Wednesday, April 20, 2011

Kwa nini watu wanapima joto kwenye paji la uso??

Mtoto wa kike na kipimajoto mdomoni


Wakati Mwili unapovamiwa na wadudu (bakterie) au virus, kwa kawaida joto huwa linapanda. Hii ndiyo sababu joto la mwilini linaweza kusaidia kugundua kama mtu ni mgonjwa. Wengi watakapo kumpima mtu joto anapojisikia kuumwa wanaweka mkono kwenye paji la uso. Hii yote ni kwasababu tu paji la uso halivaliwi nguo.(Yaani lipo wazi tu na ni rahisi kupima joto kwa haraka)

Kwa vile joto haliwezi kupimwa sawasawa na mkono, kwa hiyo mbinu hii haitoshi. Hivi karibuni kumeanzishwa aina mpya checha za vipimajoto, ambavyo vitaweza kupima joto katika paji la uso. Katika utafiti inaonyesha kwamba joto la paji la uso linayumba na 1,5 C kutoka joto kamili la Mwili. Kwa maana hii njia hii sio nzuri.

Njia nzuri zaidi ni kupima joto makalioni. Pia sikioni au mdomoni. Lakini upungufu ni sawasawa. Ni muhimu/lazima kuongeza nusu C kwa kupata joto kamili.

Chanzo: Illustrerad Vetenskap nr 6/2011

4 comments:

  1. Asante sana da Yasinta kwa kutuelimisha!

    ReplyDelete
  2. Rachel! Elimu hainyimwi ukijuacho basi wagawie na wenzako. Ahsante kwa kupia hapa---

    ReplyDelete
  3. Watoto lakini ni kawaida kuwaweka kipimajoto makalioni kwa ushuhudio wangu! Ila mkubwa mzima na kipima joto kwenye tundu la kalio ni kasheshe aisee! We fikiria Yasinta unaenda hospitalini halafu Daktari anataka akuingize themometa kwenye kalio unafikiri utakuwa na uhuru wa kumruhusu kirahisi?

    ReplyDelete
  4. With havin so much written content do you ever run into any issues of plagorism or copyright violation?
    My blog has a lot of unique content I've either authored myself or outsourced but it seems a lot of it is popping it up all over the web without my permission. Do you know any techniques to help reduce content from being stolen? I'd certainly appreciate it.


    my web page: Paydayloanspup.Co.uk

    ReplyDelete