Friday, May 27, 2011

MUDA WA CHAKULA CHA MCHANA AMBACHO NI MAKANDE

Karibu tujumuike , kwani ni muda wa kula sasa .... Msione kidogo na mkaogopa kuja kuna zaidi na si mnajua Makande hata ukila kiduchu yanashibisha sana....
Haya jamni Ijumaa njema basi
Baada ya mlo huu ili kuyeyusha chakula tuburudike na kibao hiki cha Innocent Galinoma.....

9 comments:

  1. Ijumaa njema!

    Ila makande yako ni meupe sana!
    Mie nayapenda yale yenye fulu randi fulani ichangiwayo na maharage!

    Halafu kama ni MAKANDE ya nazi huwa napenda mpaka ukokowake hasa ule ambao haujaungulia sana na kuwa mweusi /ule ukoko rangi ya brauni fulani halafu yasiwe na rojo sana.

    Ukinipikia hayo miye ntayalaza kwa kuwa starehe yake ni kuyala kama kiporo asubuhi ya kesho yake kabla ya kwenda gezaulole kushika jembe kwa siye wakulima hodari!

    ReplyDelete
  2. Tupo pamoja dada yangu, Makande kule kwetu twayaita `PURE'...SASA, utajaza mwenyewe matamshi yake, unyatamka kama maneno yalivyo, sio kwa kiingereza. TUPO PAMOJA

    ReplyDelete
  3. Makande kwa chai asubuhi kabla ya kwenda shamba kupalilia mahindi sio sikuhizi wanakula sausege na kebab.

    ReplyDelete
  4. Ijumaa njema nawe pia Simon!
    Inaonekana wewe ni mzoefu sana wa makande na pia ni mpishi mzuri sana. Nina uhakika mkeo "Wifi" hatapata taabu kwa mapishi:-) Mie huwa napenda yale makande ya mahindi mabichi, maharage mabichi, katanga mbichi au njugu..."Mdojolela"

    em3! shukrani kwa kuwa pamoja na kwa jina hilo la kipare "PURE" sie kwetu ungonini twaita "makandi" au "Ngandi"

    nyahbingi worrior! pia Simon ! hapo mmesema makande ukiyale jembe mpaka lyamba...yaani mpaka jioni.

    ReplyDelete
  5. @Yasinta: Mahindi mabichi siye WAPARE hatuyaiti MAKANDE kwa kuwa tunaamini ni chakula tofauti. Hayo tunayaita KIBULU.

    Kwa hiyo ukiongelea MAKANDE Mpare atajua unaongelea PURE na sio KIBULU.:-(

    Au sio M3 mpare mwenzangu -nimekosea?

    ReplyDelete
  6. Simon! hata wangoni hawatumii mahidi mabichi bali ni kule Ubenani na ndiko nilikojifunza kula hicho chakula. Fadhy upo nisaidie mtani...

    ReplyDelete
  7. makande oyee! kila kabila lina jinsi ya kuyapika makande haya.sisi wazee wa kazi, wasu na wanya..... wachatu! utayapenda.sifa ni ileile yasiwe na rojo yani magumu! kama uguliwetu waki suku... na kinyamw....
    asanete dada yasinta.Kaka s.

    ReplyDelete
  8. ASANTE DADA KWA KUTUKARIBISHA MAKANDE HATA MIMI HUWA NAYAPENDA SANA LAKINI MIMI HUWANIKIPIKA NACHANGA NA VIANZI MVIRINGO NA VIUNGO KAMA NYANYA,VITUNGUU,PILIPILI HOHO NA KITUNGUU SWAUMU,KAROTINA BINZARI KARRE NA NYANYA KIDOGO YA KOPO ILI ILETE RANGI NZURI BILA KUSAHAU NAZI NA NYAMA YA AINA YOYOTE UNAYOPENDA YAANI NAKWAMBIA UKIWATAYARI UTAJILAMBA KWA KWELI KWA UTAMU TENA UMENIKUMBUSHA NA KUNITAMANISHA NAENDA KUPIKA SASA HIVI ASNTE YASTA

    ReplyDelete
  9. Asante usiyeweka jina,mimi sikujua kama makande yana mapishi mengi zaidi,kweli blog ni shule.da Yasinta mmejinoma eehh na makande wangu!!!

    ReplyDelete