Saturday, November 26, 2011

LEO NI 26/11/2011 NDIYO SIKU ALIYOZALIWA ASIFIWE NGONYANI

Tarehe 26/11/1989 ilikuwa siku ya furaha kwa familia ya Ngonyani kupata binti mwingine ambaye ni Asifiwe. Ni hisia za ajabu sana mwaka huu bila kumpigia simu na kumtakia HERI kwa siku yake ya kuzaliwa ambayo ni leo. Na hii ni sababu kubwa nikaona wiki nzima iwe yake kwa vile imekuwa wiki ya matukio matatu kwa mpigo. Kweli Mwenyezi Mungu ndiye muweza ebu jaribu kuangalia Asifiwe alizaliwa 26/11/1989 siku ya jumapili ,na leo na jumamosi 26/11/2011 ange/ametimiza miaka 22 halafu sasa siku aliyozikwa ni 26/3/2011 siku ya jumamosi tena…HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA MDOGO WETU,DADA YETU,MAMA MDOGO WETU, SHEMEJI YETU, PIA RAFIKI YETU. NA USTAREHE KWA AMANI, TUTAKUKUMBUKA DAIMA.
UA HILI NIMETUMIWA NA KAKA ISSACK CHE JIAH AMBAYE PIA NI MSOMAJI WA MAISHA NA MAFANIKIO. AHSANTE SANA.

9 comments:

  1. Mhubiri 3:1-9

    1 Kuna wakati uliowekwa wa kila kitu, hata kuna wakati wa kila jambo chini ya mbingu: 2 wakati wa kuzaliwa na wakati wa kufa; wakati wa kupanda na wakati wa kung’oa kilichopandwa; 3 wakati wa kuua na wakati wa kuponya; wakati wa kubomoa na wakati wa kujenga; 4 wakati wa kulia na wakati wa kucheka; wakati wa kuomboleza na wakati wa kurukaruka; 5 wakati wa kutupa mawe na wakati wa kukusanya mawe; wakati wa kukumbatia na wakati wa kuepuka kukumbatia; 6 wakati wa kutafuta na wakati wa kuacha kutafuta kilichopotea; wakati wa kuweka na wakati wa kutupa; 7 wakati wa kupasua na wakati wa kushona, wakati wa kukaa kimya na wakati wa kusema; 8 wakati wa kupenda na wakati wa kuchukia; wakati wa vita na wakati wa amani. 9 Mtendaji ana faida gani katika jambo analofanyia kazi ngumu?

    ReplyDelete
  2. DADA MDOGO WETU ASIFIWE.
    Japo umetutangulia lakini sisi familia na marafiki wote wa MAISHA
    BADO TUNAKUWEKA KUWA UPO KATIKA FIKRA ZETU NA TUNAJUWA KUWA bado ni familia ya maisha na mafanikio tunakukumbuka na leo hii tuliadhimisha siku yako ya kuzaliwa na siku yako ya kumbukumbu TUnajuwa kuwa kiroho bado upo nasi ila kimwili umetutoka ,LEO NI SIKU YA KUZALIWA KWAKO NA LEO NI SIKU MWISHO YA KUMBUKUMBU KUTIMIZA MWAKA MOJA TOKEA UTUTOKE HAPA CHINI YA JUA TUNAJUWA BADO UNAISHI TUNAZIDISHA MAOMBI YETU KWAKO NA WEWE ENDELEA KUTUOMBEA ILI NASI TUWE NA AMANI NA UPENDO HAPA ULIPOTUACHA HAPA NI PAGUMU SANA WEWE UMEVUKA MTO NA UNAELEKEA MJI WA SAYUNI MIMI KAMA FAMILIA YA MAUSHA SINA ZAIDI NAKUTAKIA MAISHA YA KITAKATIFU ASIFIWE USIFIWE AMINA
    CHE JIAH

    ReplyDelete
  3. Hata huko ulipo, tunaendelea kukusifu, weye, Asifiwe Mtoto Mzuri!


    Hepi betideyi, kwako!

    ReplyDelete
  4. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema pema peponi.

    ReplyDelete
  5. Pole sana mlongo, ni uzuni sana kuona hii picha na mnafanana sana. poleni sana kwa familia yako yote.
    Mungu amlaze mahali pema peponi

    ReplyDelete
  6. @Ray..Halafu mchungaji wangu Ray Njau unanifurahisha sana...!

    Tunamshukuru Mungu kwa vile ilimpendeza kumleta Asifiwe siku hii, mimi ninachoamini ni kwamba kile alichotumwa kuja kukikamilisha alikwisha kikamilisha na ndio sababu akarudi kwa baba yetu wa mbinguni.

    Siku asifiwe alipozaliwa, mimi na familia yetu tulikuwa tunaadhimisha miaka kumi kamili ya mama yetu mpendwa kurudi kwa baba yetu wa mbinguni...

    Mama yetu aliishi miaka 25 tu na Asifiwe miaka 22 tu.., Basi sifa zote tumrudishie yeye kwa maana ana kusudi na kila jambo. Asifiwe Mungu wetu, Amen!

    ReplyDelete
  7. Shukrani za dheti ziwafikia wote mlipita hapa na kuwa nami katika siku hii. Na mwenyezi Mungu na azidi kuwapo upendo. Muwe na amani na upendo uzidi kutawala nyumbani mwenu na pia kila mtakapokuwa. Ahsanteni sana. MUNAPENDWA WOTE.

    ReplyDelete
  8. Mungu muweza wa Yote Awatie nguvu siku zote na Upendo wa Mungu baba utawale milele,Amina.

    ReplyDelete