Thursday, May 19, 2011

JAMANI KWELI HUU NI UUNGWANA??

Haya ndiyo maisha ya kawaida ya wakazi wa jijini Dar Es Salaam. Ambapo akina mama wajawazito ni nadra kupishwa kwenye viti vya daladala. Pichani ni jambo la kusikitisha ndani ya daladala moja kuona uonavyo. Jamani huu ni uungwana kweli?.....Picha hii imenikumbusha siku moja nilichukua daladala kutoka Ruhuwiko nikiwa na safari ya kufika Peramiho na mara kwenye daladala akaingi bibi mmoja na hakuna aliyenyanyuka kwenye kiti chake . ...isipokuwa mimi na wasafiri wengine wakaniambia kama daladala ile ni ya kwangu au nimepanda bila kulipa nauli?

Jibu langu lilikuwa kwamba nimejiona mimi mwenyewe ndani ya bibi huyu maana baada ya miaka kadhaa nitakuwa hivi na nitapenda kukua kwenye siti ....sijui kama walinielewa....Je wewe unaelewa ? Na je ungekuwa wewe upo ndani ya daladala na mamamjamzito, mama aliyebeba mtoto mgongoni bibi au babu wanaingia ndani ya daladala je ungempa siti yako?

12 comments:

  1. Unanikumbusha jana na juzi na kila siku , kwanini mimi ni mdau wa daladala, kupaka rangi imekuwa ndio jadi.
    Unajua kupaka rangi? ni kusimama kwenye daladala hujapata sit...huku Dar, ndio mtindo wetu.
    Basi ili upate siti kwenye daladala,lazima utumie mtindo wa `kugeuza nalo' yaani unatembea muda kueleekea huko gari linapotokea, upite viti kadhaa vile vyenye abiria wengi, ukaliwahi gari kabla halijafika kituo cha mwisho,
    Ukiingia, aaah, utapata siti, na adha ya kupaka rangi utaikosa. Ila ndio unalipa nauli mara mbili ya kwenda na kurudi , halafu unatumia nguvu ya kutembea.
    Sasa hii hali ya kuingiwa na mitihanii kuwa umegeuza nalo, baada ya kutembea mwendo mrefu, ukalipa nauli mara mbili na bahati umekaa kwenye kiti , anakuja kusimama pembeni yako mama mwenye mtoto au mja mzito...panakuwa patamu hapo!
    Ukumbuke safari ya kutoka Msasani HADI Goms, ni masaa mawili au matatu...kama unapaka rangi ndio usiombe, maana humo ndani unasimama kwa mguu mmoja, ukishusha wa pili umemkanyaga mwenzako...ugomvi...na ugomvi wake hauishi mapaka mwisho wa safari!
    Mtihani huo?

    ReplyDelete
  2. emu-3! Kaazi kweli, kweli huo ni mtihani tena mkubwa kweli wa kupaka rangi...sikuwahi kusikia hili neno kupaka rangi..AHSANTE. Lakini kinachonishangazi mimi ni kwamba inawezekana kuna daladala chache sana na wasafiri ni wengi mno? Na kama hivyo kwa nin i tusiwe na mabasi makubwa badala ya daladala nyingi ambazo watu wanapaka rangi kwa mguu mmoja...Au basi kwanini kusijengwe barabara za baiskeli? Mmmmh! ngoja niache na wengine wasema........

    ReplyDelete
  3. HUJUI DUNIA IMEFIKA UKINGONI ?

    'SONI KUSI' 'Magono haga',Dada Yasinta hayo mambo ya kupisha wazee,akina mama wajawazito na wenye watoto si kwa Dar peke yake hata mikoani hapishwi mtu.

    wanacho jali kalipia siti ama kawahi kiti,masuala ua umri hakuna siku hizi,Heshima hakuna miongoni wa watoto na vijana wa siku hizi.

    ReplyDelete
  4. Christian Sikapundwa! Kwa kweli hii inasikitisha sana kama ulivyosema "SONI KUSI" naitamani zamani yangu...Hakika naweza nikaamini siku zimefika ukingoni...
    kwani hiyo nimehakikisha pia si kumpisha mkubwa tu hata mtoto mdogo watu hawawezi kumwambia njoo ukae nami..au yule aliyebeba mtoto kwanini wasimpokee na yeye aendelee kupaka rangi? Tunakoenda naona roho zetu u-MIMI unazidi kuongoza kweli na tunasahau kuwa hela zilimua bwana yetu Yesu Kristu.....

    ReplyDelete
  5. Huku ni kuporomoka maadili na si jambo jingine. Tumekosa huruma hata kwa akina mama wajawazito na bibi vizee?? Halafu angalia mwanafunzi akiwa kakaa kwenye siti watakavyomzogoa!! Kama wewe mtu mzima huna adabu na huruma utamfundisha nini mwanao? Tuwe waungwana jamani kwani hiyari huanzia nyumbani...

    ReplyDelete
  6. TUSIANGALIE PICHA TU
    Lazima tuangali chanzo na kujiuliza, jee ni nani wakulaumiwa.?

