Kabla ya kulalamika kuhusu ladha ya chakula, fikiria mtu ambaye hana kitu cha kula. Kabla ya kulalamika kuhusu mume wako au mke wako, fikiria mtu amnbaye amliliaye Mungu kwa ajili ampe rafiki. Leo kabla ya kulalamika kuhusu maisha. Fikiria mtu ambaye alikwenda mbinguni mapema mnoamekufa mapema mno. Kabla ya kunung'unika kuhusu umbali gani unaendfesha garilako, fikiria mtu ambaye anatembea umbali huo kwa miguu yake. Na wakati wewe ni uchovu na ulalamikapo kuhusu kazi yako, fikiria wale wasio na ajira, walemavu, na wale ambao wanataka wangekuwa na kazi kama yako yako. Na wakati mawazo yanakutawala na kukufanya uwe na huzuni, tabasamu na ufikiri. Wewe ni hai na bado upo.
TUWE NA UHAKIKA NA TUFIKIRI/TUWAZE KWA UHAKIKA!!!!
TUWE NA UHAKIKA NA TUFIKIRI/TUWAZE KWA UHAKIKA!!!!
Nikweli nami niwe mtu wakwnza kuchangia kweli maisha ni zawadi usije ukaona mtu yule anaishi vile nawe ukaiga kuishi kama mwenzio au tuseme nduguyo ukamwona mr sam analala pazuri au anakunywa kila siku nawe ukageza huyo kapewa zawadi na hana mpinzani, ili uishi vizuri ishi kama upendavyo si kama wapendavyo hapo maisha yatakuendea vizuri na hutayumba kwani kila mtu kapewa riziki kwa namna yake si kwa namna ya mtu mwingine kipaji ni kile alichokupangia mwenye enzi si ulazimishe ,fanya mipango yako kutokana na wigo wa uwezo wako usiige kwa mtu jitahidi kukubali matokeo fanya busara kuwa mtulivu katikamipango yako ya maisha kweli
ReplyDeleteNDUGU YANGU MAISHA NI ZAWADINA MAISHA NI MAISHA KUBALI MATOKEO ILA WEKA JUHUDI KATIKA KUTAFUTA MAISHA USIKATE TAMAA
CHe Jiah
["...na kabla ya kunung'unika eti umekosa vyatu, wafikirie wasiekuwa na miguu."]
ReplyDeleteKatika ujumbe wa leo,nimeukubali kiaina. najaribu kuichambua zawadi,jinsi inavyo patikana,au mchakato wake mzima unao kuja kuitwa baadae zawadi.maisha nizawadi kutoka kwa nani,mungu,au wazazi,au dakitari aliye kuwa mstari wa mbele kumsaidia mama mjamzito kujifungua salama,na hatimaye kumpata mtoto ambaye nimimi nawewe.maisha ninini,ni pumzi au kuwa na elimu,kazi nzuri,ndo maisha.maisha nikuishi kama ndivyo nani mwenye mamlaka ya kuishi kwetu hapa duniani.wengine husema maisha nisafari ndefu? na labda wengi watakumbuka katika msemo huohuo wa maisha nisafari ndefu,ambayo mwisho wake nikifo! ,je tuna uhakika na hilo.mtoa ujumbe umeniwazisha sana,maisha nizawadi,hivyo waweza kuiomba kama mtu akikuuliza ? au kwasababu mtoa zawadi hiyo ni mungu? basi hatuna muda wakusema mimi nataka zawadi hi ? kumbe kuishi ni zawadi ukiichezea waweza kunyang'anywa? nanani? asante da Yasinta kwa ujumbe, nikipata muda nitarudi tena,ngoja nisikilize wengine wana semaje. kaka s
ReplyDeleteAsante kwa ujumbe murua da Yasinta.
ReplyDeleteUmenena da'Yasinta yaani umekugusa nyanja nyingi sana,ASANTE MUNGU KWA YOTE!!
ReplyDeleteAsante kwa neno la leo mama Camilla..
ReplyDeleteUjumbe kibonge huu! Asante kwa hii!
ReplyDeletennnnnnnnnnnnnnnnnn
ReplyDeleteMsemo:Maisha ni mchezo na dunia ni jukwaa na kila mtu anacheza anavyoweza.
ReplyDelete-------------------------------------
"WEWE UKIOMBA VIATU MWENZIO ANAOMBA MIGUU"
-------------------------------------
NINI HASA KUSUDI LA MAISHA?
---------------------------------
@Mkuu Njau:Si nasikia kusudi la maisha lingejulikana kwa uhakika kama sie BINADAMU tungeomba kuzaliwa?
ReplyDeleteKwa hiyo labda kusudi la MAISHA ni jinsi tu mtu ajitafsiriavyo kwanini yuko hai. Na kuna watakao msingizia MUNGU na watakao singizia tuko MAISHANI ili tuzae... mpaka watakaodai kusudi la kuwa MAISHANI ni KULA!
AU?
Ni kweli maisha ni zawadi na ni tunu ambayo tunatakiwa kuitumia kwa kutenda mema ili kudumisha umuhimu wa tunu tuliyopewa na mwenyezi mungu.
ReplyDeleteIli kuienzi vyema tunu hiyo tunatakiwa kupunguza choyo ya kujipenda kupindukia bali tuongeze upendo kwa wengine
Kila la kheri.
tumezoea kulalamika sana bila kuwaza vizuri,ukiyafikira sana unaona maneno yalivyojaa ukweli,si kila wakati ni wakatai wa kulalamika na kusononeka.
ReplyDelete@Mtani wangu Kitururu;
ReplyDeleteMada bado inashika kasi na sasa nikuulize hivi:JE KUSUDI NI KUZALIWA,KUISHI NDANI YA CHANGAMOTO NA HITIMISHO LA KIFO?
@Mtani wangu MANGI Njau: Wala sina jibu aisee katika swali hilo lako Mkuu!
ReplyDeleteMtani swali gumu hilo!
Ila nikikaa mkao fulani naweza kusema BINADAMU aanzaye kudadisi sana mpaka maana ya MAISHA ,.....labda huyo ana MUDA zaidi mapaka ana muda mpaka wa kufikiria.
Kwa kuwa katika kibado kikumbukwacho ni KIBADO hata kama hicho ni kipengele tu kwenye maisha ya MTU.:-(
Swali:
Si wakati hakuna muda vifikiriwavyo zaidi ni vichukuavyo muda?
Kitururu:-Endelea kufikiria zaidi na huenda ukavuka hilo daraja.
ReplyDelete--------------------------------
Suala la muda na wakati kila mtu anajipangia mwenyewe na hapa hakuna fomula.
Nachukua nafasi hii na kuwashukuruni kwa ushirikiano wenu maana bila ninyi nadhani MAISHA NA MAFANIKIO ISINGEFIKIA HAPA ILIPO. MNAPENDWA WOTE.
ReplyDeleteobat telat bulan i think your blog very informative cytotec thanks for sharing obat cytotec
ReplyDelete