Tuesday, May 24, 2011

BLOG MPYA KUANZISHWA/TWAPATA MJUKUU!!

Kwanza samahani kwa kutomtangaza mjukuu huyu kwa muda uliotakiwa. Ni kutokana na sababu za kifamilia ndizo zilizonifanya nishindwa kuwapa taarifa mapema kuwa Mwanamke wa shoka mtarajiwa kaibuka. Na si mwingine tena ni binti yake Mama Maisha na Mafanikio. Da´Camilla zaidi unaweza kumtembelea Bahati .....Nimekuwa bibi.....LOL

11 comments:

  1. du! nshamtembelea 'mjukuu' yaani mtoto wa nyoka ni nyoka (kwa kizungu kutia msisitizo: like mother like daughter).

    'nadhani' ni blogu nzuri. unajua kwa nini natumia neno 'nadhani'. ni kwa sababu ya KILUGHA kilichotumika huko.

    ReplyDelete
  2. Kaka John...ha ha ha haaaa like mother like daughter...Halafu kaka John nitamwambie aweke sehemu ya kutafsiri ...usikonde

    ReplyDelete
  3. Kaka Mcharia! naona kama kuna kitu ulitaka kusema na ukasita vipi?

    ReplyDelete
  4. Shkran hizi ni za kwako dada Yasinta kwa kunipandishia lebeneke langu kwenye mfumo mzima wa bloglist zako, na huo ndio upendo.

    Kumfanya mwenzako awe na furaha ni jambo la muhimu, kwani upendo wa kweli unasimama katika usawa na ulinganifu katika jambo lolote linalohitaji maendeleo yetu kwa malengo ya kila moja wetu.

    Nimefurahi sana sana tena sana, na nakuwahidi hapa utapata maoni kila uwekapo neno kwani nichanzo chakutambua hali halisi inayokubalika katika jamii yetu hii tuipendayo, ya ready know that, i amma peace out i love ya'

    ReplyDelete
  5. Mjukuu, hongera dada yetu, kweli kama alivyotangulia kusema mkuu Mwaipopo, kuwa mwana wa nyoka ni nyoka, na pia naongezea kwa kusemma maji hufuata mkondo...TUPO PAMOJA!

    ReplyDelete
  6. Nakupongeza wewe binafsi, yaani mama Camila kwa kutuletea mwanablog mpya.
    Nasema hivyo kwa sababu kama sio malezi yako mazuri tusingepata huyu mjukuu.

    Namtakia Camila kila la heri katika ulimwengu huu wa Blog.

    Baraka kwenu

    Shaban Kaluse

    ReplyDelete
  7. Yasinta! nasema hivi kama mmeamua kututukana haya nawewe hivyo hivyo na huyo mjukuu wako,kaa! maana natafuta hatakaneno kakujidai nako hola! safi lakini mwanzo mzuri. Kaka S,

    ReplyDelete
  8. Teh, safiiiiiii!Hongera sana na karibu libeneke jipya!

    ReplyDelete
  9. @Kaka S.
    @John Mwaipopo

    Na kweli kabisa mtoto wa nyoka atakuwa nyoka na matusi ya nyoka huwezi kuyaelewa!!

    Yule mjukuu nimegundua ni paparazzo tu. Niulize nimegunduaje?

    Nimejitahidi kwa matumizi ya GOOGLE TRANSLATE na sio mbaya sana kwani pale nimejifunza haya ya fuatao:

    Kama "Bibi" ni Kapulya au Mdadisi (kama wanavyomsifu wengi nami nikamchoka), basi "Mjukuu wake" Bahati ni hatari zaidi! Ila yeye hakugusi wala hakusemi lolote!


    Yule hasemi kabisa. Bali anakulenga tu kwa ile CAMERA yake na UMEKWISHA! Maana yake baada ya kukunasa (bila kukushika hata kidogo) ATAKUPODOA WEEE! ATAKUREFUSHA AU KUKUFUPISHA AKITAKA...MPAKA HUWEZI UKAJITAMBUA TENA WEWE JOHN MWAIPOPO, MANYANYA PHIRI AU KAKA S.!

    Mimi nimemwachia kabisa anuani yangu (EMAIL), na hapo baadaye nitamuomba achukue kabisa picha yangu NA ANIPE NDEVU KWANI "MY GOD" (kama anavyopenda kuandika yeye) KANINYIMA NDEVU!!!!


    Hongera sana, Dada Yasinta! Uzazi halisi ndio huohuo!

    Lakini unisamehe kwani mimi mjukuu nitampa jina la "Paparazzo" na kukuwachia nawe uende "Google Translate" kuelewa maana yake!

    ReplyDelete
  10. @Goodman: teh teh teh teh!

    Hongera Camila kwa kuanzisha libeneke!

    ReplyDelete