    Tusilaumu watu waliokuwa hawana hatia kwa kijifurahisha nafsi zetu, katika suali zima la usafiri wa dala dala, ninavyoona mimi hapo abiria sio wakulaumiwa, kungekuwa na sheria za kiti kimoja abiria mmoja na nimarufuku kusimama katika dala dala ambazo hazina nafasi kama hizi, kusingikuwa na msongamano, na watu kusimama ndani ya dala dala.

    Maisha yote kama hakuna sheria UNGNWANA NA HESHEMA, inakosekana mahala popote katika dunia hii ilutuzunguka.

    Kwa hiyo hapo tujiulize ni nani wakulaumiwa..?

    ReplyDelete
  7. Duuhhhii kupaka rangi ndiyo leo naipata kaka emu-three!

    Sawa umegeuza na basi na umelipia pesa x2 je kwani ukimpokea hata huyo mtoto basi si utakuwa umekaa na mama aendelee kupaka rangi?

    Zamani kuliuwa na uda tuu sasa magari ni mengi lakini bado mahitaji hayawafikii walengwa.

    mimi nawaza hivi vipanya visimamishwe na kuwe na mabasi makubwa mengi,labda tatizo litapungua.

    Pia kulikuwa na mabasi ya wanafunzi sijui yaliishia wapi?maana nao wanahangaika sana.
    Bongo Tanzania.
    Asante da Yasinta.

    ReplyDelete
  8. kwa kiasi kikubwa nataka kukubaliana na ndugu Ebou's. kuna wakati unaona mtu mzee ama mtumzito (mjamzito)akipanda gari kwa makusudi akitegemea kuachiwa siti ilhali dakika chache zijazo kuna uwezekano wa kupata gari nyingine. kuna utamaduni unajengeka wa hawa wasiojiweza kwa namna fulani ku-take it for granted.

    katu sitetei kuwa kuna mmomonyoko wa maadaili kwa walio na nguvu kujitolea kuwaachia viti wasiojiweza kama hawa. lakini hili ni la mtu binafsi. kama hataki katu usimjadili kuwa hana eti inayoitwa adabu ama heshima. unajuaje hao waliokaa chini mmoja ana ngiri, mwingine ana tumbo la kuhara, mwingine CD4 zimemnywea na mwingine ana msongo wa mawazo kutokana na mambo anuai kama kufiwa, kufukuzwa kazi na kadhalika. kweli kwa kuangalia picha tu haifai kuweka hitimisho ambaolo wengi wetu tunatamani kudhani ni hivyo.

    kama hakuna sheria kama nchi zingine za kuwaachia viti pregnant women na senior citizens, kutowaachia viti wasiojiweza sio kosa, ingawaje pia ni jambo lisilopendeza

    ReplyDelete
  9. Labda ningependa pia kusema hivi au kuuliza Hawa watu wa daladala hata kama ni pesa lakini kwa nini wasichukue watu ambao wanatosheleza vile viti vilivyokuwa? Kwa mtizamo wangu nadhani ingekuwa nafuu kwa wote abiria na wao pia...ruksa kubisha.

    ReplyDelete
  10. Mmmhhh!


    Hapa Mkuu Ebou na Mkuu John Mwaipopo hapa wamenisemea kwa kuwa naegemea hukohuko kiwazo waliko!

    ReplyDelete
  11. Ahsanteni sana ila napenda kusema hivi upendo unakuja pale panapokuwa na sheria na kanuni za kuisha na watu.

    Lawama hizi ziwafikie kampuni za usafirishaji na wenye kutoa sheria katika vyombo vya madaladala. jina silijui ngelimwaga hadharani kama hili lakwetu la kwetu ni (Montgomery County Ride-On Bus System.)

    Labda dada (yasinta.com) ungefatilia upate picha halisi na kutetea abiria wanaopaka rangi. kwa maslahi ya wenye daladala bila kujali upendo afya na usalama wa haki za mwanadamu.

    PENDEKEZO..Nengependa dada Yasinta kunipandishia mlingotini BLOG Yangu ya swahilivilla.blogspot.com, kwenye bloglist yako.
    .Shkran.!

    ReplyDelete
  12. Hii inanikumbusha nikiwa bado mdogo, tulisafiri mimi, wadogo zangu wawili, mama na baba yetu. Tulikuwa tunatoka Tanga kuelekea Arusha. Alipanda mama mjamzito, baba yangu akampisha yeye akasimama, Yule mama mjamzito alifika akashuka, baba yangu akarudi kwenye siti yake, hatukwenda mbali akaingia babu kizee hivi, baba tena akampisha yeye akasimama, Yule babu alifika akashuka sisi tukawa tunaendelea na safari. Nilikuwa simuelewi baba yangu mpaka nikakasirika sana kwa ninin yeye asimame awapishe watu hata asiowajua… aliingia mama mwingine mjamzito kama wa miezi 8 hivi kwani alikuwa anaonyesha amechoka sana. Baba yangu akampisha tena. Tulipofika Yule konda na dereva walimuita baba yangu pembeni wakamwambia hatujawahi ona kitu kama tulichoona leo. Wakamrudishia nauli yote aliyolipia ya familia nzima. Wakamwambi kweli ww mtu wa Mungu! Nilijifunza kitu kikubwa sana siku ile…..

    ReplyDelete