Wednesday, October 12, 2011

HALI YA MTOTO CECILIA NI MBAYA ARUDI BILA KUFANYIWA OPERESHENI

Mtoto Cecilia wakati akiwaomba wasamalia wema waweze kumsaidia.



Hapa Mtoto Cecilia akitoka Hospital ya Regency Dar akiwa ameshikwa mkono na afisa mmoja wa Channel Ten tayari kwa kuelekea Airport kuanza safari ya kwenda India.

Mtoto Cecilia alitangazwa hivi karibuni na Vituo mbali mbali vya habari akiomba msaada wa kusaidiwa pesa za matibabu ambazo zingeweza kumwezesha kufanyiwa operesheni ya moyo ambao umempelekea mpaka Tumbo lake kuvimba kama unavyoliona.

Taarifa za Cecilia ziliweza kutolewa na Miss Tanzania wa mwaka 2006 Bi .Hoyce Temu pale alipoamua kujitokeza na kumtangaza Cecilia akiomba msaada huo. Wasamaria wema walijitokeza na kumsaidia Cecilia mpaka akaweza kwenda India kwa matibabu, cha kusikitisha sana ni kwamba matibabu yake kwa njia ya operesheni yameshindikana kutokana na moyo wake kwa upande mmoja kuathirika na sumu ambayo madaktari wa India wamesema inasababishwa na Sumu ambayo ipo kwenye Mihogo, sumu hiyo huwaathiri sana watoto wenye umri kama wake.

Kwa hiyo imekuwa ni vigumu kumfanyia operesheni hiyo, wakashauri atumie dawa tu ili kuweza kuitoa sumu hiyo, Mtoto Cecilia mpaka sasa hali yake sio nzuri anawaomba watanzania mumuombee ili aweze kupona na aweze kutimiza azma yake ya kuwa Mwalimu. Watanzania tunashauriwa tukiona hali ambayo ni tofauti kwa watoto wetu tuwawaishe Hospitali mapema kwa uchunguzi tunaweza tukawaepusha na hali kama hii aliyofikia Cecilia.
HABARI NIMEIPATA KWA KAKA:
Henry Kapinga wa KAPINGAZ Blog

4 comments:

  1. Mfumo mmoja tu mbovu katika mwili wa binadamu unaweza kuathiri mifumo mingine tofauti namna ya huyu binti: mfumo wa damu waathiri mfumo wa chakula, na hisi.


    Nyongeza kutoka kwangu ni hili: dawa za Kiswahili nazo zifiriwe hapa kwani kama ni sumu ya mhogo (na nasikia mara ya kwanza leo ipo), je Wahenga waliitibu vipi kwa kuwa nao walikula mihogo?


    Pole Mwanangu, Cecilia: mie tayari kukuombea upone!

    ReplyDelete
  2. Mmmmhhhh kaka Manyanya dunia hii inamambo. Sumu ya Mihogo sijui tutaepukaje?

    Pole da'Cecilia Mungu yupamoja.

    ReplyDelete
  3. Huyu mtoto cesilia apelekwe Nigeria kwa TB Joshua.Kwani anapoishia mwanadamu mungu ndio huwa anainzia.

    ReplyDelete