Karibuni katika mahojiano yetu ya kila week. Week hii nimepata bahati kufanya mahojiano na Emu Three ktoka blog ya Diary Yangu. Kama wewe ni mpenzi wa riwaya natumaini mara ukiifahamu hii blog kila siku utajikuta utarudi kusoma hadithi moto moto anazoziandika Emu Three.
Karibu hapa na tunafurahi kuweza kufanya mahojiano na wewe. Unaweza kutueleza kidogo kuhusu wewe na blog yako?
Mimi naitwa emu-three, na nimetumia emu-three kama ufupisho wa majina yangu matatu yaani jina la kwangu la baba na la ukoo yote yakianzia na herufi M. Na wakati naanzisha hii blog, nilikuwa nawaza niweje jina gani , na mara likanjia jina hilo la miram3. Mira ikiwa ni jina langu halisi kwa kifupi na m3, ikiwa M.M.M.
• Je blog yako unatumia jina lako kamili au unablog kwa kutumia kivuli kingine na watu wanasoma na kuenjoy blog yako lakini hawajui wewe ni nani?
Blog yangu situmii jina langu kamili, natumia jina la kubuni tu `nick-name’, na watu wananitambua kama emu-three, kama nilivyosema awali kuwa ni kifupisho cha majina yangu matatu. Sina nia mbaya kutojiweka jina kamili na picha yangu, ila nililenga kuwa ninachokiandika ndicho kinieleze mimi. Nia ni kutoa kile nilichokuwa nacho, lakini ikiwa ni muhimu sana nitaweka picha yangu na kujielezea zaidi, hapo wapenzi wa blog hii watakapokuwa wengi na kupendekeza hivyo.!
• Ni miaka mingapi sasa umekua ukiblog?
Nina miaka mitatu sasa tangu blog hii ianzee kuwa hewani, mwanzoni na nilituma nianze kublog, kwani nilituma maelezo ya mwanzo kabisa kama utambulisho tarehe 14-7-2009.
• Ni nini kilikufanya uanzishe blog?
Mimi ni mpenzi sana wa kuandika hadithi, kuweka kumbukumbu za matukio(diary) na napenda sana kusoma vitabu vya hadithi, hasa riwaya(novels) , tamithiliya nk. Nikawa naandika visa, au hadithi katika makatasi, na mwisho wa siku hayo makaratasi yanapotea au kuharibika, nikawa naandika kwenye computa za ofisini, nazo zinakumbana na virusi, au unaondoka kwenye hiyo kampuni na ina maana kila kitu kinamepotea. Nikaja kugundua kuwa kumbe kwenye blog unaweza ukaweka hizi kumbukumbu, za visa, hadithi nk na sio kuweka tu, bali unaweza kupata watu wakazisoma, na mkachangiana mawazo. Na kwa vile nia yangu ilikuwa sio kuandika tu, bali pia kutoa maoni yangu, kushauri,nk kuhusu hili na lile, nikaona blog ni sehemu nzuri kabisa. Kwa mfano mimi ninaamini kuwa kuwa kila tukio lazima lina na sababu, basi kwanini nisiweke hayo matukio na kuanisha nionavyo mimi ni sababu gani likatokea kwa kupekenyua chanzo chake, na hatimaye iwe kama kisa ambacho sio burudisho tu, bali kiwe na mafundisho ndani yake!
• Je, wewe kazi yako ni kublog tu au hii ni kama kazi ya muda tu au hobby?
Kwakeli kublog niliichukulia kama Hobby, na nina kazi nyingine inayonifanya niishi mjini, na kama utachunguza blog yangu haina hata matangazo ya kibiashara, sio kwamba sipendi, bali sijawapata watu wa kutangaza biashara zao. Kama kuna atakayependa kuweka tangazo lake namkaribisha sana. Kwa ujumla natumia muda wangu wa ziada, gharama zangu mwenyewe, na nashukuru kuwa naweza kutumia vitendea kazi vya muajiri wangu kuweza kufanikisha hili, ingawaje ni kwa shida, na vinginevyo nategemea sana internet cafe.
• Nini changamoto unazozipata kwa kuwa na blog?
Changamoto ni nyingi, kwanza kama nilivyosema awali muda mwingine nategemea sana vitendea kazi vya muajiri wangu, kama computa na internet ingawaje najitahis sana kutokutumia muda wake wa kazi, ninachofanya nikuwahi asubuhii sana na kuandika kile nilichokusudia kabla ya muda wa kazi, na zaidi sana natumia internet cafe. Kwahiyo swala la muda, gharama na vitendea kazi ni changamoto kubwa kwangu kwa sasa.
