Thursday, April 28, 2011

YALE TUYAITAYO MABAYA NDIYO HUTUFUNZA HEKIMA!!!

Hatuwezi kujifunza kupitia mazuri bali tunayoita mabaya, tunayojifunza kwa kusikiliza si kuongea, tunakuwa wema kwa kutoa wema si kutendewa wema. Sisi ni zaidi ya mema na mabaya. Tunatakiwa kuimarisha msuli wa akili si msuli wa Mwili. Na ukweli ni kwamba hakikisha wema wako unashinda uovu.

Ujumbe huu nimetumiwa na Dada Frida Magari wa FAJI. Nami sikutaka nifaidike peke yangu nimeona ni vema niuweke hapa kibarazani ili wengi tufaidike pia kujifunza. Ahsante sana dada Frida.

8 comments:

  1. nami naongeza katika maisha ni bora kutenda wema kwa moyo na si kutenda wema huku ukitegemea kurudishiwa fadhila asante sana kwa ujumbe

    ReplyDelete
  2. Asante da Yasinta kwa maneno mazuri ya kujenga zaidi!

    ReplyDelete
  3. Wewe Yasinta unatoka dunia gani? Mbona kila ukitoa kauli ni uhai mtupu? Ubarikiwe sana, Mwanadada!


    Umekuwa malaika kwa wengi kutokana na nguvu za kalamu yako. Hasa kwangu nakuona malaika.


    Saa iliopita nami nikiwa natangatanga jijini Pretoria kwa matatizo yangu mepya, nilikuwa nawaza: "kwanini maisha yangu Manyanya mie tangu ujana (16) hadi leo... tarehe 4 mwezi ujao (MAY) ninakuwa 50... ni vita tu na vita tupu?"


    Hapo nikakumbuka maneno kuhusiana sana na msemo wako [kujifunza katika shida]...maneno kama haya http://pravstalk.com/pravs-world-gods-cup-of-tea/

    ["WE ARE LIKE TEABAGS, WHOSE STRENGTH COMES OUT WHEN WE’RE PUT IN HOT WATER. SO, WHEN PROBLEMS UPSET YOU… JUST THINK, YOU MUST BE GOD’S FAVOURITE CUP OF TEA!"]


    Yule Mungu amekunywa ujana wote wangu... karibu nimtukane: "..Shenzi TYPE!". Lakini sitayasema hayo Kwake kwakuwa Yeye ni Muumba kwangu na malaika wake kama Yasinta wapo chungu mzima kunikumbusha [yote yanania na mwisho Kwake].

    ReplyDelete
  4. Asante kwa ujumbe

    Uzuri ni kwamba hakuna kibaya bali ni tafasiri na mapokeo ya tukio au suala linalotutokea.

    Wengi tu wagonjwa wa kupenda kuona tunatendewa wema na wengine badala ya sisi kuwa watendaji.

    Kama tutaamua kuona kila kinachotutokea kinatuhusu kwa angalau kwa asilimi 60 na kuwa tayari kuwajibika kwa kinachotokea tutakuwa katika nafasi nzuri ya kutenda mema na kuzalisha mema na kuifanya dunia mahali pema na pazuri pa kuishi

    Kila la kheri

    ReplyDelete