Nimeamka asubihi hii na kukutana na ujumbe huu kwenye simu yangu ya kiganjani kutoka kwa kaka yetu na wanablog mwenzetu Shaban Kaluse, ujumbe unasema hivi:- Dada Yasinta nimegongwa na gari. Naomba uwajulishe wanablog kwamba nimepata ajali na niko AMANA ILALA kwa matibabu. Nimevunjika mono wa kulia. Nilikuwa navuka barabara maeneo ya Tabata Mawenzi ili kupanda daladala, nikagongwa na daladala lingine ambalo lilikuwa likiovertake kushoto ili kuwahi abiria, mimi sikuliona kabisa. Namba za hiyo daladala ni T 837 AUK.
pole sana mwenzetu msomaji wa blog yetu ya maisha hayo ndo maisha mungu atakupa heri utapona na utaendelea na shughuli zako .
ReplyDeleteusijali na pata faraja na soma maisha na mafanilio
pole sana mpiganaji mungu akupiganie upone haraka uje uendeleze libeneke!
ReplyDeletePole sana Kaka Kaluse, Mungu atakuponya..
ReplyDeleteJamani nchi yetu ina hatari sana..yaani watu wanajali pesa tu hata usalama hawaangalii tena, Hebu angalia kama ajali hii ilivyotokea!!
Mungu yuko nawe kaka Kaluse.
Pole sana kaka Kaluse,Mungu yu pamoja nawe.da'Mija wanawahi kula vichwa basi hata wakkiuumiza wewe hawajali.
ReplyDeletePole sana Ambiere Kaluse!
ReplyDeletePole sana. Nakuombea upone mapema.
ReplyDeleteMungu ni mwema anaweza na ana makusudi yake,hayo ni mapito tu. Prayer,blessings and Courage!
ReplyDeletePole sana Kaka kwa kupata ajali, nimepokea taarifa hii kwa masikitiko makubwa ila Mungu yupo yeye ni muweza wa yote atakusaidia utapona haraka.
ReplyDeleteMkono wa mungu usiopungukiwa, usimpungukie bali uwe ukimgusa kila siku na kumpatia uponyaji wa haraka,
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteoperation yake imekuwa ikipigwa danadana...jana nilipoongea naye alidai kwa anatarajiwa kufanyiwa saa 10 jioni.
ReplyDeleteTutaendelea kuwajuza yanayojiri!