• Ni nani wasomaji wa blog yako?
Ni wote hasa wale wanaoutumia lugha ya kiswahili, ingawaje wengine wanaweza kutumia nyezo zilizopo kwenye blogs, kutafsiri kwa lugha zao. Matarajio kama ningeliweza, nilitaka iwe kwa lugha mbili ya Kiswahili na Kiingereza, ili wengine waweze kutafsiri kwa kirahisi kwenye lugha zao kwa kupitia kwenye lugha ya Kiingereza.
• Ni nini imekuwa mkakati wako kwa ajili ya kujenga kujulikana kwa mwenyewe na blog yako zaidi?
Hilo pia limekuwa ni moja ya changamoto kwangu, kwani nimejulikana labda kwa kupitia kwenye blog nyingine ambazo wamenisaidia kuniweka kama blog rafiki, na wengine wamekuwa wakiambizana, na kuweza kuwavuta marafiki zao kuja kusoma visa kwenye blog hii, nawashukuru sana kwa hilo. Kama ujuavyo, watu wengi sasa hivi hawapendi kusoma, wanapenda zaidi kutizama, na kwahiyo mtu akiona umeandika taarifa ndefu, na haina hata kivutio kama picha anaghairi. Kwahiyo mkakati wangu ni kuiboresha hii blog, iwe ya kisasa zaidi, iwe sio tu kusoma, bali hata kutizama pia.
• Je unatumia mitandao mingine kama Twitter au Facebook kuitangza blog yako? Kama unazo unaweza kutuambia ili wasiofahamu waweze kufahamu na kukufuata?
Ndio natumia Facebook, hata Twitter, kwenye Twitter unaweza kunitafuta kama `emu-three’ lakini kwenye face book unaweza kunipata kama `diary yangu’
au http://miram3.blogspot.com/
• Je ni nini mkakati wako na blog yako kwa ujumla?
Mkakati wangu ni kuiboresha hii blog kuwa ya kisasa zaidi, na kuweza kuingiza e-book, kweny hii blog, nikipata wataalamu wa kunisaidia nitashukuru sana, na kwa vile leng ni kuwa mtunzi wa vitabu, basi blog hii itakuwa sehemu ya kujitangaza pia. Na ikiwezekana nisiifanye blog tu kama hobby, lakini iwe kazi yenye kuleta manufaa, sio kwangu tu hata kwa jamii kwa ujumla.
• Ni jinsi gani (mtu) anaweza kuelezea style/theme ya yako unavyo blog?
Mtindo wangu wa kublog unaweza kuelezewa kama blog ya visa vya kusisimua kutokana na matukio halisia. Ni kumbukumbu za kimaisha, kwani visa ninavyotunga ni vitu vilivyotokea na mimi naviboresha tu ili viweze kumsisimua msomaji.
• Je ni bloggers wapi ambao wewe unawaangalia na kufuata nyayo zao? Na kwanini?
Kwakweli kublog kwangu siwezi kusema nafuata nyayo za mtu fulani, sikumbuki kuwa nimeblg kwasababu ya mtu fulani, hapana, mimi nilipogundua tu kuwa kuna kitu kama hiki na unaweza kuweka vitu vyako bure, nikajimwaga, sio kwa ushawishi wa mtu, lakini wengi tu napenda blog zao, ikiwemo hii yako, na mimii huwa napenda sana kusoma walichoandika wenzangu, na nina imani kuwa kitu kipya ni kile hujakiona, kwahiyo kila blog ambayo sijaiona kwangu inanisismua kuisoma,na kuona mwenzangu ana nini katika mawazo yake!
• Je unafikiria kuwa unadaiwa na mtu akiacha comment/s kwenye blog yako?
Kuna jambo moja tuliweke akilini, mfano mtu akiweka comment kwenye blog yako, lazima atakuwa na shauku fulani, hasa iwe ya kuulizwa swali, ...au hata kama inakukwaza yeye atakuwa na matarajio fulani kuwa wewe mwenye blog unaweza kwa kutumia blog yako kumsaidia au kumsikia. Kwahiyo ni bora ukasema lolote, au usiitie kapuni, kwani ukifanya hivyo bila kuiweka hewani au bila kusema lolote, utakuona kama umemdharau, kwakweli ni deni...utakuwa hujamtendea haki mpenzi wa blog yako. Na pia kwa wale wanaosoma habari kwenye blog, ni busara pia ukasema lolote, kwani ni kama mtu kakupa kitu ukae kimiya,..ni busara kusema ahsante ...kwahiyo.unaweza hata ukaandika neno dogo tu la kushukurui au ukaandika `mmmh’ inatosha kabisa, ni maoni yangu tu.
