Monday, April 11, 2011

MWENZENU NIMEGUNDUA KUWA!!!!!...............

Inasemekana kuwa kuna tofauti kati ya tembo wa Afrika na tembo wa India(Uhindi) hebu angalia tofauti zao na kufananakwake hapa chini:-


Tembo wa afrika wana masikio makubwa na pembe kubwa.



Masikio yao yanafanana na Ramani yetu ya Afrika!!



Tembo wa India wana masikio madogo na pembe ndogo.



Pia masikio yao yanafanana na Ramani ya India .


Je Uligundua hili wewe pia??



10 comments:

  1. Heee its fun.Ndo najua leo,nilidhani tembo ni tembo tu.

    ReplyDelete
  2. hahaha dada Yasinta unavisa wewe!!yani sikuwa najua wala kuwaza.

    ReplyDelete
  3. Usengili!! kwa kuwa mtafiti wa kina kuhusu wanyama, sidhani wanataalamu waliosomea historia ya wanyama kama waliligundua hilo.Naungana nawe kuna ukweli ukiwaangali tembo hao kwa makini.

    Lakini tofauti nyingine za tembo hao ni kwamba tembo wa Afrika ni weusi na wa India wanarangi kama ya kahaweia pia wahindi huwatumia tembo hao kama farasi,je ni kweli ?.

    Tembo wetu wakubwa wana pembe ndefu,hivyo ni pembe au meno? (Jowayi}.kwa taarifa yako jana watu wanne wa Jijini Dar es salaam wamekamatwa na meno ya ndovu yenye thamani ya shilingi milioni 9 za kitanzania.

    Nakutakia mafanikio mema katika kutujuza kuhusu mambo mbalimbali yaliopo katika dunia yetu.

    ReplyDelete
  4. Wanatafauti hata watalaam wanasema, Tembo wa Africa ni mkubwa na ana masikio makubwa,na ni aina ya Tembo wawili tofauti,na natural hawawezi kuzaliana, labda mpaka kwa njia ya kitalaam,lakini mtoto hawezi kuzaa mtoto mwenzake kwa kuwa hawaingiliani nadhani katika maswala ya gene, ni mfano wa pundamilia na punda wa kawaida, kwa kitalam, mtoto atapatikana lakini hawezi kupata mtoto mwenzak nutural.

    ReplyDelete
  5. KAZI NZURI YA UUMBAJI WA MWENYEZI MUNGU,HAKIKA TUMWACHE AITWE MUNGU...

    ReplyDelete
  6. Hata mimi nilikuwa sijayajua haya...... Nimejifunza kitu....

    ReplyDelete
  7. Tukumbuke tu hata tembo wa AFRIKA hawafanani! Tembo wa kwenye jangwa kama NAMIB kule namibia na wa Kokngo waishio msituni ni tofauti!

    Tembo wa misituni wa Afrika ni wadogo tu kama wa Asia ila nachojua tofauti ni kwamba Tembo wa afrika ni Tembo pori na huwezi kuwafanya farasi au punda kama wa ESHIA.

    Ila ni kweli tembo wa misitu ya Kongo wa MIKUMI Tanzania na WANAMIBIA Jangwani hawafanani hata kiukubwa!:-(

    ReplyDelete
  8. duh! Sikujua kabsaa!

    Wa afrika ni weusi na wa idnia ni wa kaki?

    Aksante kwa elimu!

    ReplyDelete
  9. Unanikumbusa mbuga za wanyama, sijui lini nitafika huko, ...

    ReplyDelete
  10. Ahsanteni wote! mnajua ugunduzi huu nimeupata kwa kuwa na watoto wangu na kuangalia prag. za watoto. Watoto wanajifunza mengi sana ambayo hayta sisi hatukuyajua...Elimu ni kuelimishana..

    ReplyDelete