Saturday, January 21, 2012

MWANAMKE NA NYUSO ZAKE!!!

NIMEIPENDA NUKUU HII EBU SOMA!! "Mwanamke kama dutu la udongo wa mfinyanzi huubwa na kuumbuliwa na jamii kwa namna mbalimbali. Kama kinyonga, uso wake unabeba rangi tofauti kulingana na mikondo ya maisha na mapigo ya wakati. Itakuwaje mwanamke awe wa wa kuuzwa kama mwenye ugaga wa hisia za kujichagulia mwenyewe; au awe wa kuuzwa kama pakacha la maemba katika soko la umma? Uso wa mwanamke ni njia mbilimbili; ikiwa hazai analea, isipokuwa akirembesha anarembeshwa, kama hatumbuizi anatumbuizwa, ikiwa hajengi anabomoa; na kila mtu anamtazama na kumtarajia aonyehe uongofu wa malaika kama kwamba yeye si mtu. Haya yanapokolea ndipo mwanamke anaonyesha nyuso zake." kutoka kwenye kitabu kiitwacho NYUSO ZA MWANAMKE.

3 comments:

  1. Nafikiri mwandishi huyu,yuko sahihi kwa fasihi aliyo itumia kumuumba mwanamke anavyo muona yeye. kuhusu neno mwanamke na nyuso zake,kwangu mimi naweza kukubaliana na mwandishi katika upande mmoja nao ni pale mwana mke anapojikuta anaamuliwa kufanya kitu kwa jamii bila yeye kuafiki,kujuwa ,kuaamua na kumfikisha mahalia ambapo tafsiri yake kwa jamii yaweza kuwa kwaza wengi.mfano ukianglia matangazo,yanyo fanywa nawanawake,mengi huwaacha wakionekana na vichupi,naikiaminika kama ndo uzuri.pia kwenye kumbi za burudani,nimwanamke anaye vaa nguo nusu uchi jukwaani nakila mtu aneenda kutizama humwaga sifa kwa mwanamke huyo.hivyo nikweli mwanamke nikinyago ambacho jamii inaweza kukifinyanka ama kukichonga itakavyo. kaka s

    ReplyDelete
  2. Wanawake ni mama zetu,wanawake ndiyo wake zetu na wanawake ni dada zetu.Kwa ujumla wanawake ni sehemu muhimu sana katika harakati za maisha na mafanikio ndani ya familia.Salamu kwa wanawake wote popote pale walipo.

    ReplyDelete