Friday, March 18, 2011
JAMANI HUU KWELI NI UUNGWANA? KWELI BINADAMU KUFUNGWA KAMBA KAMA MBUZI????
Habari hii imenigusa sana kwa kweli, yaani bado tunaishi miaka ya 1970-1990 sikutegemea kabisa kama mambo haya yatakuwa bado katika ulimwengu huu. Najua ni sehemu nyingi si Afrika tu walikuwa wanaona ni kama laana kupata watoto wenye mtindio wa akili. Nakumbuka nimewahi kushuhudia kwa macho yangu familia moja ilikuwa na mtoto mwenye mtindio wa akili. Walikuwa wakimficha ndani hakuna aliyejua, kama kuna mtoto wa aina hiyo pale nyumbani pao. Siku moja nilipita pale, na nikakutana na mama wa nyumba anampeleka haja kubwa nikamuhoji inakuwaje ndo akanisumulia. Kwa kwa kweli jamii yetu haina ule utu kabisa kwani walikuwa wakiwacheka na mambo mengine mabaya mengi. Lakini kitu kimoja ambacho kimenipa nguvu ni kwamba sio sisi tu. Hata wenzetu nchi zilizoendelea walifanya hivyo walipopata watoto wa mtindio wa akili waliwaacha sehemu maalumu, lakini hata hivyo hawakupata yale maisha ambayo kila binadamu anastahili. Kwa hiyo nachotaka kusema hapa kwa fikra zangu ni kwamba najua kwamba kila binadamu anastahili kupata maisha bora awe mwenye akili timamu au mwenye mtindio wa akili. BINADAMU WOTE NI SAWA. HEBU SOMA HABARI HII HAPA CHINI KUHUSU PICHA HIYO HAPO JUU yenye kichwa cha habari kama ifuatavyo.
HUYU NI MKOROFI NDIO SABUBU ANAISHI KWA KUFUNGWA KAMBA.!!!!?
"... wewe kaka acha tu! huyo ni mkorofi sana hivi ukimfungulia kamba hapa anazunguka mitaa yote ya mji wa Tanga na hapo alipo ana majeraha ya kupigwa na kuchanjwa na nyembe kutokana na ukorofi wake hivi tumeaona njia pekee ni kumfunga kamba na kumchunga kama ng'ombe akiwa malishoni japo na usiku akilala tuna mfunga kamba pale anapolala" alisema mwanamke huyo anayekadiliwa kuwa na miaka kati ya 23 na 25
Hata hivyo anasema mbali ya kufungwa kamba pia kwa upande wa chakula wamekuwa wakimwekea katika sahani yake maalum na kula akiwa amefungwa kamba huku kwa wiki ama mwezi huoogeshwa mara moja.
Alisema kuwa sababu za kufungwa na kutengwa na familia ni kutokana na tatizo hilo la utindio wa ubongo linalomkabili na kupelekea hali ambayo ndani ya familia yao wamekuwa wakiona kama ni aibu kwa kijana huyo kutembea mitaani na tatizo hilo.
Pia alikili kuwa kijana huyo amekuwa na uwezo mkubwa wa kutambua japo hajapata bahatika kupelekwa shule na kuwa sehemu kubwa hata kutamka baadhi ya maneno ameanza kujifunza baada ya kuanzishwa kwa utaratibu wa kumfunga kamba nje ya nyumba hiyo na hivyo kubahatika kujifunza kuongea kwa kusikika kutoka kwa wananchi ambao wamekuwa wakipita eneo hilo.Hapa ni mwanzo tu zaidi inga hapa .
Huu ni mfano mdogo tu, haya yapo sana kijijini, kuna vipofu kazi yao kufungiwa ndani, wakitembea watapotea, fikiri kazaliwa anaishi kwenye giza, na bado anafugwa ndani...
ReplyDeleteNdio maana nasema kiongozi ana dhamana kubwa sana, kwani hili kama kiongozi utaulizwa mbeel ya mungu, utasema ungejuaje? Utajua kwasababu una mjumbe wa nyumba kumi yeye anafanya nini!
Yasinta, nikweli kabisa haya mabo ya kuwaficha walemavu yapo na yanaendlea katika jamii zetu.mimi therapist ( katika psychotherapy nikitumia dance movement) nimegundua mambo mengi,juu ya watu hawa,vidonge to havisaidii kumponyesha mtu huyu.swala la kmbadilisha mtu jisi anavyo fikiri ni tiba muhimu katika kusaidia watu wenye matatizo kamahuyu kijana.kama Therapist,kwanza wazazi wangepata tiba mbadala ya kuwafanya wabadili mtazamo wao juu ya huyu mtoto wao na kumuona nimmoja katika jamii,na siyo aibu katika familia.pili dawa kisha pewa hivyo, ningemuanzishia therapy session nakuanza kumjenga taratibu kisaiklogia mpaka angefika mahali aweze yeye mwenyewe kujitambua.niprpcess lakini kwa uzoefu wangu kijana anaweza kurudi kwenye mstari.kwa hiyo wapo wengi hasa watoto,na watu wazima tu.kumfunga kamba nikumtesa,kumfungia ndani pia ni kosa,najaribu kuangalia sera ya afya ina semaje juu ya walemavu/wasio jiweza,na pia sijuwi kama tuna matherapist Tanzania . kaka s
ReplyDeleteit's so saaaaad,kila mtu anahaki ya kuishi maisha huru jamani,ni unyanyasaji uliovuka mipaka kumfuga mtu kama mnyama.