• Je kuna thamani kujibu comment iliyoachwa kwenye blog yako wakati ukijua kuwa huyo aliyeiandika labda hatarudi kusoma jibu lake tena?
Ukiulizwa swali ni vyema kulijibu, kwasababu mara nyingi ukikaa kimya unatafsiriwa kuwa umezarau au sio, kwahiyo kinachotakiwa ni kulijibu lile swali, kwani muulizaji anaweza kuwa aliuliza hilo swali kwa maslahi yake, lakini swali hilo linaweza likawa limesomwa na watu wengi na hata kuwagusa watu wengine, kwahiyo kama yeye hakurudi kusoma majibu ya hilo swali watafaidika wengine, walioguswa nalo.
Nakushukuru sana kwa kunitupa fursa hii na sina cha kukupa zaidi ya kukuombea heri na fanaka katika utendaji wako, kwani wewe umekuwa mtu wa watu. Kujali wengine, ni kazi kubwa sana, inahitaji moyo, wewe hili umeliweza hilo, shukurani sana.
Asante sana Emu Three Kwa kufanya mahojiano haya na sisis na tunakutakia mafanikio mema katika blog yako........kuendelea kusoma habari/maelezo haya bonyeza hapa.
M3, Oyeeee!
ReplyDeleteYasinta NaNgonyani, Oyeee!
ASANTE SANA KWA KUTUPATIA MAHOJIANO NA HUYO, M3. NAFIKIRI ATAENDA MBALI NA MAANDISHI YAKE. NASEMA ASIFE MOYO: WAKATI MWINGINE HATUNAMUDA WA KUSOMA KILA HERUFI KATIKA KILA TOLEO LAKE, LAKINI TUNAMTHAMINI SANA NA SIKU MOJA TUTAPATA MUDA WA KUSOMA NA KUJADILI KILA ALICHOANDIKA. (Tutayiacha ile sahani yake safi kwa kuiramba tu!)
BIG UP!
Ahsante SANA dada Yasinta kwa kunijali hadi kuamua na wewe kuyaweka mahojiano haya niliyofanya na blog ya Tanzania Blog awards. Mungu akubariki sana.
ReplyDeleteNa ndugu yangu Goodman, nakushukuru sana kwa kuwa wakwanza kusema lolote , najua wewe hukupewa jina hilo bure `Goodman' linaendana na tabia yako. Tupo pamoja Daima
Hongera ndugu yangu emu-three, unajiamini mpaka unanipa raha...hivi ndivyo inavyotakiwa ati..:-)
ReplyDeletehuyu dada ni blogger wa ukweli. ni mtoa maoni na mchangiaji wa ukweli.
ReplyDeleteMira wewe ni mtaalamu wa kujibu maswali...
ReplyDeleteSasa ombi langu ni picha yako, wadau wako tungetamani tukufahamu kwa sura..
Hongera kwa mahojiano.
M3 nazimia sana kazi zako Mkuu!
ReplyDeleteNaavache thana Kikore!
@Mija Shija Sayi
ReplyDeleteNaapa: hata huyo Kapulya wa Maisha na Mafanikio hana kabisa picha yake huyo M3 bali maskini Kapulya ataishia na picha yake tu Bikizee waKimasai mwenye jina “WOTE TUTAKUWA HIVI HIVI HATA MIMI PIA NITAKUWA HIVI”!
Lakini picha yake M3 kuona ni sawa-sawa na kuona meno yake kuku nikwambie, Mdogo Wangu Mija!
Nashukuruni kwa maoni yenu wadau, na nimefarijika sana kuwa kumbe kazi ninayofanya inakubalika, nawakaribisheni sana kijiweni kwangu kwa wingii na mnisaidie kunipigia debe kwa wengine, ni hilo tu kwa leo. Shukurani nyote, na shukurani Da'Yasinta
ReplyDeleteNimeyakumbuka haya mahojiano ni muda kwakweli...Ahsante sana
ReplyDeleteNI SIKU NYINGI SANA, LKN KWENYE DIARY YANGU BADO IPO.....TUSITUPANE NDUGU YANGU
ReplyDelete