Sunday, November 20, 2011

JUMAPILI NJEMA KWA WOTE...NA TUKUMBUKE KUMSHUKURU MUNGU KWA TULICHONACHO/TULICHOPEWA NA TULICHOPATA!!!

Bwana ndiye mchungaji wangu.Sitapungukiwa na kitu. Katika malisho ya majani mabichi hunilaza. Kando ya maji ya utulivu huniongoza. Hunihuisha nafsi yangu, na kuniongoza. Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake'. Naam, nijapopita katika bonde la uvuli wa mauti. Sitaogopa mabaya. Kwa maana wewe upo pamoja nami. Gongo lako na fimbo yako vyanifariji. Waandaa meza mbele yangu. Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu. Na kikombe changu kinafurika.Hakika wema na fadhili zitanifuata. Siku zote za maisha yangu. Nami nitakaa nyumbani mwa bwana milele. Amen. ZABURI 23:1-6.
JUMAPILI NJEMA KWA WOTE NA WOTE MNAPENDWA!!!

4 comments:

  1. Asante kwa ujumbe wa kiroho kwa jumapili hii. namshukuru mungu kwa kila pumzi anayo nipa. jumapili njema na wewe,leo nasherhekea siku yangu ya kuzaliwa,japo siku kamili ni jumanne 22/11/2011. kutokana na kuangukia siku ya milimo/kazi leo ndo nakula pweza wangu. kaka s.

    ReplyDelete
  2. Asante kwa zaburi ya 23, huwa inanibariki sana. Nawatakieni jumapili njema wooote watakaopitia blogu hii.

    ReplyDelete
  3. Ubarikiwe sana da Yasinta Mungu azidi kukufunulia zaidi na wengine tufaidike kupitia hapa.

    ReplyDelete
  4. Kaka Sam! una vituko wewe ngoja siku moja nikupikie hiyo supu maana naona unaipenda kwelikweli...Kaka S... nakutakia nawe kila la kheri kwa kusheherekea siku yako najua ni leo jumanne. Sijui unatimiza miaka mingapi:-)
    Mija! nifuraha kwangu kama umejisikia hivyo. Nawe pia nahisi umekuwa na jumapili njema kwani umepita katika blog hii.

    Da´Rachel nawe pia ubarikiwe. Na asante kwa hiyo baraka.

    ReplyDelete