Wednesday, November 23, 2011

TUTAKUKUMBUKA DAIMA ASIFIWE NGONYANI!!!

Kwa vile leo ni JUMATANO NA NI JUMATANO YA KIPENGELE CHA MARUDIO YA mada/makala/matukio mbalimbali. Basi JUMATANO YA LEO imeangukia kuwa tarehe 23/11 ambayo si mara nyingi inakuwa hivi. nasema hivi kwasababu 23/3/2011 siku ya jumatano tuliondokewa na mpendwa wetu Asifiwe na leo imetimia miezi nane na imeangukia siku ya jumatano na tarehe 23/11-11 kusema kweli nimeshikwa na butwaa kidogo maana si mara nyingi inakuwa hivi. Kwa hiyo nimeona si vibaya kama tukimkumbuka Asifiwe wetu.

Hapa ndipo mahali alipopumzika Asifiwe katika safari yake ya mwisho. TUTAKUKUMBUKA DAIMA ASIFIWE.KWANI UPO NASI KIROHO ILA SI KIMWILI. PUMZIKA KWA AMANI MDOGO WANGU/WETU.

17 comments:

  1. Halafu leo nimelitafakali sana jina lake, Hivi ni kwa nini unadhani alipewa jina hili la Asifiwe...Lina maana kubwa sana..

    Pumzika kwa amani dada Asifiwe.

    ReplyDelete
  2. OOH Poleni sana ila kwa kuwa sisi wana blog hii ya Maishs tupo pamoja na familia hii kwa maombolezi hayo basi Mimi kwa niamba ya wana blog hii natoa pole sana kwa yote kuweni na amai na utulivu Dada Yasinta Pole kwani huu ndio ulikuwa muhimili wako sasa muhimil wako ni yesu, mtegemee mtukuze na mpende kama umpendavyo jirani wa blog na jirani unaeishi karibu nae kuwa makini katika siku hizi za UZUNI na kumbukumbu usijisikie upo pekee yako sisi wanablog hii tupo nyuma yako MTEGEMEE SANA MTETEZI WAKO
    MIMI KAKA YAKO
    CHE JIAH
    AMINA

    ReplyDelete
  3. Ayubu 14:1-22

    1 “Mwanadamu, aliyezaliwa na mwanamke,

    Ana maisha mafupi na yenye kujaa msukosuko.

    2 Amechanuka kama ua na kukatiliwa mbali,
    Naye hukimbia kama kivuli wala haendelei kuwako.

    3 Ndiyo, umefungua macho yako juu ya huyu,
    Nami unanitia katika hukumu pamoja na wewe.

    4 Ni nani anayeweza kutokeza mtu safi kutoka katika mtu asiye safi?
    Hakuna hata mmoja.

    5 Ikiwa siku zake zimeamuliwa,
    Hesabu ya miezi yake iko kwako;

    Umeweka amri kwa ajili yake ili asiweze kuvuka.

    6 Geuza macho yako kutoka kwake ili apumzike,
    Mpaka apate raha kama mfanyakazi wa kukodiwa anavyopata katika siku yake.

    7 Kwa maana hata kwa ajili ya mti kuna tumaini.
    Ukikatwa, utachipuka tena,

    Na tawi lake halitakoma.

    8 Mzizi wake ukizeeka katika udongo
    Na kisiki chake kikifa katika mavumbi,

    9 Utachipuka unaponusa harufu ya maji
    Nao utatokeza tawi kama mmea mpya.

    10 Lakini mwanamume hufa na kulala akiwa ameshindwa;
    Na mtu wa udongo hukata pumzi, naye yuko wapi?

    11 Maji hupotea kutoka baharini,
    Na mto hutiririka na kukauka.

    12 Mwanadamu pia hulala chini wala haamki.
    Hawataamka mpaka mbingu itakapokuwa haipo tena,

    Wala hawataamshwa katika usingizi wao.

    13 Laiti ungenificha katika Kaburi,

    14 Mtu akifa, je, anaweza kuishi tena?
    Mimi nitangojea siku zote za kazi yangu ya kulazimishwa,

    Mpaka kitulizo changu kije.

    15 Wewe utaita, na mimi mwenyewe nitakujibu.
    Kwa kuwa utaitamani sana kazi ya mikono yako.

    16 Kwa maana sasa unaendelea kuhesabu hatua zangu;
    Hutazami lolote isipokuwa dhambi yangu.

    17 Maasi yangu yamefungwa kwa muhuri katika mfuko,
    Nawe unatia gundi juu ya kosa langu.

    18 Hata hivyo, mlima, unaoanguka, utafifia,
    Na hata mwamba utaondolewa mahali pake.

    19 Maji kwa hakika yanakula hata mawe;
    Kumwagika kwake kunayachukua mavumbi ya dunia.

    Ndivyo ulivyoliharibu tumaini la mwanadamu anayeweza kufa.

    20 Unamshinda milele hivi kwamba yeye anaenda zake;
    Unauharibu uso wake hivi kwamba unamwacha aende zake.

    21 Wanawe hupewa heshima, lakini yeye hajui hilo;
    Nao wanakuwa wasio na maana, lakini yeye hawafikirii.

    22 Ila tu nyama yake iliyo juu yake ndiyo itakayoendelea kuuma,
    Na nafsi yake ikiwa ingali ndani yake ndiyo itakayoendelea kuomboleza.”

