Thursday, January 12, 2012

MAJI YA KWENYE MTUNGI NI MATAMU JAMANI!

Maji ya mtu ni matamu sana hasa kama unatumia kata au kikombe cha bati kama uonavyo hapo kwenye picha. Mtungi huu una historia yake:- Ni Hivi mwaka jana nilipokuwa Matema beach, pale kuna soko kubwa la vyombo vya aina mbalimbali vya udongo wa mfinyanzi. Nami nikaona ngoja niende nikasafishe macho. Kwa bahati nzuri nikaona mtungi huu nikaununua. Nakuambieni penye nia pana njia. Niliupakata mtungi huu kuanzia Matema Beach mpaka Songea/Ruhuwiko. Halafu kabla hatujafika nyumbani Ruhuwiko tukasimamishwa na Polisi pale Bombambili kwa wale wanaojua umbali wa kutoka Bombambili mpaka Songea mjini /Ruhuwiko. Tukamsalimu, mnajua alitaka nini, baada ya kuangalia ndani ya gari? MTUNGI HUU! Duh! hapo nikasema simpi ngó, naye akasema nitawatoza kwa spidi ila mkinipa mtungi nitawaacha nami nikamjibu, sawa tu..kwa vile nilijua hatukuwa katika mwendo wa spidi. Akashindwa na tukaendelea na safari. Hii ni historia fupi ya MTUNGI HUU.
Hapo juu nimesema maji ya mtungi ni matamu kwa kunywa kwa kutumia KATA. Kwa wale wasiojua kata ni nini . Katika picha hii hapa mnamwona Stella Manyanya akijaribu kunywa maji kwa kutumia KATA. Hivi ndivyo ilivyokuwa hapo zamani ni utamaduni wetu.

2 comments:

  1. stela manyanya anakunywa "kitu ingine" sio maji. au?

    ReplyDelete
  2. Duhh da'Yasinta tena uwayananukia udongo hayo maji,duuhh tena kimbe hicho kwa familia nzima mnapokezana hehehhhe Siri ya Mtungi aijua KATA....Ubarikiwe da'Yasinta na woooteeee!!

    ReplyDelete