Na tuone kile ambacho Mungu alimwezesha Yesu kufanya.

    ReplyDelete
  8. Pole sana familia ya Ngonyani,Pumziko la milele umpe ee Bwana!!!

    ReplyDelete
  9. Mungu atukamilishe ili tukutane nay tena Paradiso

    ReplyDelete