Tulipokuwa nyumbani mwezi wa sita mwishoni mpaka wa nane mwanzoni bahati nzuri ulikuwa ni msimu wa kuvuna. Tulimkuta Mzee ngonyani/babu amevuna mahindi. Na hapa mnamwona kijana Erik akimsaidia babu kupiga mahindi, kwa babu Songea Ruhuwiko.
Baada ya kazi nzito ya kupiga mahindi nguo zilikuwa zimechafuka kwa hiyo ni lazima kufua na hapa mnamwona anafua nguo zake....hapa ni Songea Ruhuwiko ....
Dada mtu naye siku yake ya dobi ikaja kama mnavyoona naye anafua nguo zake. Hii /hizi kazi ni moja ya kujifunza kuishi kwa kujitegemea.Uzuri wake maji tulikuwa nayo humu humu uani.
MAISHA NI KUJIFUNZA.
hongera sana kwa malezi mazuri unayowapa watoto ..kweli mtoto umleavyo ndivyo akuavyo...
ReplyDeletetutafika tu
hongera sana dada yasinta kwa malezi yako mazuri maana kuna watu wengine wakishakuwa ulaya basi ni mambo ya uzungu tu mambo ya kumfundisha mtoto jinsi ya kujitegemea inakuwantabu tupu waswahili husema mzarau kwao ni mtumwa kweli dada ninavyokuonaga wewe pamoja na kukaa kwako nje ya nchi lakini hujasahau mila na desturi za nyumbani tz hiyo ni safi sana maana kuna wengi wakikaa nje kidogo tu full majivuno na uzungu mwiiingi hata watoto wao hawataki wazungumze kiswahili huo ni ulimbukeni wa kutupwa big up dada yasinta nakupenda sana maana uanaonekana una utu na busara sana uabarikiwe sana na familia yako
ReplyDeleteSafi sanaaa...nimependa sana hii, na hongera sana Dada Yasinta kwa kuwa na vijana wachapa kazi.
ReplyDeleteHongera sana da'Yasinta yaani nakukubali mnoooooo duuhh wewe ni mama haswa na Mungu azidi kuwabariki wewe na familia yako, pia wote wataopita hapa.Mimi penda sana wewe!
ReplyDelete"Mama lea mtoto!"
ReplyDeleteMmmH Watoto wa shoka! Hapa halaumiwi mzazi.
ReplyDeleteHongera Yasinta.
samahani nilisahau kitu,
ReplyDeleteHawa watoto kama wanaweza kazi hivi, basi nina hakika kabisa hutapata shida mdogo wao akija.
Abarikiwe atakayepitia hapa.
Edo! wengi wanasema kulea mimba si kazi ila kulea ndo kazi ni kweli naamini. Na ahsante kwa kuona kuwa nawafunza wajombao maisha haya niliyopitia mimi.Ni kweli tutafika tu.
ReplyDeleteUsiye na jina mimi siona sababu ya kusahau kwangu au kujifanya kuwa nimesahau. Ahsante sana kwa kulisema hilo ni kweli wapo tena wengi tu.
Kaka Baraka! Nafurahi kama umependa hii na Ahsante kwa kunipa hongera ni kwamba najitahidi ili wajue tamadani zote huwezi kujua...
Rachel! Najitahidi kuwaonyesha tamaduni zangu ili wasipate shida waendapo . Nawe unapendwa pia na wewe kwa vile umepita hapa basi tayari umebarikiwa.
Kaka mkubwa Phiri! najitahidi kuwalea kadiri nilivyolelewa mimi mwenyewe pia.
Mija! ni kweli mtoto wa shoka ni shoka au mtoto wa nyoka ni nyoka. Ahsante ndugu wangu...hahahaaaaa
haaaaaa mwe nimecheka kwelikweli mbaka mbavu hazina hali ETI UNA UHAKIKA KABISA MDOGO WAO AKIJA HATAPATA SHIDA HA HA HAAAA. nawe pia kwa vile umepita hapa basi nawe umebarikiwa . HAYA MBARIKIWE WOTE MLIOPITA HAPA NA wataopita hapa na pia amani na upendo viwe nanyi.
Hongera, nimeipenda hii, watoto lazima wazoee kazi, vinginevyo watapata shida wakiwa wakubwa
ReplyDeletehata kuosha sahani itakuwa kazi.
Umekuwa mzalendo wa maisha ya ulikotoka.Hiyo safi mnoooooooooo!! wengi wanawafunza ya huko walikolowea tu na kudharau walikotoka.Pongezi sana.Mimi nina watoto wangu hapa USA,huwa siwaruhusu kufua nguo zao kwenye mashine, nawachagulia ni nguo gani waoshe kwa mashine na nguo gani waoshe kwa mikono kama wanavyofanya wanao hapo.
ReplyDeleteDada P. Ahsante sana Si unajua tupo safarini sisi binadamu.
ReplyDeleteUsiye na jina! Hongera na wewe kwani hawa watoto hawataishi na sisi milele watahitaji kuishi peke yao. Kwa hiyo inabidi kuwafunza kama sisi tulivyofunzwa. Hata kupika vyakula inabidi kuwafundisha. Mbarikiwe sana wote mnaopita hapa.