Blog ya MAISHA NA MAFANIKIO inapenda kuwataarifu wasomaji wake kwamba haitakuwa hewani kwa muda.
Sababu kubwa ya kutokuwa hewani, nadhani wengi mmeona/soma/sikiliza posti ya 22/6 kuwa KAPULYA atakuwa SAFARINI na posti ya 22/6 ilikuwa kama kionjo tu yaani akifikiri jinsi safari itakavyoanza ....Sio safari nyingine bali ya NYUMBANI-TANZANIA.
Nitajitahidi kuwataafu mawili matatu. TUKUTANE TENA WAKATI MWINGINE PAMOJA DAIMA. NAWATAKIENI WOTE KILA JEMA. TUTAONANA.
NGOJA DR. Remmy amalizie kwa wimbo huu......
KARIBUNI SANA SONGEA-RUHUWIKO:-(-----:-)
Safiri salama Da Yasinta. Salama zao na usikose kutujulisha yanayoendelea huko kwa Wangoni....
ReplyDeleteNajua pia kwamba utakuwa na huzuni kwani Asifiwe hatakuwepo kukulaki. Natumaini kwamba Mungu Atakutia nguvu na moyo wa matumaini....
safari njema ufike salama da yasinta
ReplyDeleteSafari njema Nangonyani!
ReplyDeleteSafirini salama Dada, msiache kutuletea zawadi ya karanga.
ReplyDeleteTutakumiss sana.
Shibe shibe shibe, haina bei
ReplyDeleteaenda kula nyumbani,
haina bei,
kwani nyumbani ni nyumbani
hata kama ni kichakani,
nyumbani kwetu, nyumbani,
Muungwana ni vitendo, karibu sana,
NIMEANDAA NDEGE YA LUPALU A.K.A UNGO
Safari njema da'Yasinta!
ReplyDeleteKila la kheri dada Yasinta na wasalimie wote hapo nyumbani....
ReplyDeleteKaribu Tized
ReplyDeleteSafari njema dada...enjoy nyumbani :-)
ReplyDelete"JASIRI HAACHI ASILI NA MUACHA ASILI NI HASIDI NA HANA AKILI"
ReplyDeleteSafari njema mdau wetu Yasinta.
Nakutakia kila la kheri afya njema,baraka tele la kila jema liandamane na michirizi ya nyayo zako njema sana.
Safari njema mama Erik! usile sana huko maana unahamu na kila kitu!!!!
ReplyDeleteKaribu bongo, natumai utakuwa umejiandaa, maana macho yalizoea mwanga, huku usiku ni giza kwakwenda mbele...lakinii usijali ndio nchi yetu ...KARIBU SANA MPENDWA, UKIFIKA UJARIBU KUTUTAFUTA...
ReplyDeletehivi mtu hukaribishwa kwao? kama ndivyo yasinta ngonyani KARIBU NYUMBANI
ReplyDeleteSafari njema, Dada! Hatimaye, KILA MTU KWAO TU! (Sikua na muda wa kusoma taarifa yako ya kwanza juu ya safari yako na hayo ni tukokana na pilika-pilika za kwangu hapa, lakini naamini unakuja nao kabisa 'wajomba' zetu akina-Erik tukacheze nao mpira nasi: huenda tutaweza kusahau kidogo mambo mazito yanaotuathili daima eti!)
ReplyDeleteSafari Njema Mama Erick!!!
ReplyDeletekaribu nyumbani usikose kutembelea vijiwe vyetu vya manzase
ReplyDeleteMlongo husisahau kuludi na mangatungu, chikandi, na mdonyolela. Safari njema kwako na familia yako. Mmbarikiwe sana. tutaonana ukiludi.
ReplyDeleteDada'ngu Yasinta, bado hujarudi tu? Kweli hii ni likizo, tumekumiss sana sana!Ukipata ka-upenyo turushie mawili matatu!
ReplyDeleteNi matumaini tu ulifika salama dada Yasinta.Kila lakheri huko bombiyumbi lol
ReplyDeleteDa Yasinta Kama upo Songea Call 0755448177 au 0655448177 au fika Ofisi ya Waandishi wa habari jengo la Saccos ya walimu mtaa wa Zanzibar uliza Nyumayo. Karibu sana nyumbani.
ReplyDeleteAhsanteni wooote nilisafiri salama namshukuru Mungu. Samahanini kwa kutowataarifu mapema. Muda ulibana mno.
ReplyDelete