Sunday, January 30, 2011

NI JUMAPILI YA TANO NA YA MWISHO YA MWEZI HUU NAWATAKIENI JUMAPILI NJEMA!!!

Katika jumapili hii ya mwisho na ya tano ya mwezi huu basi nimeona tuimalize kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa sala hii :- SALA YA MKE KUMWOMBEA MUMEWE Ee Bwana , ni ajabu, Jinsi fikra zangu zinavyomrudia kila mara Huyu, mume wangu, Mwenzi anayeshiriki maisha yangu kwa namna ya pekee. Ninapofagia nyumba na mazingira yake, Nataka kutengeneza nyumba nzuri kwa ajili yake. Ninapopika chakula vizuri,Napenda kumfurahisha. Ninaponunua nguo mpya na kujaribu kuonekana mrembo, Ni kwa ajili yake tena, Ee Bwana. Na ninaweza kukuambia kwamba Ninamwonea fahari, Anafanya kazi kwa bidii ili kupata riziki yetu; Ni mtu mwenye haki, mwadilifu, Naye hujitahidi kutufurahisha. Kwangu, yeye ni mpole na mwangalifu. Hunijali na kuonyesha kweli kwamba anajali. Hunifanya mimi nijiamini mwenyewe, Anajua jinsi ya kuondoa hofu zangu, Hunipatia usalama na upendo ambao nahitaji sana. Ee Bwana, ninakuomba, Umbariki na umlinde. Katika safari zake, umfikishe salama. Kazini mwake, umpe fanaka Na hapa, nyumbani petu naomba apate amani na heri. Bwana, unisaidie mimi pia Niweze kuwa yule mke anayehitaji. Unifanye niwe mtu anayeweza kumwamini daima, Mwanamke ambaye anaweza kumfurahia, Niweze kumsaidia asahau matatizo yake, Niweze kuondolea mbali hofu zake na kupunguza uchungu wake. Bwana, Wewe ndiwe uliyenipa mume huyu, Na katika yeye,Umenipatia sehemu ya nafsi yako mwenyewe. Ninakusifu kwa ajili yake, Ee Bwana.

8 comments:

  1. Amen.
    Ninaimani sala hii imeunganisha wanawake wote wa Tanzania kwa waume zao. Ubarikiwe Dada pamoja na familia yako.
    Ulipo ishia naongezea tena;
    EE mungu uliye wa rehema wajalie waume zetu wavishinde vishawishi vya mwovu shetani, uwajalie wenye ugomvi wapatane,wasiojali familia zao wazikumbuke,walioachana warudiane,hatimaye furaha yao iwe matunda ya kukutukuza wewe daima na milele.

    ReplyDelete
  2. Dada yangu mbona kama ni Jumapili ya 4, jumapili ya tano ni ijayo. Au mimi ndo nakosea?

    Basi nikutakie jumapili njema sana wewe na familia yako.

    ReplyDelete
  3. Dada Yasinta, Dhehebu gani hilo la kuwafundisha wake zetu kutupenda kiasi cha kutuombea namna hiyo? NATAKA NIENDE NIKAJIUNGE!

    ReplyDelete
  4. Ahsanteni wote kwa kuwa pamoja daima. Kaka Goodman mimi dhebu langu ni KATOLIKI!!

    ReplyDelete