Monday, February 13, 2012

Majambazi wawili wachomwa moto wakiwa hai mkoani Ruvuma Songea/Ruhuwiko


Baada ya kusoma makala hii nimepatwa na mshtuko pia woga na halafu maswali mengi sana. Binadamu wanaamua kufanya hivi kwa binadamu wenzao kuchukua sheria wenyewe je? nani hapa ni muuaji? Haya hebu soma mwenyewe...
........................................................................................................................................................................
Pichani ni miili ya watu wawili wanaodaiwa kuwa majambazi ambao walipigwa na kuchomwa moto hadi kifo katika eneo la Ruhuwiko manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.Baadhi ya wakazi wa eneo la Ruhuwiko ambao hawakutaka kutaja majina yao walidai kuwa kabla ya tukio hilo watu hao hawakuweza kufahamika majina yao waliwasili eneo hilo majira ya saa tatu asubuhi wakiwa na lengo la kuuwa na kuondoa viungo vya uzazi vya binadamu ambavyo inadaiwa vinauzwa kwa fedha nyingi.Wananchi hao walidai kuwa watu hao walifika kwa mama mmoja ambao walidai wanamtafuta hatimaye wakiwa wanakunywa katika klabu moja ya pombe za kienyeji inadaiwa wakazi wa eneo hilo waliwatilia mashaka watu hao na kuaanza kuwahoji ambapo inadaiwa baada ya kupata kipigo na kuanza kuchomwa walieleza kwamba wao ni wauaji na walipewa fedha kwa ajili ya kuuwa na kwamba tayari wamekuwa wamefanya matukio kadhaa ya mauaji .Chanzo cha habari kimebainisha kuwa wauaji hao walidai kuwa wapo 50 na wanatakiwa kuuwa watu zaidi ya 100 wakiwemo wanaume 60 na wanawake 40 kwa kuwaondoa sehemu zao za siri ambazo inadaiwa ni biashara ambayo inawapatia fedha nyingi . Baada ya wauaji hao ambao walikutwa na shilingi 500,000 kukiri kuwa kazi yao ni kuuwa ndipo wananchi wengi wenye hasira waliamua kuanza kuwapa kipigo kizito kisha kununua petroli na kuanza kuwachoma wakiwa hai .Hadi polisi wanafika katika eneo hilo miili ya watu hao ilikuwa inaendelea kuungua kwa moto.Uchunguzi umebaini kuwa wakazi wa Ruhuwiko waliamua kuchukua sheria mkononi baada ya matukio ya uharifu na mauaji kujitokeza katika eneo hilo na kwamba hii ni mara ya pili kwa wakazi wa Ruhuwiko kufanya mauaji ya kutisha ambapo miaka 25 iliyopita watu wengine wawili waliodaiwa kuwa ni majambazi sugu waliuwa na kisha miili yao kuchomwa moto."Mimi binfasi nimefurahia sana kitendo hiki labda sasa majambazi yataogopa kuendelea kufanya uharifu katika eneo hili,hivi sasa hatuna amani kabisa wizi imekuwa ni jambo la karibu kila siku ,mauaji nayo yanazidi kuendelea ,waharifu wengine wanakamatwa na kuachiwa acha wananchi wajichukulie sheria mkononi'',alisema mama mmoja ambaye hakutaka jina lake kuandikwa.Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na polisi bado wanaendelea na uchunguzi.
Habari hii nimeipata hapa.

9 comments:

  1. Dah Jeshi la polisi,usalama wa taifa,watu wa uhamiaji,wapelelezi kwa kweli inabidi wajipange upya....lakini serikiali pia inabidi isaidie taasisi hizi kwa kuwatengea bajeti inayoeleweka na kuwasimamia kwasaabu kama taasisi hizi zingeweza kulihakikishia taifa letu usalama....mambo kama haya yasingekuwa yanatokea.Vinginevyo we should be ready for the worst.

    ReplyDelete
  2. Duuhh, hii inatisha,nilifikiri mambo haya yanafanyika Dar tuu kumbe Nchi nzima AAAAhh Bongo Tambalale!

    ReplyDelete
  3. Hizi ndizo athari za mshuko wa maadili kwa jamii yetu.

    ReplyDelete
  4. Kwanza dada habari za magono,wandu makoko,wakazi wa Ruhuwiko wamechoka na watu wa aina hiyo maana muuaji lazima auawe wala uaingoje serikali,maana serikali kuua hajali sana kwani mtu akiua leo kesho kutwa utamkuta anajigamba kuwa mtu akileata taabu nitammaliza na sifanywi chochote.
    Dada mkoa wa Ruvuma sasa umeingiwa na shetani mbaya wa mauaji,ushirikina na unafiki,jana tulikuwa na mkutano na Mkuu wa mkoa huu anasema mkoa unamatukio mengi ya mauaji na ushirikina mfano wilaya ya Mbinga na Mbamba - Bay.wala wauaji hao usiwaonee huruma wacha wachomwe hata na makaa ya mawe ili kisibakie kiungo chao kikaja kuleta balaa.

    ReplyDelete
  5. Sheria za jino kwa meno hizi. Sheria za nchi zikishindwa kufuatwa na seriakali, basi walioiweka serikali hutoa maamuzi yao

    ReplyDelete
  6. mmmhhh!hii inatisha,jamani majambazi wanaudhi,kama umewahi kuingiliwa na majambazi utawezaona ni sawa wache wauawe ila jamani mi naona bora sheria ingechukuliwa kuliko watu kujichukulia sheria mkononi.ila kwa kweli ni suala gumu sana hasa huko kwetu sheria haifuatwi,watu wanakamatwa then wanaachiwa huru inaudhi sana.watu wanakosa imani na serikali yenyewe.
    Mlongo wa US.

    ReplyDelete
  7. DU kwakweli ni hatari tunakoelekea hii ni kwavile ni ukosefu wa ajira au ugumu wa maisha ukweli hatufiki mbali kwa mtindo huu
    CHe Jiah

    ReplyDelete
  8. Nachukua nafasi hii kwa kuwashukuruni wote kwa mchongo wenu. Yote yaliyosemwa ni kweli ila nataka niwe tofauti kidogo ni kwamba hata kama unamchukia mtu sio ndiyo umuue. Je? kwa mfano hapa najiuliza ni nani sasa hapa ni muuaji? Ndiyo watu wanachoka na tabia hiyo lakini ilibidi wapeleke habari kwenye vyombo vya habari...

    ReplyDelete