Saturday, January 7, 2012

NIMEULIZWA SWALI HILI NA BINTI YANGU....

Ilikuwa mwaka jana siku ya Noeli ...Binti yangu Camilla akaniuliza:- Mama, hivi kwa nini Yesu alizaliwa tarehe 25/12..Lakini, kipindi cha Pasaka huwa tuna sema kuwa Yesu anakufa, kwa nini ile tarehe ya kufa huwa haiwi ileile kila mara? Je kuna Yesu wangapi?...Mmmhhh!! hapa nikawa natafakari na sijapata jibu na leo nimeona niombe msaada hapa kibarazani kwani palipo na wengi huwa hakiharibiki kitu....

7 comments:

  1. Swali gumu hilo Da' Yasinta.
    Heri ya Mwaka Mpya pia, kwako na wengine wote.
    Maggid,
    Iringa.

    ReplyDelete
  2. hata mimi huwa inanikwaza kwasababu mtu akifa mfano tarehe 13/5/mwaka wowote si inabidi iwe tarehe hiyohiyo kila mwaka na mwezi huohuo??!!!sasa kufa kwa yesu mara tarehe 20/3 mwaka mwingine inakuwa tarehe 24/4 hapo inakuwaje?

    ReplyDelete
  3. Kaka Mjengwa/mwenyekiti! Ndiy ni swali gumu tena sana na ndi maana nikana niwaulize na wenzanu..Watoto ni walimu wakuu...Heri ya mwaka mpya nawe pia familia yako.

    Usiye na jina! labda tusubiri twaweza kupata jibu ...

    ReplyDelete
  4. Sipati picha huko shuleni waalimu wake wanavyokoma na maswali...

    ...Mwambie tunalifanyia kazi.

    ReplyDelete
  5. Du. huyu ni kapulya mwingine kweli nyoka huzaa nyoka.

    Nampa hongera na nakuomba uendeleze hicho kipaji chake cha udadisi wa masuala yenye kufikirisha kama hilo

    jaribu kuwasilana na wataalamu wa masuala ya dini

    Kila la kheri

    ReplyDelete
  6. hasa pasaka ilikuwepo kabla hata yesu hajazaliwa na ilikuwa ni wakati wakipindi chakutoka baridikari huko ulaya kwenda kwenye kipindi cha joto.hivyo basi kwasababu enzi hizo zamani bado teknologia ilikuwa bado yaani watu kutengeneza vitu kama hitasasa watu wakawa wanakufa sana kutokana na hiyo baridi sasa wale waliopona ndio wakawa wanaulizana kwa kiingereza hivyo basi ilipokuja dini wakaunganisha humo kuwa ndio ukombozi lakini asili ya pasaka ni kutoka hicho kipindi cha baridi kari kuja kwenye joto huko ulaya tuko pamoja?

    ReplyDelete
  7. naona maneno yameruka WAKAWA WANULIZANA KWA KIINGLISHI HAVE YOU PASS OVER FROM THE BARIDI KALI

    ReplyDelete