Saturday, April 23, 2011

KUMBUKUMBU:- LEO UMEFIKA MWEZI MMOJA TANGU ASIFIWE WETU ATUTOKE!!

Leo imetimia mwezi mmoja tangu Asifiwe wetu atutoke!


Ilikuwa tarehe 23/3/2011 mpendwa wetu Asifiwe alitutoka ghafla. Leo tarehe 23/4/2011 imetimia mwezi mmoja tangu atutoke. Familia ya Mzee Ngonyani ipo katika harakati za kufanya arobaini(thelathini) ambayo itafanyika Nyumbani Ruhuwiko-Songea 30/4/2011. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya mpendwa wetu Asifiwe mahali pema peponi amina.

Hapa china nilitumiwa barua pepa na kaka Raymond Mkandawile ujumbe huu ufuatao. Nami nimeupenda ni ujumbe mzuri na nimeona ni vizuri niuambatanishe hapa. Ahsante sana.Ujumbe wenyewe ni huu :-
Duania tu wapitaji na hakuna ajuaye siku yake ni lini. Hivyo hatuna budi kujiandaa na kuwa tayari kila itwapo leo.Dada yetu Asifiwe pumzika kwa amani na sisi pia tunafuta....bwana alitoa na yeye ametwaa jina lake libarikiwe.
Si vibaya kama tukisikiliza na nyimbo hizi ambazo Asifiwe alikuwa akisikiliza sana....

HALAFU HUU PIA ALIUPENDA PIA....

WOTE TWAJUA UMETUACHA KIMWILI LAKINI KIROHO UPO NASI NA TUTAKUKUMBUKA NA KUKUPENDA DAIMA!!!

22 comments:

  1. Najua watu tu tofauti! Lakini kama mimi nimefiwa na kila siku nahesabu ndugu au nimpendaye alifariki lini nahisi mpaka leo ningekuwa nalia sana kila siku kwa kuwa NIWAPENDAO na ndugu wa karibu waliofariki ni wengi na natarajia wengine karibuni kutokana na wauguavyo sasa hivi watafariki nao!

    Nachojaribu kusema ni kwamba kukumbuka marehemu ni poa lakini kuwakumbuka kama kufariki kwao nia kama maumivu tatizo au MUNGU alikosea nayo labda sio poa pia!

    MUNGU walaze peponi kama kuna peponi MAREHEMU!
    Na tufunze kuachia marehemu na kumbukumbu zetu za MAREHEMU kama twawakumbuka ziwe zile tunajua wameenda kupumzika na tusiwe na maumivu yafanyayo kumbukumbu zetu za MREHEMU zinafanya kwamba kama uliamua wafe tusiwe tunaugulia vifo vyao kama vile tuna fikiria ulikosea kazi yako ya kuwafanya wafe MUNGU!

    AMEN!

    ReplyDelete
  2. Nami naungana nawe Dada Yasinta...katika kumkumbuka mpendwa wetu Asifiwe.
    Mungu azidi kumpumzisha kwa amani tele katika maisha ya huko mbinguni. Amina!

    ReplyDelete
  3. Pumzika kwa amani mpendwa wetu,mazowea yanatabu utakumbukwa daima.

    ReplyDelete
  4. sasa nimekuelewa da yasinta,natumai mungu atampumzisha asifiwe kwa amani na nina imani leo tukisherehekea kufufuka kwa yesu amefufuka naye.jina la bwana lihidimiwe amina.

    ReplyDelete
  5. Hakika tulimpenda sana, alkini Mungu amempenda zaidi. Tuzidi kumwombea yeye na wengine wote waliotangulia mbele ya haki. Sote tutafuata.

    ReplyDelete
  6. Pole sasa Yasinta najua jinsi gani inavyo kuuma lakini Mungu atazidi kukupa nguvu na uvumilivu zaidi!

    ReplyDelete
  7. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  8. Hivi ni wangapi hapa waongeao kihuruma ni kweli walikuwa wanamjua ASIFIWE hata kama kisentensi wanaweza kupoza aliyefiwa?

