Monday, February 21, 2011

HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA KWAKO CAMILLA !!!/Grattis på Födelsedagen Camilla!!!

Miaka 13 imepita leo tangu binti yetu Camilla azaliwe. Ni binti ambaye anapenda sana kusoma, kuandika, kucheza mpira wa mikono (handball) anapenda michezo ya kuigiza na kuimba. Twakuomba Mwenywezi Mungu uwe /uzidi kumbariki binti yetu Camilla azidi kuwa kama alivyo. Na pia twakuomba uzidi kutupa sisi wazazi/walezi nguvu ya kumlea ili azidi kuwa binti mwema na mwenye busara. CAMILLA HONGERA SANA KWA SIKU YA KUZALIWA.!!!!!
na hapa ni mziki ambao napenda kusikilizakwa hiyo leo ni siku yangu na nataka kusikiliza pamoja nanyi



.

16 comments:

  1. Siku zinaenda jamani, ni juzi tu tulisherehekea miaka 12, leo ushakuwa teenager, furaha iliyoje?

    Hongera sana kwa siku yako hii maalum, Mungu azidi kuwa nawe akubariki kwa kila jambo zuri uliombalo kuwa, awabariki na wazazi wako pia ili waweze kukutunza vizuri hadi hapo utakapoweza kujitegemea mwenyewe.

    **Yasinta please tuongezee picha za akiwa uwanjani anacheza mpira na nyinginezo za vitendo...

    Enjoy your day my daughter!!!!!!!!
    Happy Birthday.

    ReplyDelete
  2. Hongera Camilla!



    Nje ya tundu:

    -Hivi Camilla maana yake ni nini?

    ReplyDelete
  3. Hongera Camilla,God bless you and long live

    ReplyDelete
  4. Uzidi kukua na kujazwa busara na utu wema Camilla!

    ReplyDelete
  5. "Ni binti ambaye anapenda sana kusoma, kuandika..."


    Basi 'tumekwisha'! (LOL)


    Yupo Mzee mmoja naye alizaliwa siku ya leo:Miaka 87 iliyepita. Enzi zake za ujana naye ["alipenda sana kusoma, kuandika..."]


    Kwaruhusa yako Mkuu Yasinta acha niseme:


    "Hongera kwenu wote wawili Camilla Klaesson (21 February 1998-)...


    "...na Robert Gabriel Mugabe (21 February 1924-)!"


    Tupe basi, Mkuu Yasinta kwa lugha ya kikwao hiyo "HAPPY BIRTHDAY", tafadhali.

    ReplyDelete
  6. Hongera Camilla!

    We Mt, acha kuuliza maswali mengi juu ya maana ya hilo jina kwa kuwa utapata majibu ya kuchekesha...kwani ukilitamka jina huko kwetu watu hawatakuwa na mbavu...lol!

    Ni vijimambo tu!

    ReplyDelete
  7. @Mtu aliyenitonya chobi:

    Nanukuu

    ``mzima wew?
    nimesoma maoni yako unataka kujua maana ya jina Camilla
    je jina lako lina maana gani???´´


    Mimi: ```Simon maana yake ni : to hear ; au to be heard. Ila mama alilichgua kwa kutaka lieleweke kama.The one who will be heard´´


    Mtu:``hakuna maana ya kiswahili?´´


    Mimi: ``nadhani To hear kwa kishwahili ni : Kusikia.
    to be heard: Atakayesikilizwa.

    The one who will be heard. Ambaye atasikilizwa.``


    @Kadinali CHACHA:

    DUH! Nakumbuka huko kwetu MUSOMA kuna yule Rais wa Zambia F. CHILUBA ilikuwa tatizo kumzungumzia kwa jina.:-(

    ReplyDelete
  8. Happy birthday uncle!! Mungu akujalie heri na afya tele uendelee kuwa faraja ndani ya mioyo ya wazazi wako! UJUMBE: waheshimu baba na mama upate miaka mengi na heri duniani...!

    ReplyDelete
  9. Oh wow!cute girl!hongera sana Camilla kwa siku yako ya kuzaliwa,mungu azidi kukuongoza utimize ndoto zako,hongera sana pia kwa wazazi kwa malezi bora,Yasinta ongeza picha please!!!!!mimi nasubiri cake yangu Camilla usininyime.
    Happy birthday and have a lovely, lovely day, enjoy!xxxx.

    ReplyDelete
  10. 'ongela' mwanakwetu KAMILA. Ukubwa haupigi hodi.

    ReplyDelete
  11. Hongera sana Camilla katika siku yako ya kuzaliwa.Jamani miaka inakimbia juzi juzi tu tulikupongeza.....

    ReplyDelete
  12. HONGERA SANA MJOMBA CAMILA, kwa bahati mbaya sitakuwa na mengi ya kusema kwa kuwa niko ugenini Arusha na mtandao huku unasumbua

    Mjombako Shaban kaluse

    ReplyDelete
  13. Ndugu, jamaa na marafiki wote kwa niaba ya Camilla ninachukua nafasi hii kuwashukuruni wote kwa kumtakia kheri katika siku yake ya kuzaliwa na pia maisha yake. Mwenyezi Mungu azidi kuwa nanyi wote. Ahsanteni sana.
    Yasinta/Camilla

    ReplyDelete