Wednesday, March 9, 2011

HII NI KAZI YA NANI??

Naona ni siku nyingi hatujasimuliana hadithi na leo nimeona ni wakati mzuri niwasimulia kahadithi haka:-Hadithi, hadithi….


Mmhh! ngoja kwanza nikune kichwa!!


Hii ni hadithi kuhusu watu wanne waitwao Kila mtu, Mtu, Mtu na Hakuna mtu. Kulikuwa na kazi muhimu kufanywa na kila mtu alikuwa na uhakika kila mtu angeweza kufanya kazi hiyo. Kila mtu angefanya kazi hiyo, lakini Hakuna mtu alifanya hivyo. Mtu alipata hasira kuhusu hili, kwasababu ilikuwa ni kazi ya kila mtu. Kila mtu aliwaza kuwa Kila mtu anaweza kufanya hivyo lakini Hakuna mtu aliyetambua kwamba kila mtu asingefanya hivyo. Na mwisho iliishia Kila mtu kumlaumu Mtu wakati Hakuna mtu aliyefanya chochote ambacho Kila mtu angeweza kufanya. ……mwisho wa hadithi!!!!

14 comments:

  1. Umependeza kabinti ka kingoni.kwakweli hii ni kazi ya kilamtu,japo kuwa kila kitu lazima kiwe na mwanzilishi.hivyo ni jukumu letu lako wewe kama mtu kuwajibika pale ulipo kwa faida mtu.nimemependa sana fasihi hii uliyo tumia,na nafikiri wengi wana zuoni watakuna vichwa vyao juu ya mtu mimi . kaka s

    ReplyDelete
  2. Kweli hata mimi nakuna kichwa nikiwaza mengi...`kulaumiana' inakua ndio jadi, na ndio maana kuna ile hekima ya vidole, kuwa wakati unamnyoshea mwenzako kidole kwa nia ya `kumlaumu' au vyovyote iwavyo, ujue yeye unamnyoshea kidole kimoja, lakini angalia vingapi vinakuelekea wewe
    HEKIMA. Ni kuwa kwanza angalia nfasi yako kuwa umewajibika kiasi gani, huenda tunacholaumu kinatokana na `udhaifu wetu wenyewe'
    Dada Yasinta, sijui nimepatia au nimetoka nje ya hadithi ...AU TUKUPE MJI

    ReplyDelete
  3. dah...Yasinta haka ka stori kanafanana na zile picha za illusion...au tuseme ni Illusion story. Ni story fupi iliyonichukua muda kidogo kuimaliza..

    haya tupe stori zaidi

    ReplyDelete
  4. MWANAFALSAFA nimekubali hii kitu maana imenifanya niandike kwenye kitabu cha kumbukumbu

    ReplyDelete
  5. Waooo!!!!! nimeamini kuwa wewe ni mbunifu. So creativity and intelligent. I love your work of art Mwaaaaa!!

    ReplyDelete
  6. hiyo kazi ilitakiwa ifanywe na MIMI. Tukiondoa fikra za kutaka kufanyiwa jambo na binadamu mwingine na kufanya sisi wenyewe ama mimi mwenyewe tutaongeza mafanikio. hao (mtu, mtu mwingine nk) ndio chanzo cha kuchelewa na kudorora kwa mambo mengi.MIMI kwanza, mwingine baadae.

    ReplyDelete
  7. umependeza yasinta hadithi nzuri inafunza na chemsha bongo.

    ReplyDelete
  8. Nimependa staili yako pichani ya kukuna kichwa!

    ReplyDelete
  9. Habari Dada Yasinta. Hiyo SWEDEN vile umeandika hapo nini unamaanisha?

    ReplyDelete
  10. Ni hadithi nzuri na inamafundisho ndani yake
    Kwa kutegemea wengine watawajibika kwa jambo linalokuhusu hata kama ni la kijamii na kuona kama hauhusiki mwisho wake huwa majuto na kulalamika na kulaumu.
    Tunatakiwa kufahamu kuwa muwajibika wa kwanza katika kila jambo ni mimi kwa maana mtu mmoja mmoja na kwa kufahamu hilo mambo yatakwenda vizuri,pia kama hasa sisi watanzania tutawajibika kila mmoja katika nyanja yoyote ili ya maisha kwa asilimia si chini ya 60 na wengine wakawajibika kwa silimia 40 zilizosalia akiwemo muumba tutafanya mambo makubwa. Mimi huwa mara nyingi naamini kuwa kuna ishara nyingi zinazotuonyesha tunatakiw akuwajibika si kwa chini ya asilimia 60. Mfano unamnyoshea kidole cha lawama hata wanentu mara nyigi vidole viwili kidole gumba na kidole cha kwanza baada ya kidole gumba ndivyo vinvyoelekea kwa unamuonyesha na vitatu huwa vinakuonyesha wewe. Hata kwa makabila ambayo huwa wanajiapiaza mfano wapogor hupenda kusema mungu wangu aliyejuu na kuonyesha vidole viwili kuelekea juu mbinguni na vitatu kuonyesha chini usawa wa kichwa cha huyo anayejiapiza.

    ReplyDelete
  11. Habari
    Nimesoma maoni ya wasomaji kuhusiana na hadithi uliyoitoa, bado tuna kazi ya ziada katika kuhakikisha tunatumia vipaji tulivyonavyo kwa faida yetu na jamii inayotuzunguka. Nimefurahishwa na maoni ya mwaipopo na mwingine ambaye hakutaja jina yanamafundisho ndani yake na kuleta udadisi.

    Nakupongeza kwa kutoa changamoto mbalimbali kupitia katika blog yako na kwa kupitia blog yako tunajifunza na kujielewa sisi watanzania tulivyo.

    ReplyDelete
  12. Za siku tele,
    Hapo unawazaaa sijui umetunga? ila ipo bomba sana

    ReplyDelete