Friday, September 23, 2011

HII NI HABARI YA KUSIKITISHA SANA WATOTO WAWILI WAUWAWA NA MAMA YAO MZAZI NCHINI SWEDEN!!!

WATOTO WALIO UWAWA NA MAMA YAO MZAZI, ELIAS (KUSHOTO) MIAKA 4 NA TEVIN MIAKA 8.WALIUWAWA KWA KUZAMISHWA KWENYE MAJI.TUKIO LILITOKEA TAREHE 18 SEPTEMBER SIGTUNA SWEDEN.

Kwa undani zaidi unaweza kusoma hapa na pia hapa.

9 comments:

  1. Ndiyo Simon inasikitisha ..ukizingatia wengine kila kukicha wanatafuta watoto .

    ReplyDelete
  2. Ama kweli kila siku ina jina lake na kila tarehe ina tarakimu zake na kila sekunde na tukio lake iwe ni hasi au chanya.Kila mtu hulia mama yangu au Yarabi nafsi yangu!
    Hapa sijui hapa tulie na nani?
    Dkt Remmy aliimba:
    Kifo eeh,kifo hakina huruma!Hapa tuongeze akina mama eeeh,mioyo yenu ya uchungu wa uzazi na mioyo huruma imeishia wapi?

    ReplyDelete
  3. Zaburi 127:1-5

    Wimbo wa Mipando. Wa Sulemani.

    1 Yehova mwenyewe asipoijenga nyumba,

    Ni bure kwamba wajenzi wake wameifanyia kazi ngumu.

    Yehova mwenyewe asipolilinda jiji,

    Ni bure kwamba mlinzi ameendelea kukaa macho.

    2 Ni kazi ya bure kwamba ninyi mnaamka mapema,

    Kwamba mnakaa mpaka kuchelewa,

    Kwamba mnakula chakula kwa maumivu.

    Hivi ndivyo anavyompa hata mpendwa wake usingizi.

    3 Tazama! Wana ni urithi kutoka kwa Yehova;

    Uzao wa tumbo ni thawabu.

    4 Kama mishale mkononi mwa mwanamume mwenye nguvu,

    Ndivyo walivyo wana wa ujanani.

    5 Mwenye furaha ni mwanamume ambaye amelijaza podo lake na hao.

    Hawataona aibu,

    Kwa maana wataongea na adui langoni.

    ReplyDelete
  4. inasikitisha saana,kweli sio wote wasema mungu mungu watauona ufalme wa mbigu.huyu dada alikua mlokole flani hivi muimba kwaya mzuuuur sana

    ReplyDelete
  5. Ni vibaya ku generalize; ila kuna habari kama hii niliisoma think this year; Mkenya mwingine Marekani kaua mke na watoto wake wawili na kumbakiza mmoja. Majirani wakabaki wanashangaa kwani hawakutegemea. Na baada ya kuwaua aliendelea kudunda mtaani huku akiwambia walimu wa mmoja wa watoto wake kuwa mtoto sijuhi mgonjwa. Maiti zilikutwa ndani baada ya days. Je hawa wenzetu ni wakatili au ni coincidence.

    ReplyDelete
  6. Habari hii Inasikitisha sana. Nimeifuatilia hiyo habari, hiyo lugha na viziro ziro juu ya herufi vimenichanganya, nikaishia kuangalia picha na kusoma nisichokielewa.

    ReplyDelete
  7. Mwanamama yule anaumwa akili (DEPRESSION NEUROSIS). Tumuombee apate kupona.

    ReplyDelete
  8. Ni habari ya kusikitisha. Nakubalina kabisa na Manyanya Phiri.

    Chib: Usipate shida na translation, ingiza tu majina ya mtuhumiwa kwenye google na utapata habari za kiingereza na hata kiswahili.

    ReplyDelete