Mmmmh! Kazi inaanza sasa. Kaziiiii kwelikweli, maana mtu unavaa nguo na mwisho unaonekana kama una kilo elfu kumi. Haya ngoja niache.
Ila pia ni wakati mzuri sana hasa miti inapopata rangi nzuri kama huu hapo juu inapendeza kusema kweli...Tatizo humwoni mtu ...pia ni kipindi kizuri kwenda mstuni kuchuma uyoga ila unatakiwa kujisitiri kweli .... huu mti rangi zake nipezipenda sana ila muda si mrefu majani yote yatapukutika na kuuacha na vijiti tu au mti unakuwa "uchi":-(
Dada habari za siku.
ReplyDeleteDada Yasinta,niko katika mchakato wa KUFUFUA JUMUWATA(Jumuiya ya Wanablogu Tanzania).
Tafadhali naomba ufungue hii kurasa ya http://blogutanzania.blogspot.com/ kisha upendekeze jinsi ya kufufua JUMUWATA.
Luiham Ringo.
Habari za siku.
ReplyDeleteKama mwanablogu kutoka Tanzania,nakuomba kushiriki kuchangia Mchakato wa KUFUFUA JUMUWATA(Jumuiya ya Wanablogu Tanzania).
Tafadhali naomba ufungue hii kurasa ya
http://blogutanzania.blogspot.com/
kisha upendekeze jinsi ya kufufua JUMUWATA.
Ahsante
Luiham Ringo.
AFYA NJEMA NA BARAKA TELE!!
ReplyDeletekwa hiyo baada ya muda mtakuwa kama mpo kwenye friza
ReplyDeleteInaonekana hali nzuri kwa sasa halafu muda mfupi baadaye barafu na theluji. Kwa kweli Mola kaibariki bara letu la Afrika.....
ReplyDeleteJohn Fisher Kanene
Hivi Dada Yasinta unawezaje kutambua uyoga wenye sumu na ule ambao hauna sumu, maana nishasikia kesi nyingi tu za watu kula uyoga wenye sumu baada ya kuuchuma msituni
ReplyDeleteWote asanteni kwa kutochoka kipita hapa na kuacha kitu.----Kaka Bennet niwapo mstuni kwa ville najua aina tatu tu basi nachuma hizo ni "Chantarelle" ni ule uyoga wa njano au orenji, karl johan, sijui jina la kiswahili na pia kuna jamii ya "chantarelle" ambao ni blauni na upo kama mrija vile. Zaidi ya hapo sichumi uyogo mwingine. Ahsante kwa kutujali.
ReplyDeleteMtoto Mzuri wewe! Bado naangalia picha! kwa hiyo usiniulize umeandika nini!:-(
ReplyDelete