ReplyDeleteAga gangi, Dada Yasinta,ukweli unabakia pale pale wa kukosa huruma,wazazi hao wanadai kumfunga kamba mtoto wao kwa ajili ua utundu,hivyo utundu aliyokuwa nao huyu mtoto una uhusiano gani na kuacha kumwogesha.
ReplyDeleteIsitoshe kunashule za watoto wenye mtindio ambao wanafanya mambo ya ajabu kumshinda yule mwenye akilitimamu.
Kuna michezo ya Olympic ambayo wao wana fanya vizuri kwenye mashindano ,mf.shule ya msingi mfaranyaki songea.
Mimi nafikiri kumfungia siyo dawa, kwani anakosa uhuru ndiyo maana akipata nafasi anatoroka. Mwisho wa siku akipata upenyo na kufungua hizo kamba, Hatorudi kwani tabu zimemzidi kuliko raha,kwani anaumia ebu tujimjaribu huyo mama kumfunga kwa saa moja tuu aone.Na kutenga kwenye chakula kukosa kuoga je navyo vinaingiliana vipi!!.
ReplyDeletehabari hii inasikitisha sana dada Yasinta, ngoja niende Kanisani, nikirudi nitaweka mtazamo wangu
ReplyDeleteInasikitisha sana !
ReplyDeleteLakini tusihukumu wafikiao kufunga kamba vichaa au hata kuficha wenyevifafa!
Jamii imechangia sana kufanya watu wafanye hivi na fuatilia historia utastukia.
Najua kuna makabila kama WAPARE sisi ilikuwa familia yako ikijulikana ina vichaa / wenye mtindio wa akili au hata wenye vifafa au tu mazeruzeru ,..
... iliwezekana kufanya ukoo wenu mzima upate tabu kuozesha mtu au hata kuoa kwa kuwa jamii ile ya wazee kuchunguza ukoo kabla hawajakuchagulia mke ilikuwa ni moja ya dondoo inazinukuu ili kukwepa watu na haki ya nani hata kama mzuri vipi kama kwenu kuna wenda wazimu au wenye vifafa na tukiachinia mbali kuwa hata watoto mapacha walikuwa wanachukuliwa kama nuksi- nyie ukoo wenu na wewe mwenyewe unaweza kukwepwa kama vile sijui nini .
Na tukumbuke ustawi, SERIKALI ,ndugu hata ELIMU NDOGO ya HAYA MAMBO katika jamii haisaidii kihivyo.
Kumbuka kuna mambo mpaka ya kukute ndio unaweza kuelewa vizuri ni jinsi gani watu wanafikia kufunga kamba mtu.
Kabla hujahukumu mtu tembelea viatu vyake katika yake uone .
Kuna wengi hapa watafunga mtoto au kuficha mtoto kwa kuwa najua wengi tu WASOMI kabisa ambao wanadiriki kutolipa ada ila kuchangia harusi za jirani na KICHENI pati kwa ajini ya kuficha uso na kujifanya mambo shwari.
Sasa kama presha za michango ya HARUSI na KICHENI pati zinafanya watu wajibaraguze hivyo kuficha aibu kuwa kuna kibano ,...
...unafikiri ila kuepuka aibu ni mangapi wanaweza kufanya kama wanamtoto MWENDAWAZIMU ambaye anaharibu statasi zao mtaani?
Na pia baadhi ya wenye mtindio wa akili ni hatari kwa kuwa hawajui baya wala zuri na kama wewe inabidi ndani ya siku uhangaikie mpaka kuuza maandazi yako ili kieleweke hata katika mipango ya msosi ,..
... usishangae ukafunga mtu ambaye hatabiriki hasa kama unajua ukimuachia huru hujui atakachofanya.
Ni wazo kwa sauti la chapuchapu!:-(
yoooote !!!!!! tisa kumi mi nafikiri kilichotawala hapo ni ukosefu wa huruma ya kibinadamu pia kitu kingine ni uvivu wa kupindukia kuna mtu hapa duniani anjua kuwa akilima lazima avune??? chochote chaweza kutokea na watoto ni hivyo ukiwa na bidii ya kumtunza nikiwa na maana ya kumsikiliza mwanao lazima mambo hayatakuwa yalivyo hasa mama unashindwa kuelewa zawadi aliyokupa Mungu uitunzeje!!!! kwa kusikiliza wataalamu hapo wala pesa haihitajiki wamama tumesahau uchungu tulioupata wakati wa kujifungua unamfunga mwanao kamba ! wewe unakwenda wapi?ukimpenda mwanao na wengine watampenda ukimwelekeza vizuri mwanao na wengine watafanya hivyo.
ReplyDeleteobat cytotec i think your blog very informative obat penggugur thanks for sharing obat telat bulan
ReplyDelete