    ReplyDelete
  4. Pumzika kwa amani mdogo wetu asifiwe,sisi tulikupenda lakini mungu kakupenda zaidi.

    ReplyDelete
  5. We are with you in your sorrow sister. But in the spirit of the wangoni we also celebrate your sister's good deeds while mourning. Umkuluqango makabe nawe. May God be with you.

    ReplyDelete
  6. Pumziko la milele umpe ee Bwana!!!!!

    ReplyDelete
  7. so sad jamani.Mungu akuweke pema Asifiwe.

    ReplyDelete
  8. Pole sana mlongo tuko pamoja nawe katika wiki hii ya maombolezo. Mbarikiwe sana.

    ReplyDelete
  9. Ufunuo 21:1-8

    1 Nami nikaona mbingu mpya na dunia mpya; kwa maana mbingu ya kwanza na dunia ya kwanza zilikuwa zimepitilia mbali, na bahari haipo tena. 2 Nikaona pia lile jiji takatifu, Yerusalemu Jipya, likishuka kutoka mbinguni kwa Mungu na limetayarishwa kama bibi-arusi aliyepambwa kwa ajili ya mume wake. 3 Ndipo nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha ufalme ikisema: “Tazama! Hema la Mungu liko pamoja na wanadamu, naye atakaa pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Na Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao. 4 Naye atafuta kila chozi kutoka katika macho yao, na kifo hakitakuwapo tena, wala maombolezo wala kilio wala maumivu hayatakuwapo tena. Mambo ya zamani yamepitilia mbali.”

    5 Na Yule aliyeketi juu ya kiti cha ufalme akasema: “Tazama! Ninafanya vitu vyote kuwa vipya.” Pia, anasema: “Andika, kwa sababu maneno haya ni ya uaminifu na ya kweli.” 6 Naye akaniambia: “Yamekuwa! Mimi ndiye Alfa na Omega, mwanzo na mwisho. Kwa yeyote aliye na kiu mimi nitampa maji bure kutoka kwenye chemchemi ya maji ya uzima. 7 Yeyote anayeshinda atarithi vitu hivi, nami nitakuwa Mungu wake naye atakuwa mwanangu. 8 Lakini kwa habari ya waoga na wale wasio na imani na wale wenye kuchukiza katika uchafu wao na wauaji na waasherati na wale wanaozoea kuwasiliana na pepo na waabudu-sanamu na waongo wote, fungu lao litakuwa ndani ya lile ziwa linalowaka moto na kiberiti. Hili linamaanisha kifo cha pili.”

    ReplyDelete
  10. Kwa tuliowahi kumuona Asifiwe na kuongea nae ama kuwa karibu nae huwa tunapata wakati mgumu sana tunapokumbuka kuwa hatupo pamoja naye tena Duniani. Asifiwe alikuwa na kila sababu ya kuitwa jina hilo .. Ingawa sidhani kama ni jibu sahihi kwa swali la dada Mija Shija Sayi .. Asifiwe alikuwa ni msichana mwenye kustahili sifa. Utulivu wake, uzuri wake, hekima zake, nidhamu zake zilikuwa kigezo na uthibitisho kamilifu wa kustahili kuitwa jina Asifiwe.

    Sio dada Yasinta na familia ya Mzee Ngonyani pekee imepoteza mtu muhimu lakini pia watu wote waliowahi kumuona, marafiki zake na marafiki wa ndugu zake na Taifa kwa ujumla tumempoteza binti mwenye kustahili kusifiwa, binti ambaye maisha yake yalikuwa na yangekuwa kioo muhimu kwa wasichana na jamii kwa ujumla.

    Mungu Ailaze Roho ya Asifiwe mahali Pema.

    ReplyDelete
  11. Ahsanteni sana kwa kuwa nami katika siku hii ya jumatano 23/11. Ndiyo inauma kumpoteze tumpendaye lakini Mungu hafanyi kosa ni kwamba ana makusudi yake. Basi na tuzidi kumwombea ili nasi siku moja tufike alipo yeye. Pia kumbukumbu inaweza kuwa ya aina nyingi kuomba misa, au kuwasha mshumaa, au kusali peke yako lakini mimi nimeona niswashirikisha ndugu zangu.
    Karibu kuendelea kusema....

    ReplyDelete
  12. Kila lakheri huo uliko Asifiwe...tunazidi kukuombea upumzike kwa amani. Najua hata wewe unatumiss sana nakutuombea sana. Naamini ipo siku tutaonana....kwani kifo si mwisho wa yote, bali ni daraja katika kuyaendelea maisha ya uzima wa milele.

    ReplyDelete
  13. mwenyezi mungu ailaze roho yake mahali pema

    ReplyDelete
  14. Mungu ndiye atoae na kutwaa pia jina lake na libarikiwe....Amina
    dada Asifiwe na apumzike kwa amani daima,yeye ametangulia na sisi tunafuata....

    ReplyDelete