Saturday, December 24, 2011

HAPA SWEDEN LEO NDIO CHRITMAS..NAS TWASEMA HERI YA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA ..GOD JUL OCH GOTT NYTT ÅR!!!!

Picha hii ilikuwa mwaka jana siku kama ya leo angalia kulivyokuwa kweupe na hapo ndipo chrstmas inakuwa kweli christmas........Nimejaribu kuuliza kwanini wanasheherekea Christmas leo na sio kesho kama wengi wanavyofanya sijapata jibu la kuniridhisha kwa kweli kwa hiyo ukienda sehemu na ukikuta wanatembea uchi nawe tembea.


Kuamka leo asubuhi sehemu ileile kama picha ya hapo juu. Lakini leo mpaka nyasi zinaonekama hakuna theruji, Jua linawaka...ila kuna kaubaridi kwa mbali...Na hii inasemekana haijawahi kutokea.....KHERI KWA CHRISTMAS/GOD JUL TILL ALLA. Oh naondoka kwenda kubeba mabox mwenzenu...Tutaonana baadae au kesho au keshokutwa au niseme tu TUTAONANA TENA.

6 comments:

  1. Inamaana hawa Waswidi hawakawii hata kidogo kwa vitu vitamu na wanaona kusubiri masaa 24 zaidi ya chelewesha!!!!?

    Basi ndio maana wametuchukulia mke mzuri haraka hivyo!!!



    Nataka kusema: Hongereni kwa siku ya Xmas, Da'Yasinta na familia yako kote-kote ilipo Ulaya na Afrika.


    Mwaka mpya 2012 ukupe nguvu na maarifa mepya ya kuendeleza mafanikio yako kama mzazi kwa watoto wako; kama mke kwa mumeo; na kama malikia wa kimawazo kwetu sisi tuliezowea kusoma blogu yako.


    Kwa upande wa wasomaji wa blogu yako WOTE naomba nao kuwatakia memba kwa wakati huu.

    "Punguzeni pombe, lakini; na kama umepata mbili ya baridi na ya moto, BASI KAA HUKOHUKO NYUMBANI USITANGATANGE NA JIJI LOTE NA ULEVI HATUTAKI MSIBA WAKO SIE KWA WAKATI HUU!!!"

    ReplyDelete
  2. Ha ha haa kaka Manyanya una maneno??

    Kila la heri jamani wote huko.

    ReplyDelete
  3. Nimewasemehe Waswidi, lakinini sijawasahau!

    ReplyDelete
  4. Kaka Phiri..Unajua hizi mila na desturi kwa kweli kila sehemu wana zao..Nazidi pia kushangaa na jibu sipati kwani wao hapa pasaka wanasharekea siku moja kabla..Ntafikisha ujumbe kwao. Ahsante kwa yote..nimeshindwa kuacha nukuu hii:- "Basi ndio maana wametuchukulia mke mzuri haraka hivyo!!!" ww mkali kweli:-)

    Mija yaani kaka huyu ana maneno haswa umeona hiyo nukuu hapo juu...Kila la kheri nawe pia..

    Kaka Phiri..Ntafikisha salamu..kweli usiwasahau:-)

    ReplyDelete
  5. nakweli wamemchukua mwanamke mzuri tena sana.huyo mswid anajua kuchagua

    ReplyDelete