    Nimewaza tu kwa sauti!:-(

    R.I.P Asifiwe!

    ReplyDelete
  9. Ni kweli inauma sana kwani tulimpenda dada yetu Asifiwe lakini Mungu alimpenda zaidi hivyo hatuna budi kukubariana na hilo huku tukimuombea apumzike kwa amani...Amen.
    Mungu na akujalie nguvu na uvumilivu dada yetu Yasinta kwani ni wazi pengo la mdogo wetu kamwe halitozibika.

    ReplyDelete
  10. Ndio Simon Kitururu.

    Kufa ni lazima, maana ilishatamkwa na aliyetuumba mwenyewe. Kila mmoja anawakati wake. So, ni bora kusonga mbele na mambo mengine.

    Vinginevyo tutajikuta tunaendelea kufa kutokana na kuwa na kumb kumb za mara kwa mara.

    Hamjui kuwa maneno huumba?? vyovyote vile utakavyoyatumia, katika kuwaza, kusema n.k.

    Na mtu akisha kufa/fariki kumb kumb zake hufungwa na hana ijara tena maana kama ni hukumu yake ipo sild kwa Mungu mwenyewe kulingana na matendo ya husika.

    ReplyDelete
  11. NaNgonyani (Da' Yasinta), je umeshafika kaburini la marehemu? Au ulikwepo wakati wa mazishi?

    Kama ni "hapana" kwa yote ma suali, basi wewe na Mzee, labda na watoto, mtatakiwa mwende huko alikozikwa ili mukamuage rasmi.

    Wazee huko watakwambieni mfanye nini huko kaburini ili moyo wako utulie.

    Pole sana! (Lakini yule amekwishakuwa mkongwe huko peponi na anakusubiri wewe kwa shangwe kukupokea siku ya kifo chako... nakuomba sana umruhusu aende zake tafadhali).

    ReplyDelete
  12. UKIWEZA, TEMBELEA HAPA: http://www.swahilitruth.com/

    Kuna kitabu kinaitwa:
    "JE WAFU WANAWEZA KUONGEA NASI".

    Pata muda ukisome, kipo ktk hiyo wavuti na unaweza download bure, please.

    ReplyDelete
  13. Tunazudi kumuombea dada yetu Mungu. Mungu ndiye aliyempenda zaidi sisi wote kweli ni wapita njia kila duniani si hahara petu mbali mbinguni kwa baba yetu ndiko makazi yetu yaliko. Ameni

    ReplyDelete
  14. Mzee Simon..nanukuu

    Hivi ni wangapi hapa waongeao kihuruma ni kweli walikuwa wanamjua ASIFIWE hata kama kisentensi wanaweza kupoza aliyefiwa?

    Nimewaza tu kwa sauti!:-(

    R.I.P Asifiwe!

    mwisho wa nukuu.

    ReplyDelete
  15. Ni vyema Dada yasinta tusali na sala zetu tumpelekee Yesu Kristo aliye yashinda mauti,siku ya tatu alifufuka.Roho ya ASIFIWE ikae mahali pema Peponi.Amina.

    Ni matumaini yangu Kumbukumbu hiyo imefanyika Lilambo kwa Nyimbo mbalimbali.Tuko pamoja katika kumkumbuka ASIFIWE.Kumbukumbu yake imeenda sambamba na kumbukumbu ya mateso na kifo chake Yesu Kristo,kwa ajili ya watu wakosao.Tumuombe Bwana amtakase awe safi astarehe ASIFIWE kwa amani peponi.

    ReplyDelete
  16. Mungu atukamilishe ili tukutane paradishe na huyu mpendwa wetu

    ReplyDelete
  17. of your sister, Asifiwe.
    I am deeply sorry. please accept my condolence together with my apology for not contacting you for a long time and not visiting your blog where I would have got the news in time.
    I was so preoccupied with my problems. Sorry a thousand times.
    May Almighty God forgive Asifiwe's and May Almighty God rest her soul in peace.
    njonjo

    ReplyDelete