Baadhi ya wananchi wakiwa wameokoka katika eneo hilo.......................................
Wamachinga Mbali mbali wakikimbia katika eneo la tukio wakati wa machafuko hayo yamepamba moto
Polisi wakijaribu Kuzuia Ghasia katika eneo hilo na kufukuza Wamachinga.......
Watu Mbali Mbali wakiwa wanakimbia ili kujiokoa na Hatari katika eneo hilo ......
Watu Mbali Mbali wakiwa wanakimbia ili kujiokoa na Hatari katika eneo hilo ......
Picha zote na: http://www.latestnewstz.blogspot.com/. Nimetumiwa Picha na HABARI na:
LATEST NEWS T.
LATEST NEWS T.
Naona mwisho wa juma hili umeanza vibaya nimejiuliza au hii tarehe 11/11/-11 nini? LOL!!
Duuh kweli mwisho wa juma umeenza vibaya.Nakutakia mwisho mwema wa juma mdada.
ReplyDeleteTaswira ya mwandishi ni uwakilishi halisi wa maisha ya jumla ya jamii yetu.Machinga ni msamiati unaowakilisha sekta ya ujasiriamali usiorasimishwa nchini Tanzania.
ReplyDeleteSekta ilianza kuibuka kimyakimya kutokana na ukuzi wa uchumi usioenda sanjari na ongezeko la watu na ajira rasmi.
Lakini unapotazama nyuma ya pazia sekta hii ni matokeo ya mfumo wa elimu unaotaiyarisha jamii kwa ajili ya kupata ajira na siyo kujiajiri.
Mfumo huu hauzingatii umakini na umahiri katika maisha na mafanikio kupitia stadi za kazi-maisha na badala yake umesheheni nadharia inayowasilishwa kupitia lugha za kigeni na kuifanya jamii ikariri taaluma kwa ajili ya kuingia kwenye vyumba vya mitihani na kubeba vyeti lukuki bila stadi za maisha.
Kule Unguja wanasema:"TUMESOMA HATUKUJUA,TUMEJIFUNZA TUMEFAHAMU"
-----------------------------------
Nawatakieni nyote maisha na mafanikio yasiyo na mikikimikiki ndani ya wikiendi hii.
===================================