Leo nimetamani kweli mlo huu ningependa kweli kula mchana wa leo Ugali wa muhogo na samaki. Yaani nimerudi nyuma enzi zileee Lundo/Nyasa kila siku ugali na samaki. Katika picha hii ni samaki aina ya Tilapia "TILAPIA FISH CURRY" picha toka blog ya kaka Isaack yaani nimeiona picha hii tangu juzi nimemezea mate weeeeeeee nimechoka nikafikiri naota ndoto.
Mmmh, na mcha ndio huo ukakaribia, sijui tutaupatawa pi huo ugali, shukurani dada Yasinta
ReplyDeleteASANTE KWA HUO UGALI NI KWELI LEO TULE CHAKULA HIKI NA FAMILIA ZETU KWA PAMOJA ILA UMENITIA CHACHU KWA HUYU SAMAKI NITAMWAGIZA SASA HIVI JAMAA YANGU NDUNGURU YUPO KULE NYASA ANILETEE MBELELE WANGU NILE BASI NIKIKOSA NITAENDA PALE POST YA ZAMANI NIKANUNUE JAPO WALE DAGAA WA NYASA NAO KWA UGALI WANAFAA
ReplyDeleteMCHANA MWEMA DADA WE MCHOKOZI MATE YA MATAMANIO YAMETUJAA
CHE JIAH
Na sie watu wa visiwani hapo umetukoga nyoyo, japo umetuacha tumeshiba mate tu!
ReplyDeleteDuuhh njaa dada yanguuu,mmmhh ngoja nikimbie hapa!!!!!
ReplyDeleteUgali na samaki ni mlo wenye ladha maridhawa.
ReplyDeleteem3! nadhani uliupata huu mlo!
ReplyDeleteKaka Issack Che Jiah...wewe sasa mchokozi mbelele du umenitamanisha ile mbaya maana ni miaka miiiingi sana nimekula ila mbufu nilikua mwaka 200 Mbamba bay...
Kaka Chib! Pole kwa kushiba mate tu:-)
Rachel! Utakimbia utaweza ndugu wangu:-)
Kaka Ray ! Yaani katika mlo ninaoupenda ndio huo halafu kuwa na mboga majani kidogo pembeni ...aahh basi tu naache