Nimerudi toka kazini huku nikawa na hamu kweli kweli ya supu...baadaye nikakumbuka nina spinachi. Kwa hiyo hapa, ni supu ya spinachi ambayo ni:- spinachi, maji, na chumvi. Inaandaliwa kwa dakika 10...Kwa anayetaka anaweza kuweka nusu kikombe cha maziwa au cream. na katika kula unaweza kula na kipande cha mkate pia yai moja la kuchemsha. Ila Kapulya hapendelei sana vitu hivyo kwa hiyo anakula kama ilivyo. KARIBUNI SANA TUJUMUIKE!!!!
Sijawahi kuonja hiyo kitu!
ReplyDeleteIla imekaa kiafyaafya vile ingawa sina uhakika kama inatufaa siye walevi!:-(
he hee,supu ya spinach na hang-over hii dada??
ReplyDeletengoja kidoogo ntarudi kunywa
YAM YAM,NITAKUTAFUTA BAADAE DADA.
ReplyDeleteSimon! Basi nakushauri ujaribu au panga safari uje nitakutenezea utaacha kula vyakula vingine vyote. Ni kweli ina afyaafya...Hata kwa walezi ni inapanda:-)
ReplyDeleteKaka isaackin! umenichekesha kwelikweli ...haya ukirudi utaikuta na utaifurahia...
Edna ni kweli YAM YAM, nitafurahi ukintafuta:-)
MIE NIENGENEZEE SUPU YA MBELELE
ReplyDeleteHAPO TUNGEKUWA WOTE ILA NA HII KWAKWELI MIMI HUWA NATENGENEZA MWENYEWE KILA JUMAPILI NI SUPU MZURI SANA ILA MCHANA HAPANA INAWEZA ISIPANDE KAMA ALIVYONENA NDUGU YANGU ISAACKIN JUMAPILI HII NAFUATA FIGILI PALE SOKONI BUGURUNI NITAYARISHE KABISAA TENA UMENIKUMBUSHA
CHE JIAH ISSACK
Hivi ni jumapili leo? mie nilidhani ni IJUMAA? mmmhh sijui ni nani katingwa hapa...Hiyo figili usinnyime sijui italiwa na nini?
ReplyDeleteumenikumbusha supu zaaina mbalimbali. kuna supu ya kongoro,supu ya utumbo wa mbuzi,supu ya mkia,supu ya kichwa,supu ya kuku wa kienyeji, supu ya ulimi, supu ya mapumbu ya ng'ombe/mbuzi, supu ya pweza,supu yasamaki wakuchemsha.katika hizi kiboko ni kongoro ikifuatiwa na supu ya nanii za ng'ombe na mbuzi,hasa kwa waonjaji wa pombe kama sisi.Kaka S
ReplyDeleteKakaS. Duh! ni kweli kuna supu nyingi zote hapo ziƄpo juu ila hiyo ya nani hapana...nakumbuka siku moja nikiwa katika mizunguko yetu tukafika mpaka MTO WA MBWA na pale tukasimama na kupata supu ikaja hiyo supu ya nani we bwana weee bahati mbaya walikata vibaya basi harufu hiyo. Nakuambia nilipakua si mchezo na hamu ya supu yote ikaisha ....sema zaidi sasa!!
ReplyDeleteYasinta unataka kudai NANIHII zinanuka?
ReplyDeleteSimon! za hiyo supu ya huko mbwa wa mto yaani ya mbuzi ..ni kweli ilikuwa inanuka ..SAMAHANI LAKINI NI KWELI:-( Kwani wewe umewahi kula?
ReplyDeleteKwa walevi kama mimi wa KITANZANIA ni vigumu kuruka hiyo kitu!:-(
ReplyDeleteIla labda KUNUKA na KUNUKIA ni pua ya mtu!:-(
Oh! Simon unaposema mlevi una maanisha nini? ni kweli pua zetu zipo tofauti mwingine anaona inanuka na mwingine anaona inanukia.
ReplyDeleteSi ulevi ni ulevi tu Yasinta?
ReplyDeleteAsante da'Yasinta kwa Supu, kwangu naona bora hivyo kuliko na mathiwa tena, mmhh mimi si mpenzi wa maziwa. Jamani kaka S [Sam] mimi sikuwanajua kama kuna Supu ya nanihii, kumbe kaka Kitururu na da'Yasinta mmesha onja,nilitamani kuonja lakini da'Yasinta umenitisha.
ReplyDelete@Kaka Isaac ukikuta tumemaliza itabidi unywe ya Maharage!!!!!!!!
duh hiyo nikikuta mmemalizza ntafurahi wacha.
ReplyDeletehizo supu za p*mbu za ngombe basi kipindi fulani nimepita mitaa ya suga ray nje nikakuta jamaa wanazichoma za nguruwe mbuzi na ngombe ebwana zilikuwa zimenona kweli kweli mi sikujua kitu gani nikaagiza sahani top mix na pilipili kibao baada ya kufakamia ndo nikauliza nini hiki ndo nikaambiwa ni mbupu za wanyama hao kutapika nikataka kumeza nikataka.
hapo sawa
ReplyDeleteAh! aH! ah!
ReplyDeleteHizo nani hii za ng'ombe na mbuzi kwa sie wazoefu tunaziita ASHUA, ISAACK kumbe unakuja suga ray siku hizi inaitwa KISUMA
ReplyDelete